Wanandoa Wanapaswa Kufanya Ngono Mara Ngapi Kwa Wiki?

Wanandoa Wanapaswa Kufanya Ngono Mara Ngapi Kwa Wiki?

Contrary to popular belief, a lot more happens in a marriage than having "legal" sex.

Ni swali la kusisimua ambalo lina majibu ambayo huenda yaka kushtua. Wanandoa hufanya ngono mara ngapi kwa wiki? Utafiti una dhibitisha wanandoa hufanya mapenzi mara ngapi kwa siku? Jibu ni fupi, ina lingana na unaye uliza.

Wanandoa hufanya nfono mara ngapi?

how often do married couples have sex statistics

Kuna utafiti mwingi huko nje unao onyesha ujumbe tofauti. Hapa kuna baadhi ya waliyo yapata:

Jarida la Newsweek lilifanya utafiti na kugundua kuwa wanandoa katika ngono hufanya mapenzi mara 68.5 kwa mwaka, ama zaidi kwa kiasi kidogo kwa wastani. Jarida pia lilipata kuwa wanandoa hufanya ngono mara 6.9 zaidi kwa mwaka ikilinganishwa na watu ambao hawajao oleka.

Kulingana na utafiti wa Chuo Kikuu cha Chicago unaojulikana kama “The Social Organization of Sexuality: Sexual Practices in the United States,” karibu asilimia 32 ya wanandoa walio oleka hufanya mapenzi mara mbili ama tatu kwa wiki, asilimia 80 ya wanandoa hufanya mapenzi mara chache kwa mwezi ama zaidi na asilimia 47 hufanya ngono mara chache kwa mwezi.

Katika somo lingine, mara hii na David Schnarch, Ph.D., aliye fanya utafiti kwa wanandoa 20,000, ni asilimia 26 pekee ya wanandoa wanaofanya mapenzi mara moja kwa wiki, ama mara moja ama mbili kwa mwezi.

Hakuna jambo la "kawaida”

Kwa hivyo, wanandoa hufanya ngono mara ngapi? Kama vile ulivyo ona kwenye ripoti hizi tofauti, ni rahisi kujua kuwa hakuna jambo la kawaida. Katika utafiti mwingi, watafiti na wataalum walisema kuwa ina tegemea na wanandoa.

Hamu ya ngono ya watu hukua tofauti, kila wanandoa hukua tofauti, na maisha yao ya kila siku hukua tofauti. Kwa sababu kuna vitu nyingi sana zinazo husika, ni vigumu sana kujua ni kipi "cha kawaida." Swali bora la kuuliza ni, je, ni kawaida kwako na mchumba wako? Ama kila mmoja wenu angependa kipi kiwe "kawaida" yenu?

Iwapo nyote mna furahia kufanya mapenzi mara moja kwa wiki, ama kwa mwezi, haijalishi kitu ambacho wanandoa wengine wanafanya. Lakini iwapo mmoja ama wawili wenu hamna furaha, huenda mkataka kuwa na mjadala kuhusu jambo hilo. Kwa wanandoa wengi, mtu mmoja mara zote huenda akataka kufanya ngono mara nyingi, na huo mwingine mara chache. Ni jinsi mnavyo tatua tatizo hili ili kusaidia wawili wenu litakalo leta tofauti.

Kiwango kipi cha ngono ili muwe na furaha?

wanandoa hufanya ngono mara ngapi

 

Utafiti mmoja wa kusisimua uliangalia furaha ikihusishwa na kiwango cha kufanya mapenzi. Wakati ambapo huenda ikaonekana kama ngono zaidi ni zuri, kuna kiwango ambacho furaha hupungua. Somo hili lilichapishwa na The Society for Personality and Social Psychology na kufanya utafiti kwa wanandoa 30,000 huko Umarekani kwa miaka 40.

Kwa hivyo ni kiwango kigani cha kufika unapo husisha ngono na furaha? Mara moja kwa wiki kulingana na watafiti. Kwa ujumla, ngono zaidi huongeza furaha, lakini hakuna haja ya kila siku. Kitu kingine chochote hakikuonyesha ongezeko la furaha.

Bila shaka, usikubalishe hiyo iwe jisababu ya kutofanya ngono zaidi; huenda wewe na mchumba wako mnapenda kufanya ngono zaidi ama kidogo. Kitu muhimu ni kuzungumza na kugundua kinacho wafurahisha. Ngono huenda ikawa ni jambo nzuri ya kupunguza fikira zako, na kukufanya uwe karibu zaidi na mchumba wako. Kwa hivyo iwapo, nyote mngependelea, hakuna sababu ya kutofanya kinacho wafurahisha.

