Wamama 11 Mashuhuri Nigeria Wanao Tuonyesha Jinsi Ya Kuwa Mama

Wamama 11 Mashuhuri Nigeria Wanao Tuonyesha Jinsi Ya Kuwa Mama

Je, ungependa kujua utakako pata vidokezo vya urembo, afya, mapishi na ulezi? Tuna orodha ya wamama mashuhuri Nigeria ili kurahisisha kazi yako. Maisha yao yanakuonyesha maana ya kuwa mama katika nchi ya Nigeria na kufuzu katika jukumu hili.

wamama mashuhuri Nigeria

Sisi Yemmie. Chanzo: Onobello

Wamama Mashuhuri Zaidi Nchini Nigeria

1. Tinuke Atilade

wamama mashuhuri Nigeria

Tinuke Atilade of OliveTree Kits.

Mama huyu wa Nigeria Tinuke Atilade ana ongoza OliveTree Kits, mavazi ambayo yanatoa utunzaji kwa wamama wenye mimba. Anahitaji nafasi kwenye orodha hii kwa sababu ana njia iliyo na mafanikio ambayo wamama wa Nigeria wanakusanyika na kuongea kuhusu ulezi. Unaweza soma mengi kutoka kwake kupitia kwa kurasa yake ya Instagram.

2. Daisy Parenting

Kurasa inayo milikiwa na Daisy Umenyiora, Daisy parenting sio kurasa ya Instagram iliyo shida tuzo tu. Ni chanzo bora kwa wazazi wanao wataka watoto wao wafuzu kwenye masomo. Ana tumia hadithi kudhihirisha maoni yake kwa watu wachanga ili waelewe.

Iwapo ungependa ushauri na vidokezo vya ulezi, fuata kurasa ya Daisy.

3. Parenting by Design

Kurasa ya Parenting by Design ni ya kipekee kufuatia mtindo wake na maono yake. Kocha wa ulezi Ijeoma Uba ndiye akili nyuma ya kurasa hii. Ana vyeti vya walimu na kukuza nidhamu na uleaji wa Kimungu. Kulingana na yeye, kila mzazi ni ajenti wa Mungu.

Fuata vidokezo vingi vya ulezi, kuhamasishwa, ushuhuda, bidhaa na ushauri wa kimasomo. Yote haya utapata kwa kufuata kurasa ya Parenting by Design on Instagram.

4. Wives and Mothers

Wives and Mothers iko katika orodha yetu ya wamama mashuhuri nchini Nigeria kwa sababu ya umaarufu wa kurasa hii. Mama mashuhuri huyu ana angazia kuhakikisha kuwa kuna jamii salama kwenye mitandao ya kijamii. Ni aina gani ya utegemezi ambao wamama na mabibi wanaweza pata kwenye mtandao?

Mama huyu wa Nigeria anawaelimisha, kuwapa vidokezo, kuwa hamasisha na kuwa burudisha. Mada zina tofautiana kama vile afya, utamaduni, haki na zinginezo. Zina saidia wamama kupata shepu walio kuwa nayo hapo awali kabla ya kujifungua na kunyonyesha.

Je, ungependa ndoa na kazi yako ipae? Fuata kurasa hii ya Wives and Mothers on Instagram.

5. Fabmumng

mom in nigeria

Jayne A. of Fabmumng. Chanzo: fabmumng.com

Jayne A., ndiye akili nyuma ya kuruasa hii ya ulezi, na ni mtetezi mkuu wa utunzaji bora wa wamama. Ana amini kuwa kujitunza sio kuwa mchoyo. Unaweza mfuata kwenye mtandao wa Instagram.

6. Blazers & Baby | Career Mum🇳🇬

Kurasa hii ina ongozwa na Osemhen Okenyi, ni bora kwa wamama walio na kazi wana taka kupepea katika kufanya kazi na ulezi. Wanawapatia wamama vidokezo vya kufuzu katika kazi yao na maisha.

Pata ushauri wa kitaalum kutoka kwa wataalum. Soma kutoka kwa wamama ambao wamepitia mambo sawa. Wamama wanao fanya kazi duniani kote wanasoma kuhusu lishe, mimba, mitindo na mambo tofauti kuhusu kazi na kuwa mama. Bonyeza hapa kuangalia kurasa yake ya Instagram.

7. Sisi Yemmie

Mama mwenye watoto wawili Yemisi Odunsanya alianza kurasa yake ya afya na mitindo miaka michache iliyo pita. Ila imekuwa chanzo cha kupata vidokezo vya ulezi, urembo na zaidi. Hakuna njia ya kutengeneza orodha ya wamama mashuhuri bila kuhusisha jina Sisi Yemmie. Chukua muda uangalie kurasa yake ya Instagram!

8. Tito Idakula

Watu wengi wanajua Tito kama bibi ya mwimbaji Bez Idakula, ila yeye huvalia kofia nyingi. Hivi karibuni, alichapisha kitabu chake cha ‘Royalty’ kinacho elezea kuhusu safari yake ya mimba na kifo cha mtoto wake wa kwanza. Na sasa yeye ni mama wa wawili, wafuasi wake wa Tito’s Instagram  wanamjua kwa kupatiana vidokezo jinsi ya kuwalea watoto wanao mwogopa Mungu.

9. Adorable Mums

Odira Okwuagwu ni mama mwenye fahari ya watoto wake wawili. Kikundi chake cha Facebooke cha Adorable Mums kina ma-elfu ya wafuasi. Ni mahali ambapo wamama wanapata vidokezo vya ulezi na kupata ushauri kutoka kwa wamama wengine. Pia iwapo mama ana shaka zozote kuhusu watoto wake, anapata maelezo na ushauri kutoka kwa wengine. Bila shaka, anastahili nafasi ya kwanza katika orodha ya wamama mashuhuri nchini Nigeria.

10. Diary of an Abuja Mum

Diary of an Abuja Mom inafuata maisha ya mama wa kukaa nyumbani wa Abuja. Jinsi anavyo ishi maisha yake na vidokezo vya ulezi na wamama kutoka duniani kote.

11. Nafasi ya mama

Kama jina linavyo sema, hii ni nafasi ya mama wa karne hii wanao hitaji vidokezo muhimu vya ulezi. Wamama wa mara ya kwanza na wanao kuwa wazazi peke yake na kila mama Nigeria wana weza kusanyika kuwa na mjadala kuhusu changamoto zao na raha zao.

Siku ambazo wamama walijiachilia zimeisha. Siku hizi, wamama hufanya vingi wawezavyo kuhakikisha kuwa wana pendeza, uzito wao wa mwili uko sawa na pia nguo zao ni za hivi sasa.

Iwapo unapenda kuvalia nguo za mitindo ya kisasa, tizama kurasa hii ya  The Mum Zone.

 Fikira za mwisho kuhusu wamama mashuhuri nchini Nigeria

Siku ya mama ina sherehekewa siku tofauti katika pande tofauti duniani ila siku ya mama ni kila siku. Tuliangazia picha na hadithi za wamama 11 wa Nigeria ambao mitindo yao inawahamasisha wengine kufanya zaidi maishani. Kuna urembo mwingi na nguvu katika kuona wanawake wakifanya kazi, kulinda nyumba na watoto wao na bado kutimiza malengo yao duniani. Hasa wanao kuwa na biashara zao.

Tazama makala haya ya wamama mashuhuri nchini Nigeria na kuwa hakika kuhakikisha kuwa unatuambia jinsi unavyo hakikisha kuwa unafanya kazi zako na majukumu yako kama mama.

Pulse NG

Soma pia: Profitable work from home jobs in Nigeria for moms

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio