Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

Ni Wakati Upi Ambapo Mama Hapaswi Kufanya Ngono Akiwa Na Mimba?

Kufanya tendo la ndoa ni muhimu kwa mama mjamzito. Ila kuna wakati ambapo sio salama kwake wala kwa mtoto. Tazama wakati wa kuacha ngono katika mimba.

Wanawake wajawazito na wachumba wao mara kwa mara huwa na shaka ikiwa ni salama kwao kujihusisha katika tendo la wanandoa. Ni wakati wa kuacha ngono katika mimba ni upi? Je, huenda kitendo hiki kikasababisha kuharibika kwa mimba? Mitindo yote ya ngono ni salama kwa mwanamke mwenye mimba?

Je, mama mwenye mimba ako salama kufanya ngono?

wakati wa kuacha ngono katika mimba

Kufanya mapenzi ni asili kwa wanandoa. Mwanamke huenda akapata hamu zaidi ya kufanya mapenzi akiwa na mimba. Ni salama kwa wanandoa kujihusisha katika kitendo hiki bila hofu ya kumwumiza mtoto. Hii ni kwa sababu mtoto amezingirwa na amniotic fluid inayo mlinda.

Wanawake pia huwa na hofu kuwa kufika kilele kutawafanya waanze kuhisi uchungu wa uzazi kabla ya mimba kukomaa. Kubanwa kwa uchungu wa uzazi ni tofauti na kufika kilele wakati wa tendo la ndoa. Ni vyema kwa wanandoa kutumia kinga ama kondomu wananpo fanya mapenzi ikiwa mwanamme ana zaidi ya mchumba mmoja. Kupata maambukizi ya ngono ni hatari kwa mama mwenye mimba pamoja na mimba. Huenda yaka sababisha kuharibika kwa mimba.

Tendo la ndoa katika ujauzito hubadilika?

Naam, tendo la ndoa katika ujauzito na bila ujauzito huwa tofauti. Hamu ya tendo la ndoa huja iki fifia, na ni kawaida kwa hivyo usiwe na shaka unapo shuhudia hili.

Wakati usio salama kwa wanandoa kufanya ngono

wakati wa kuacha ngono katika mimba

Kwa wanawake walio na mimba isiyo salama, ni muhimu sana kuwasiliana na daktari wao na kujadili kuhusu mimba salama. Tazama wakati ambapo sio salama kufanya ngono katika ujauzito.

  • Mama mwenye mimba isiyo salama
  • Wanawake walio na mimba ya watoto mapacha ama zaidi
  • Mwanamke aliye katika hatari ya kupoteza mimba ama mwenye historia ya mimba kuharibika
  • Mama aliye na hali ya placenta previa
  • Kwa mama ambaye amniotic fluid yake imeanza kudondoka
  • Mama mwenye hatari ya kujifungua kabla ya wakati

Fuata maagizo ya daktari wako kwa makini. Anapo kushauri ukome kufanya tendo la ndoa, huo ndiyo wakati wa kuacha ngono katika mimba. Ili mimba yako isiwe na matatizo.

Soma Pia: Kutengeneza Uhusiano Na Mtoto Ukiwa Na Mimba Na Manufaa Ya Kiafya

Written by

Risper Nyakio