Wamama Hawa Wa Mashuhuri Wa Kenya Wanafanya Ulezi Uonekane Rahisi Zaidi

Wamama Hawa Wa Mashuhuri Wa Kenya Wanafanya Ulezi Uonekane Rahisi Zaidi

Ulezi ni mojawapo ya safari za kupendeza zaidi na pia zenye changamoto zaidi. Hasa katika dunia hii ambapo kuna majukumu mengi yaliyo twika kwenye mbega za mama. Huenda ukapata kuwa baadhi ya wamama wanafanya majukumu yote peke yao, kuwa lea watoto wao bila kuwepo kwa bwana yao. Kuenda kazini kutafuta pesa za kuichunga familia na kadhalika. Na sio wakati rahisi kwa wamama hawa. Pia kwa walio na mabwana zao, sio wakati rahisi ila wanajikaza. Kuenda kazini, kuwa mama na kuwa bibi na kufanya majukumu yote ya nyumbani. Katika makala haya, tuna angazia baadhi ya wamama mashuhuri wa Kenya walio wazazi na ambao wanafanya ulezi na kuwa mama ionekane rahisi zaidi. Ili kuwashawishi wamama wengine kuwa hawako peke yao na haijalishi wanacho pitia kwani kuna wamama wengine walio pitia na wanakazana kuhakikisha kuwa familia zao na watoto wao wako salama kabisa.

Wamama Mashuhuri Wa Kenya: Wanao Wahamasisha Wamama Wengine

1. Size 8 Kenya

Size 8 ambaye ni bibi yake Dj Mo wamekuwa kwa ndoa kwa muda wa miaka zaidi ya sita. Wamebarikiwa na watoto 2. Msichana na vijana, anaweza kufanya majukumu yake kama mama, mke, mwana muziki na mwana biashara. Kulingana na size 8 ambaye ana mwamini Mungu. Anasema sio rahisi, ila ukimwamini Mungu anakusaidia kufanya mambo yote. Pia anawashauri wanaume wawasaidie wanawake wao kwani mwanamke huwa na majukumu mengi na lazima bwanaye awe naye katika wakati huu, hasa baada ya kujifungua. Hivi majuzi wame weza kuanzisha kipindi chao cha 'Dining With The Muraya's' ambacho ni kipindi wanacho eleza kuhusu maisha yao ya kila siku kuhusu ndoa.

Wamama Hawa Wa Mashuhuri Wa Kenya Wanafanya Ulezi Uonekane Rahisi Zaidi

2. Betty Mutei Kyalo

Betty Kyalo ni mojawapo ya sura zilizo maarufu zaidi kwenye televisheni zetu hapa Kenya. Kwa muda mrefu sana, Betty amekuwa akionekana kwenye runinga zetu kama msomaji wa habari za saa tatu. Amefanya kazi kwa kampuni nyingi za habari ikiwemo K24 na KTN. Bila shaka anawapendeza wengi na kuwatia wamama wengi nguvu. Sio kwa kazi yake tu ila hata katika jukumu lake la kuwa mama. Ni mama wa msichana mmoja kwenye jina Ivaanna. Mwaka ulio pita hasa haujakuwa rahisi sana kwake kwani bintiye alikuwa amelazwa hospitalini kwa muda wa miezi minane. Ila, hakuwahi kosa kwenda kazini, alijikakamua na kusawasisha majukumu yake kama mama na bado mfanya kazi. Kwa kweli Betty ni mtu wa kutazamiwa na watu wengi, wazee kwa wadogo. Na unapo kuwa na matatizo katika ulezi wako, angalia maisha ya Betty Kyalo na utapata uhamasishaji unao hitaji kuendelea.

