Kabla ya kuanza, ni vyema kusisitiza kuwa: hii sio njia ya kifupi ya kutatua masuala yenu yote kwa kutumia njia hii ili kusuluhisha matatizo ya kindoa yanayo wakumba. Hata hivyo, ni mbinu ya kweli iliyo jaribiwa ambayo kila wanandoa walio katika ndoa zenye furaha hutumia. Katika machapisho ya hivi karibuni na Macy Williams, aliangazia mambo yote ambayo wanandoa wenye furaha hufanya kila siku.
Ili kubaini vyanzo vya ndoa zenye ufanisi, Williams aliwauliza wanandoa wachache maswali kwanini ndoa zao zilifuzu. Kama anavyo ripoti, walikuwa na maswali mbalimbali kwa jibu hilo. Cha kushangaza ni kuwa wote walikuwa na jambo moja sawa: walizungumza na wachumba wao.
Siri ya kuwa katika ndoa yenye furaha sio kuzungumza tu, ni kwa wanandoa kuwasiliana. Ili kudumisha mawasiliano na mazungumzo yenye afya, wanandoa wanapaswa kufanya vitu hivi vitatu. Soma zaidi ili upate kufahamu jinsi ambavyo wanandoa wanavyo dumisha furaha katika ndoa zao.
Pande Tatu Muhimu Za Mazungumzo

Eleza hisia na mahitaji yako
Hakuna jinsi ambavyo mchumba wako anaweza kufahamu mahitaji yako katika uhusiano usipo mweleza. Hakikisha kuwa unaeleza kinaga ubaga hisia zako - iwapo una furaha ama huzuni. Hakikisha kuwa wakati wote mchumba wako anaelewa kinacho kukumba. Hana uwezo wa kusoma akili yako na kujua matarajio yako. Unaweza kusoma kitu kipya kumhusu pia.
Hata kama unamfahamu mchumba wako kumliko mtu mwingine yule, haimaanishi kuwa wana uwezo wa kujua kila kinacho endelea moyoni na akilini mwako. Ikiwa una kitu akilini, jaribu kuwaeleza kwa njia iliyokomaa bila kutumia maneno ya kukera moyo. Usiwe na uwoga wa kumwonyesha udhaifu wako.
Kuwa mwaminifu
Dakika unapo anza kudanganya ndipo mambo yanapo enda mrama. Iwapo huwezi kuwa mwaminifu na mtu unayempenda, utakuwa mwaminifu na nani mwingine? Mbali na kuwa wazi kuhusu uhusiano wenu, mweleze unapokuwa na siku mbaya kazini ama baada ya rafiki kuumiza hisia zako. Jinsi mnavyo zungumza kuhusu mambo tofauti zaidi, ndivyo mnavyo kuwa na utangamano wa karibu zaidi.
Ulipofunga pingu za maisha na mchumba wako, mlikubaliana kuwa mngesema ukweli wakati wote. Mchumba wako sio mama ama baba ya watoto wako tu, mbali ni mpenzi wako wa maisha. Ni muhimu kuwa mkweli nao wakati wote.

Usi zungumze tu, hakikisha una sikiliza pia
Mbali na kuzungumza na mchumba wako na kumweleza yote unayo hisi na unayofikiria, ni muhimu kusikiliza pia. Huenda mchumba wako akawa anakueleza kuhusu vitu unavyopaswa kubadilisha, ni vyema kuwa na mawazo wazi. Pia, hakikisha kuwa unamsikiliza mchumba wako.
Soma Pia: Ndoa Za Kudumu Muda Mrefu: Ishara Kuwa Ndoa Yako Haiwezi Vunjika