Kuna sababu nyingi ambazo huenda zinafanya uhusi uhusiano wenu unabadilika sio kama hapo awali. Na hiyo ni ishara kuwa kuna vitu vinavyopaswa kufanyika. Makala haya yanasaidia wanandoa kufahamu vitu ambavyo hawafanyi, wanandoa wanapaswa kufanya mambo haya!
Wanandoa wanapaswa kufanya haya

- Mwaminishe mchumba wako unampenda na kumjali
Ikiwa haumwelezi mchumba wako unavyo mjali na kumpenda mara nyingi uwezavyo, ni vyema kuanza mapema uwezavyo. Mwanasaikolojia wa mapenzi alidhibitisha kuwa ishara za mapenzi za mara kwa mara zina matokeo chanya katika mahusiano. Huenda ikawa rahisi kama kumnunulia zawadi, kumpeleka kula hotelini ama kumkumbatia asipotarajia na kumwambia unampenda. Ishara za kimapenzi huchangia pakubwa katika uhusiano.
2. Kuwa wazi usione haya kuonyesha udhaifu wako
Kulingana na mwandishi wa kitabu cha mapenzi Randi Gunther, ni rahisi kunyamaza na kujiwekea matatizo yetu tunapokuwa na jambo linalo tusumbua ama tunapo kasirishwa na mtu mwingine. Walakini, kufanya juhudi za kuwa wazi na kuweka kiburi chini inapofika kwa mawasiliano kuna afya zaidi. Kutapunguza michezo ya kiakili na kutosikizana kusiko faa. Haijalishi kinachofanyika, wanandoa wanapaswa kuzungumza kinachoendelea akilini mwao bila kumfanya mwingine ahisi haya.
3. Weka maisha yake ya kimapenzi siri
Ili kuwa na uhusiano wenye utangamano mzuri, ni muhimu kwa wachumba kuheshimu maisha ya kimapenzi ya wachumba wao na kuyaweka siri. Hasa inapofika kwa marafiki wenu. Huenda ikaonekana kama jambo nzuri kumweleza rafiki yako kinacho endelea katika uhusiano wenu, ni muhimu kukumbuka kuheshimu mipaka ya mchumba wako. Kufanya hivi kutaboresha uhusiano wenu. Ikiwa una tatizo na mchumba wako, ni vyema kumweleza badala ya kumwongelelea. Kunasaidia kutatua matatizo yenu na kuyaepuka katika siku za usoni.
4. Kutazama sinema pamoja

Kulingana na utafiti uliofanyika, wanandoa wanaotazama sinema pamoja angalau mara moja kwa wiki walikuwa na nafasi za chini za kutengana. Hata hivyo, usimlazimishe mchumba wako kutazama sinema asizo zipendelea. Sinema mnazotizama zinapaswa kuwa za kimapenzi mapenzi. Watafiti waligundua kuwa kutizama na kuzungumzia sinema kuhusu mahusiano ni njia bora ya kupunguza nafasi za kutengana. Iwapo ungependa kuboresha uhusiano wenu kwa njia inayo sisimua na bora, unapaswa kutizama sinema na mchumba wako.
5. Jihusishe katika vitendo vya kujikuza pamoja
Wanandoa wazuri waliokatika uhusiano mwema na wenye afya mara nyingi hujaribu kujihusisha katika vitendo vya kujikuza. Huenda vikawa kutembea pamoja, kufanya mambo mapya ya kusisimua kwa pamoja. Ikiwa ungependa kujenga msingi wa uhusiano wenu ama ndoa yenu, mnapaswa kujaribu njia nyingi na mbalimbali za kuboresha uhusiano wenu kupitia kwa vitendo vya kujikuza.
Soma Pia: Tabia Tatu Zinazo Leta Hujuma Katika Uhusiano