Wanawake katika miaka yao ya late 20's bila wachumba huambiwa mambo mengi. Hasa na wanawake wengine walio katika mahusiano ama ndoa. Kila mtu anaona doa katika wanawake hawa. Hata wanapokuwa wakiishi maisha mazuri bila kukosa chochote. Wanawake walio katika late 20's bila wachumba wangependa mfahamu haya.
Fahamu haya kuhusu wanawake katika late 20's bila wachumba

- Sio rahisi kuwa bila mchumba katika late 20's
Kuna changamoto za kuwa bila mchumba katika miaka ya late 20's. Zote za kijamii na kibinafsi.
Kufanya baadhi ya vitu ukiwa peke yako sio raha ama huenda kukawa changamotoo. Ukiwa na mwenzio, mnafanya kazi zingine kwa kasi, pia hauna upweke. Unapohitaji kubadilisha balbu ya nyumba, itabidi utafute mtu atakayekusaidia. Ingekuwa rahisi kama ungekuwa na mchumba wa kukusaidia na baadhi ya kazi kama hizo.
Jamii na familia wanashangaa kwa nini ungali huna mchumba. Huku wengine wakitaka upate mtoto. Kwa sababu hauna mchumba, hawataelewa kwa nini hauendi kuwatembelea kila wikendi na likizo.
2. Kuwa bila mchumba hakumaanishi nataka mtu yeyote
Wanawake walio katika umri wa makamo bila wachumba wana viwango vya juu vya wachumba. Kuwa bila mchumba kwao haimaanishi kuwa wamekata tamaa na wangetaka kuwa na mtu yeyote ili isemekane kuwa wana mchumba, la.
Huenda marafiki wakafikiria kuwa wanawake hawa wamekosa watu wanaowatamani. Ukweli ni kuwa, wanawake hawa wana wanaume wengi wanao wachumbia, ila, hawafiki kiwango walichoweka cha kuchumbiwa.

4. Niko sawa sina tatizo
Mara nyingi wanawake walio katika ndoa huwaangalia wanawake walio katika makamo bila wachumba kana kwamba wana tatizo. La, wanachotaka kutoka kwao ni kwako kuwakubali na kutooana kana kwamba kuna tatizo nao. Huenda pia wakadhani kuwa hawana furaha, na kuwa lazima uwe na mchumba ili uwe na furaha.
Kumbuka kuwa kuna wanawake wanaoamua kubaki peke yao ili kutimiza malengo yao ya kimaisha ama kwa sababu wanapendelea hivyo.
5. Kuwa katika ndoa sio kibali cha kuwa mjeuri
Watu katika ndoa huwa na maoni mengi kuhusu wanawake ambao hawana wachumba. Kuwa bila mchumba hakumaanishi kuwa mwanamke ana wachukia wanaume. Ama hana furaha, ama amekata tamaa na maisha. Kuwa bila mchumba hakumfanyi mtu asiye kamili la hasha. Kwa hivyo jitenge na kuhakimu maisha ya wanawake wasio na wachumba.
Soma Pia: Mchumba Wako Ni Mwanatimu Wako, Na Wala Sio Adui Yako