Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Utafiti: Wanaume Huumia Zaidi Baada Ya Kutengana Na Wachumba Wao

3 min read
Utafiti: Wanaume Huumia Zaidi Baada Ya Kutengana Na Wachumba WaoUtafiti: Wanaume Huumia Zaidi Baada Ya Kutengana Na Wachumba Wao

Kulingana na utafiti uliofanyika mwaka wa 2017, imedhihirika kuwa wanaume huumia zaidi baada ya kutengana katika ndoa ama uhusiano. Sababu ni zipi?

Mojawapo ya sababu kuu kwa nini wanaume huumia zaidi baada ya kutengana na wachumba wao katika uhusiano ikilinganishwa na wanawake ni kwa sababu mara nyingi wanaume hupenda kunyamazia mambo.

Tamati ya uhusiano haiwi sawa kwa mtu yeyote. Wanaume huumia, wanawake vivyo hivyo baada ya hisia za furaha kuisha kufuatia kuachwa. Hata pale ambapo kukosana kulikuwa kuna tarajiwa, mchakato wa kuhuzunika bado huuma.

Kwa Nini Wanaume Huumia Zaidi Baada Ya Kutengana Na Wachumba

wanaume huumia zaidi baada ya kutengana katika uhusiano

Somo lililo chapishwa lilionyesha kuwa wanaume huumia uchungu zaidi na kwa muda mrefu baada ya kuachana katika uhusiano ikilinganishwa na wanaume. Swali asili linalo fuata hapa ni: kwa nini? Kivipi na mbona wanaume wana umia zaidi ilhali wanaonekana kupata wachumba wengine kirahisi na bila kudhihirisha uchungu wowote.

Kulingana na makala yaliyo chapishwa mwaka wa 2017, sio suala tofauti kusema kuwa wanaume hutatizika zaidi baada ya kutengana na wachumba wao kuliko wanawake kwa sababu, kihisia, wanaume mara nyingi hawana mwitiko chanya kwa masuala makubwa ya maisha. Cha zaidi, mbinu za kukabiliana na hali zilizo badilika wakati wote hazisaidii.

Katika mwaka wa 2015, utafiti ulio fanywa na Makala ya Afya ya Wanaume, iliegemeza matamshi hayo. Watafiti wa somo hili waligundua kuwa kuenda kwenye vilabu kulitajwa kama mojawapo ya njia bora zaidi za kukabiliana na kutengana na mchumba, kulingana na utafiti huo. Wakati ambapo theluthi ya majibu walisema kuwa, sherehe hiyo ingekuwa bora mwanamme asipo onyesha hisia zozote kuhusu tukio hilo.

Hiyo ni mojawapo ya sababu kuu kwa nini wanaume huumia - kutokuwa tayari kukabiliana na kilicho tendeka na kukubali jambo hilo.

"Wanaume walikuwa katika jamii inayo wakumbusha baada ya kila tendo ndogo kuwa 'wanaume hawapaswi kulia' na wakati ambapo wanaume wanafanya mambo tofauti ama kukabiliana na hisia zao kwa njia tofauti, haimaanishi kuwa hawahisi uchungu ama kuumia kwa kiwango sawa na wanawake," alisema daktari mmoja kutoka Dublin. "Kwa hivyo kwa vizazi vingi, wanaume wamefunzwa jinsi ya kupuuza hisia zao, uchungu na kuumia ili kuwa 'mwanamme' na hawana nafasi ya kuonyeshana unyonge wao."

Kwa Nini Wanawake Hupona Mbio Baada Ya Kutengana Katika Uhusiano

chumvi kupima mimba

Kwa upande mwingine, wanawake wana hisi wako huru zaidi kutafuta mtu wa kumwelezea hisia zao na kinacho wasumbua. "Mara nyingi, wanawake hawategemei wenzi wao kihisia- wana marafiki wengi na wanaweza waelezea jamii na familia yao kwa njia ambao wanaume watapata ikiwa vigumu kwao kufanya.

Sababu nyingine kwa nini wanawake hawaumii sana baada ya kutengana na wachumba wao ni kwa sababu mara nyingi, wao ndiyo huwaacha wachumba wao. Kwa kufanya hivi, wanawake wana wakati mwingi zaidi wa kuanza kujitayarisha kimawazo, kiakili na kihisia kuhusu uchungu wa tendo hilo. Na kuanza kujipanga watakayo fanya wanapo tengana. Wanapo fanya uamuzi wa kutengana, nafasi nyingi ni kuwa watakuwa wamemalizana na kipindi hicho, wakati ambapo, mara nyingi, mwanamme atakuwa anaanza tu.

Hitimisho

Ni vyema kwa wanaume kujifunza jinsi ya kuzungumza kuhusu hisia zao badala ya kunyamaza. Na kwa njia yenye afya zaidi, ikilinganishwa na kunywa pombe kuwasaidia kusahau wanacho kipitia.

Soma Pia: Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Utafiti: Wanaume Huumia Zaidi Baada Ya Kutengana Na Wachumba Wao
Share:
  • Mambo Ya Kufanya Baada Ya Kuwachwa Na Mchumba Wako!

    Mambo Ya Kufanya Baada Ya Kuwachwa Na Mchumba Wako!

  • Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

    Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

  • Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

    Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

  • Kwa Nini Wanawake Wanavutiwa Na Wanaume Walio Katika Ndoa Kulingana Na Sayansi

    Kwa Nini Wanawake Wanavutiwa Na Wanaume Walio Katika Ndoa Kulingana Na Sayansi

  • Mambo Ya Kufanya Baada Ya Kuwachwa Na Mchumba Wako!

    Mambo Ya Kufanya Baada Ya Kuwachwa Na Mchumba Wako!

  • Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

    Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

  • Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

    Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

  • Kwa Nini Wanawake Wanavutiwa Na Wanaume Walio Katika Ndoa Kulingana Na Sayansi

    Kwa Nini Wanawake Wanavutiwa Na Wanaume Walio Katika Ndoa Kulingana Na Sayansi

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it