3. Akothee Kenya

Akothee ni mojawapo ya wanawake walio tajiri zaidi. Katika mwaka wa 2015. Akothee aliibuka kama mwanamke tajiri zaidi Kenya. Ana kampuni yake ya ziara na matembezaji inayo julikana kama Akothee Safari's. Mbali na hayo, yeye ni mwimbaji anaye tambulika Kenya, Afrika Mashariki na duniani kote kupitia nyimbo zake za kusisimua. Mbali na hayo, yeye ni mama kwa watoto watano. Na cha zaidi ni kuwa anawalea peke yake. Sio rahisi kwake, ila tuna furahia kuona anavyo wakakamua wamama wengine kupitia kwa kurasa zake za kijamii na kuwa hamasisha kuto tegemea wanaume ila kufanya wawezavyo kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata vitu vyote wanavyo hitaji. Hili linaonekana kwa njia aliyo walea watoto wake hasa wasichana ambao wamekua. Wanatamba katika tasnia walizo amua kufuata maishani. Kama vile Rue baby ambaye ni 'model' na kifungua mimba wake aliye mzawadi cheo cha mkurugenzi mkuu wa kampuni yake ya Akothee Safari's. Bila shaka tuna ona kuwa amewalea mabinti wake kwa njia inayo faa na wamekuwa wanawake wenye juhudi na wafanya biashara. Jambo ambalo ni la kuigwa na wanawake wengine.

wanawake mashuhuri wa kenya

4. Wahu Kagwi

Wahu ni bibi yake Nameless Kenya, na familia yao inajulikana kama 'The Mathenge's'. Wote ni wasanii wanao watumbuiza watu Kenya kwa ngoma zao kutoka miaka ya 2000. Wanapendwa na watu wengi kufuatia jinsi wanavyo ishi maisha yao. Hata kama kila mtu anajua familia yao, hakuna anaye jua kinacho endelea katika familia yao. Wahu ni mama wa kufuatwa kwani amekuwa mama mzuri katika ulezi wa watoto wao wawili ambao wote ni mabinti. Mbali na kuwa mama, mke, na mwimbaji, yeye pia ni mfanya biashara. Nguvu zake katika kusawasisha yote haya ni ya kuigwa. Anapendwa sana na bila shaka unaweza soma mawili matatu kutoka kwa njia yake ya ulezi.

wazo yetu ya mwisho kuhusu wamama mashuhuri

Kutoka kwa wamama hawa, tuna soma kuwa, kuwa mama hakuna maana kuwa haupendezi wala kuvalia nguo za hivi sasa. Kuwa mama ni safari ya kupendeza na unapaswa kupendeza wakati wote. Pia, afya ni jambo la maana kama tunavyo ona kwani wengi kati ya wamama katika orodha yetu wana fanya mazoezi ili kuhakikisha wana afya na wana ishi kwa muda mrefu ili waweze kuwaona watoto wao wakikua. Hakikisha kuwa unafanya mazoezi, kupunguza uzito na kuwa na afya. Pia ni muhimu kwa kila mama kuhakikisha kuwa anavalia nguo za kupendeza na kuwa mshawishi mkuu katika maisha ya watoto wao. Kitu kingine tunacho soma ni kuwa marafiki na watoto wetu na kuongea na wao kwa uwazi kwani usicho wafunza, watasoma kutoka kwa dunia na halitakuwa somo rahisi. Kuna mengi tunayo yasoma kutoka kwa wamama hawa mashuhuri wa Kenya, angalia maisha yao kisha uamue utakacho fuata kutoka kwao. Kumbuka kuwa wao ni binadamu na huenda wakawa na makosa hapa na pale katika maisha yao, kama ilivyo kwetu sote.

wamama mashuhuri wa kenya

Siku ya wamama duniani kote ina sherehekewa siku tofauti katika pande tofauti duniani kote ila hakuna siku hasa ya kuwasherehekea wamama. Kwani hakuna siku wanapo chukua likizo kuto kuwa mama na kuyatimiza majukumu yao. Kwa hivyo, mama anapaswa kusherehekewa siku zote. Katika siku zinazo tambulika za mama dunia kote, ni vyema kuhakikisha kuwa unamsherehekea mamako kwa njia spesheli. Kuwa na wakati na yeye, kumnunulia zawadi ama kwa njia yoyote ile itakayo kupendeza. Pia iwapo mamako mzazi hakuwa nawe ulipokuwa, mkumbuke mwanamke aliye timiza jukumu la 'mama' maishani mwako.

 

Pulse NG

Soma pia: Profitable work from home jobs in Nigeria for moms

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio