Ikiwa umesikia kuhusu wanaume wanaofilisika kimawazo na kupata kiwewe cha mawazo mengi kufuatia kushuhudia kuzaliwa kwa watoto wao, wazo lako la kwanza huenda labda lilikuwa kushtuka na kushangaa. Kivipi? - Ni mzaha? Ni wanaume wagani hawa wanaodai kuhofia maisha wakati ambapo ni wake zao waliopitia maumivu ya mgongo kwa miezi mingi, ugonjwa wa asubuhi na mhemko wa hisia na uchungu wa kujifungua? Ni kweli kuwa wanaume hupata kiwewe wake zao wanapojifungua.
Lakini kulingana na utafiti uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Oxford, ulivumbua kuwa wanaume hupata kiwewe wakati wa kuzaliwa kwa watoto, hasa wake zao wanapopitia upasuaji mgumu. Baba pia walikubali kuwa walishindwa kusema walichohisi kwa sababu walihisi kuwa zingatio lao kuu lilikuwa kuwatunza mama na mtoto.
Wanaume hupata kiwewe wake zao wanapojifungua?

Tunaposikia kuhusu kujifungua, wakati wote, tunafikiria kuhusu mama na mtoto, na kumtupilia baba katika mchakato huu, hata kama wakati mwingi, sio kwa kusudi. Na sio imani za kijamii tu, kuna baadhi ya madaktari wanaowatenga kwa kutowajulisha hali ya mama na mtoto.
Kwa usawa, mwanamme anaye andamana na bibi yake kwenye chumba cha kujifungua, huenda akashtuka kumwona mchumba wake akiwa katika uchungu mwingi na kiwango cha damu anachovunja. Huku akiwa amesimama kwa umbali, bila hakika anachostahili kufanya na atakavyomtuliza bibi yake aliye katika uchungu, sio jambo geni kuwa wanaume huhisi uwoga kufuatia shinikizo jingi linalo wakumba.
Kwanini shaka hizi huibuka
Wazo ambalo mwazo liliibua hasira hueleweka zaidi tunapogundua jinsi tunavyowapuuza wanaume katika masuala ya kujifungua yanayohusishwa na wanawake. Ni jambo la kawaida kumpata baba akiwa amesimama nje ya chumba cha kujifungua bila kufahamu iwapo bibi yake na mtoto wako uhai.
Kuona placenta ya mama kwenye meza huenda kukamtia baba katika wasiwasi na kudhani kuwa jambo mbaya limetendeka baada ya kuona damu jingi na kukosa kumwona mama ama mtoto. Kwa sababu hakuna anayeshughulika kumweleza kinachoendelea na hali ya mtoto na bibi yake. Kungoja kwa muda mrefu kutamfanya awe na kiwewe kila mara anaposikia kuhusu kujifungua.
Watunze wanaume vyema, tafadhali

Wanaume huwa na jukumu kubwa na hai katika ulezi na kuegemeza wake zao katika mchakato wa kujifungua. Je, kuna jambo ambalo linaweza kufanyika ili kuwasaidia wanaume hawa? Wakati ambapo kujifungua huwaweka katika athari ya kupata kiwewe, tunaamini kuwa linaweza kutatuliwa kwa usaidizi wa utunzaji wa kibinafsi wa kimatibabu.
Ni vyema kuwa na huruma kwa wanaume wanaotia juhudi kuwasaidia wake zao wanapoenda kujifungua. Kuwajulisha kinachoendelea chumbani cha kujifungua, kunawasaidia kupunguza mawazo mengi.
Soma Pia: Manunuzi Muhimu Ya Mtoto Kabla Ya Kwenda Katika Chumba Cha Kujifungua