Je, Kufanya Ngono Asubuhi Kuna Ongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba?

Je, Kufanya Ngono Asubuhi Kuna Ongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba?

Kumpa bibi yako mimba huenda kukawa kazi nyingi kwa wanaume. Je, unapate ujumbe unao faa? Mwanamme ana nguvu nyingi za kiume lini? Soma mambo ya kusisimua kuhusu ukweli wa manii ya kiume.

Baadhi ya wanandoa hupata mimba bila juhudi nyingi, ila kwa wengine, kupata mimba kunaweza kuwa kazi ngumu. Wanaume watapata ushauri mwingi kuhusu kila kitu- hata wakati na jinsi ya kufanya ngono. Mojawapo ya ushauri kawaida zaidi? Fanya ngono asubuhi. Ila, je, hii ni kweli? Wanaume wana nguvu za uzazi nyingi lini? Tuna jifunza zaidi kuhusu jambo hili!

nguvu za uzazi nyingi- manii

Manii yana uwezo wa kutunga yai zaidi lini?

Sayansi Kuhusu Kutunga

Kabla tuongee kuhusu manii ya wanaume, tujifunze zaidi kuhusu kutunga.

Tuko katika kikundi cha mamalia ambao jinsia ya kike huwa na mzunguko wa mwezi wa uzazi unaojulikana kama mzunguko wa hedhi. Mwili wa mwanamke hutayarisha kwa ujauzito unao wezekana katika muda fulani kila mwezi.

Katika kipindi chake chenye ‘rutuba’ – mara nyingi karibu siku 12-14 kila mwezi – mwanamke hutoa ovum, ama yai linalo kufa katika masaa 24. Walakini manii yanaweza ishi hadi muda wa siku tano.

Kwa hivyo, ikiwa unapanga kupata mimba, ‘kipindi chenye rutuba’ unapaswa kulenga siku mbili ama tatu kabla ya siku yako ya kupevuka kwa yai hadi siku moja baada. Ikiwa vipindi vya hedhi vya bibi yako ni vya kawaida, unaweza tumia apps zilizoko kujua wakati bora kwake.

Ukweli kuhusu manii

Katika masomo, ilipatikana kuwa utoaji wa manii mwilini huja kwa sehemu mbili. Ya kwanza, huwa na madini muhimu kama zinc na huwa na manii zaidi yenye nguvu na tayari kufanya yai litunge.

Ya pili huwa na kemikali ambazo zinaweza ua manii mengine, kwa mfano kutoka kwa mwanamme mwingine! Na kulinda kupita kwa DNA.

Chochote ukifanyacho, hakikisha kuwa sehemu ya kwanza ya manii inaingia ndani kwenye uke.

Kwa hivyo, wanaume huwa na uzazi mkubwa lini?

 

when are men most fertile

Kuna ushuhuda mwingi wa anecdotal kuwa wanaume wana ‘rutuba’ zaidi wakati wa asubuhi. Pia, masomo yana dhibitisha kuwa idadi ya manii ya mwanamme huwa nyingi wakati wa asubuhi.

Hilo na ukweli kuwa wanaume huamka wakiwa na mhemko wa kufurahisha asubuhi– naam, kuna nafasi za juu za kupata mimba na ngono ya asubuhi.

Walakini, jina kuu ni ‘nafasi za kuu kiasi’. Kwa hivyo ikiwa mnapendelea ngono ya alfajiri ama usiku bila shaka, ni vyema kufanya kinacho wapendeza.

Kwa hivyo jibu la swali hili ni nini “wanaume wana uzazi zaidi lini?”.

Wana uzazi zaidi wanapokuwa na afya na furaha!

Badala ya kumrukia bibi yako wakati wowote ule unapokuwa na mhemko wa asubuhi, kuna njia bora za kuongeza nafasi zenu za kutunga.

Kuna mambo matatu unapaswa kuhakikisha unapo jaribu kutunga.

  1. Fanya ngono mara kwa mara. Dhidi na watu wengi wanavyo amini, masomo yameonyesha kuwa kukaa bila kufanya ngono kwa masaa 18 hakupunguzi nguvu za manii. Ili kutumia kipindi cha rutuba cha mwanamke, una mwany mdogo wa siku chache. Kwa hivyo utumie zaidi, na ufanye ngono zaidi. Usipitishe kiwango kwani huenda kukawa hakuna faida. Kupata manii mara kwa mara ni bora kuliko mara unazo zipata.
  2. Kula vyema, uwe na afya. Kuvuta sigara, kunywa pombe na vyakula vyenye viwango vya juu vya sukari na chumvi kuna athari hasi kwa manii yako. Kwa hivyo, kula vyakula vyenye afya kwa angalau miezi miwili kabla ya kujaribu kupata mimba (mzunguko mzima wa manii huchukua siku 64), usi gonjeke, na ufanye mazoezi. Mazoezi mara kwa mara yata punguza mawazo mengi ya kutunga mimba.
  3. Usivalie nguo za ndani zinazo kubana. Joto ita athiri manii kwa njia hasi, hasa kwenye nchi zinazo shuhudia joto jingi. Kwa hivyo, ikiwa unafikiria kuhusu kupata watoto, chagua nguo za ndani zisizo kubana. Huenda ukahisi hauna starehe kwa siku za kwanza chache kabla uzoee. Pia unalala vizuri sana kwa nguo zisizo kubana.

Hii ni hatua kubwa ya kuanza familia. Nina uhakika umefikiria kuhusu mambo mengine kama fedha, ukichukua hatua hii kubwa. Kwa hivyo usingoje hadi asubuhi kuongeza nafasi zako za kutunga, na usiwe na shaka nyingi kama “wanaume wana nguvu za uzazi nyingi lini?”

Vyanzo:

  1. Andrology, open access
  2. Science Direct
  3. Science Daily

Soma piaKula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Written by

Risper Nyakio