Kufuatia sababu zisizo eleweka, wanandoa hubishana zaidi wakati wa likizo. Likizo ni wakati wa kupumzika na wapendwa wetu na hakuna anayependa kutumia wakati huo akikorofishana na mchumba wake. Tazama baadhi ya sababu zinazopelekea wanandoa kukorofishana wakati wa likizo na jinsi ya kuziepuka.
Wanandoa kukorofishana wakati wa likizo
- Zawadi uliyonunua haikuwa bora kwao
Sio kila mtu ana uwezo wa kufahamu zawadi bora, baadhi ya watu huwa na uwezo dhaifu wa kuwapa wengine zawadi. Ni mojawapo ya sababu maarufu kwanini wanandoa hukorofishana. Na ni rahisi kuelewa kwa nini. Kumpa mwenzi wako kadi ya krisimasi haihisi vyema. Hasa kama wewe ni watu wanaochukua muda na kuwatunza watu zawadi nzuri.
Ili kuepuka kukorofishana na mchumba wako, hakikisha kuwa unapanga muda kabla na uchukue muda kufikiria kuhusu wanacho hitaji. Sio lazima ziwe vitu vya bei ghali, mbali zenye maana na spesheli.
2. Kutumia pesa zaidi wakati wa likizo

Sawa na mambo mengi yanayo husiana na pesa, wanandoa hukorofishana sana mmoja wao anapotumia pesa zaidi wakati wa likizo. Haijalishi iwapo alitumia kununua zawadi ama kufanya mambo mengine, ni sababu maaufu inayowafanya wanandoa kukorofishana wakati wa likizo.
Njia moja ya kuepuka haya ni kukaa chini na mchumba wako na kupanga bajeti ya matumizi yenu yote ya kipindi cha likizo na kuhakikisha kuwa mnazingatia bajeti hiyo. Epuka kutumia pesa zaidi ya uwezo wako hata unapotarajia pesa za zaidi kipindi hicho. Inapofika wakati wa zawadi za marafiki na familia, sio lazima ziwe zawadi za bei ghali, lakini kumbuka zinapaswa kuwa spesheli.
3. Sherehe nyingi za likizo
Sherehe wakati wa likizo ni njia ya kusisimua na kupatana na watu ambao hamjaonana kwa muda mrefu. Hata hivyo, kwenda sherehe nyingi kunaweza kufanya uwe na uchovu mwingi. Ukihisi kuwa unachoka sana, unaweza mweleza mchumba wako kuwa ungependa kupumzika. Ni bora kukosa kuhudhuria sherehe zingine na kupumzika badala ya kuhisi uchovu na kushindwa kufanya kazi zako za kawaida.
4. Mawazo mengi wakati wa kusafiri

Kuna baadhi ya wanandoa wanaofanya uamuzi wa kwenda nchi zingine wakati wa likizo, na wakati ambapo kuzuru nchi tofauti ni jambo la kusisimua, huenda ikawa chanzo cha wanandoa kupigana.
5. Maoni tofauti ya vitu vya kufanya wakati wa likizo
Kila familia huwa na mila zake za likizo. Baadhi ya familia huwa na sherehe rahisi nyumbani mwao, wakati ambapo familia zingine hupenda kufanya vitu vikubwa. Ili kuepuka kukorofishana kuhusu jinsi ya kutumia wakati wao wa likizo, jambo la maarifa la kufanya ni kuelewana. Ni vyema kwa wanandoa kukaa chini na kujadili mambo ambayo wangependa kufanya katika kipindi hiki.
Chanzo: Huffingtonpost.com
Soma Pia: Vidokezo 3 Muhimu Vya Jinsi Ya Kutumia Mitandao Kwa Wanandoa