Hamu ya chini ya ngono na sababu zingine

Na iwapo ngono hata haiko kwenye akili yako? Kwa bahati mbaya, watu wengi ama hata wote wawili katika ndoa huenda wakakosa hamu ya ngono ama kukawa na sababu nyingine inayo wazuia. Kulingana na jarida la Newsweek Magazine, asilimia 15-20 ya wanandoa huwa katika ndoa zisizo kuwa na ngono, ambayo ni sawa na kufanya ngono mara zaidi ya 10 katika mwaka. Utafiti mwingine ulidhibitisha kuwa karibu asilimia 2 ya wanandoa hawafanyi ndoa kamwe. Sababu za jambo hili hazidhibitishwi wakati wote-hii huenda ikawa ni kwa sababu ya vitu tofauti na kuwa na hamu ya chini ya ngono ni mojawapo.

Hamu ya chini ya ngono inaweza tendekea jinsia zote mbili, hata kama wanawake wana ripoti hali hii zaidi. Kulingana na USA Today, asilimia 20-30 ya wanaume huwa na hamu ya chini ya ngono ama kukosa yote, asilimia 30-50 ya wanawake husema hawana hamu ya kufanya mapenzi ama wana hamu ndogo. Watafiti wanasema kuwa, kadri unavyo zidi kufanya ngono ndivyo unavyo pata hamu zaidi ya kujihusisha na kitendo hiki.

Hamu ya ngoni ni kitu cha kusisimua. Inaonekana kuwa baadhi ya watu huzaliwa na hamu ya juu ama ya chini ya ngono, ila kuna sababu zinazo husika. Jinsi uhusiano wenu ulivyo ni sababu kuu, ila kudhulumiwa kingono hapo awali na sababu zinazo husika na ngono huenda ikawa sababu pia.

Kulingana na International Journal Of Impotence Research, sababu nyingi zaidi huadhiri mtazamo wa wanawake kwa ngono ya kindoa. Baadhi ya sababu hizi ni:

  • Matatizo ya kuwa na hamu ya ngono
  • Matatizo ya kufika kilele
  • Vita vya kinyumbani
  • Kuto zungumza kwa ndoa
  • Dini
  • Kukosa kumtayarisha mchumba wako kwa kitendo
  • Matatizo ya afya

Sababu tulizo angazia bila shaka zita athiri kiwango cha ngono ambacho wanandoa wako nacho.

Jinsi ya kuongeza nambari?

wanandoa hufanya ngono mara ngapi

 

Unashangaa kiwango cha ngono ambacho watu wengine huwa nacho. Huenda ikawa ni kwa sababu hauko mahali ambapo ungependa kuwa katika ngono kwa ndoa yako. Jambo hili hufanyika. Kuna changamoto mbali mbali. Nyakati za fikira nyingi, kama kuhama, ama kupata mtoto, ugonjwa huenda yaka ingilia kati.

Lakini ikiwa wewe na mchumba wako mmekuwa na matatizo kwa wakati, na huenda kukakosa kuwa na sababu kuu kwanini. Zaidi ya hicho nyi wote wawili, kuongea na mtaalum wa mambo yanayo husikana na wanandoa ni hiari njema. Mtaalum mzuri wa wanandoa anaweza kusaidia kugundua chanzo cha matatizo ya ngono, na awasaidie kuwaleta pamoja tena.

Zaidi ya kuona mtaalum, kuna vitabu vingi kuhusu ndoa na ngono na wewe na mchumba wako mnapaswa kusoma pamoja kupata mawazo zaidi. Iwapo nyote mnafurahia hiari hii na mngependa kujaribu hiari hii, mbona msipange likizo ndogo ya kuanza vitu upya?

Wanandoa hufanya mapenzi mara ngapi kwa wiki? Kulinganisha ubora na mara

Jambo lingine muhimu la kuangazia ni ubora na mara unazo fanya ngono. Iwapo nyote wawili mnapenda ngono mnayo ifanya, ni sawa pia. Kuna vitu ambavyo unaweza fanya kuwa nayo mara nyingi iwapo nyote mngependa hivi. Watafiti wengi husema uiratibishe. Inaonekana kama itakuwa kawaida, ila unapo anza utaipendelea. Kuiratibisha kuna maana kuwa itakuwa ya maana zaidi kwenu.

Iwapo ubora wa ngono uko chini, huenda ikawa sababu kwa nini mnaifanya mara chache. Katika ndoa, ngono ndiyo inayo waleta pamoja. Iwapo unashuhudia kupunguka kwa hamu yako ya ngono, jaribu kufanya utafiti kujua kwa nini jambo hili limetendeka na unaweza mwuliza mchumba wako pia. Chochote unacho pata, hakikisha kuwa unatumia muda kutafuta suluhu. Wacha kumlaumu mwingine na uchukue jukumu kutafuta suluhu. Pia, tia akilini kuwa mtaalum wa mambo ya wanandoa anaweza wasaidia kuimarisha mambo yoyote mnayo kuwa nayo.

Kuna utafiti mwingi uliofanywa kuhusu wanandoa hufanya ngono mara ngapi, na ndiyo unaotueleza mara ambazo ni kawaida kwa wanandoa kufanya ngono. Lakini ukweli ni kuwa, hakuna kawaida. Kila wanandoa huwa tofauti, kwa hivyo ni jukumu yenye kujua kinacho wafurahisha.

Kumbukumbu: Marriage

Soma pia: Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Written by

Risper Nyakio