Mwanamke katika kikundi cha marafiki wanawake anapoingia katika ndoa. Uhusiano wake na marafiki wake hasa walio bila wachumba hubadilika. Wanawake katika ndoa wangependa marafiki wao bila wachumba wafahamu haya. Ili waendelee kuwa na uhusino.
Wanawake katika ndoa wangependa ufahamu:

1. Kuwa na bwana hakumaanishi kuwa mimi sio rafiki yako tena. Na unapotaka mtu wa kuelezea kuhusu mwanamme mliyepatana naye sina wakati. La. Tungali marafiki tena wa dhati. Nipigie simu wakati wote kunieleza jinsi date yako ilivyokuwa.
2.Ninapoteta kuhusu bwanangu kwako, haimaanishi kuwa nitamwacha. Mbali nataka kuzungumza na mtu mbali na yeye. Nisingetaka pia umtusi ama umwulize maswali ama kunikumbusha kuwa naweza pata mwanamme mzuri kumliko.
3. Ninapokwambia kuwa nitazungumza na bwanangu kisha nikwambie, si maanishi kuwa namwomba ruhusa. Ila sisi ni wanatimu na nisingependa kufanya kitu chochote bila kumjuza. Kwa njia sawa, nisingependa afanye vitu kabla ya kunijulisha.
4. Ni jeuri kutuuliza tutapata watotot lini. Kuwa katika ndoa hakumaanishi kuwa wanandoa wangependa kupata watoto. Kuna wachumba wanaoamua kuishi bila watoto na kufuata kazi na masomo yao. Pia, huwezi jua ama wachumba wanapitia matatizo kushika mimba.

5. Ni sawa kuamua kukaa peke yako bila mchumba. Licha ya jumuiya kumwambia msichana kuwa kuna umri fulani anapaswa kuwa ameolewa na kupata mtoto. Ni sawa kufanya uamuzi wa kubaki peke yako na kutimiza malengo yako ya kimaisha. Usiwasikize watu wengine, fuata unachotaka.
6. Wakati mwingine nauonea uhuru wako wivu. Nina kazi nyingi za nyumbani, kusafisha vyombo, nyumba na kuitunza familia yangu. Watoto hawanipatii nafasi ya kuwa peke yangu.
7. Kuolewa hakukunibadilisha. Ningali rafiki yako na sijabadilika. Ila, nina majukumu zaidi na huenda nikakosa muda wa kuwa pamoja nawe kama ilivyokuwa hapo mbeleni.
8. Unapoona kuwa rafiki yako katika ndoa mbaya na kamwe hakusikizi. Usikate tamaa kumsaidia. Zungumza na rafiki yako bado. Siku atakapoamua kutengana na bwanake, watahitaji mtu wa kumwegemeza.
9. Nakupenda lakini naipenda familia yangu zaidi. Usione wivu ninapokuwa na familia yangu muda zaidi. Unaponiita twende mahali kisha kukwambia kuwa niko na familia yangu, usiskie vibaya.
Soma Pia: Vidokezo Vilivyothibitishwa Ambazo Washauri Wa Mahusiano Hutumia Kurejesha Ndoa