Sababu Kwa Nini Wanawake Wanapaswa Kufahamu Jinsi Ya Kuanzisha Ngono

Sababu Kwa Nini Wanawake Wanapaswa Kufahamu Jinsi Ya Kuanzisha Ngono

Sababu kwa nini wanawake katika ndoa na uhusiano wana himizwa kuanzisha ngono ni sio kungoja wanaume waanzishe wakati wote.

Kulingana na utafiti, imedhihirika kuwa mwanamme wa wastani hufikiria kuhusu ngono angalau mara moja kwa siku. Pia, wanaume ikilinganishwa na wanawake, wamedhihirika kuanzisha ngono mara mbili zaidi kuliko wanawake.

Sababu Kwa Nini Wanawake Hawako Huru Kuanzisha ngono Kama Waume

wanawake kuanzisha ngono

Wanawake wengi hawahisi vyema ama hawana ujasiri tosha kuanzisha ngono. Jambo hili huenda lika husishwa na jamii tunayo ishi ambapo wanawake wanao kuwa na hamu ya juu wanaonekana kama wabaya. Lakini mwanamme aliye na hamu ya juu ya ngono ana pongezwa na kusifiwa. Sababu hizi zime fanya iwe rahisi na ionekane asili kwa wanaume kuanzisha ngono. Kwa wake walio katika uhusiano na ndoa, hamna nafasi ya kufikiria kwa njia hii.

Kumwacha mume wako aanzishe ngono wakati wote na kukataa kushika usukani hakutoshi. Unapaswa kusoma jinsi ya kuongoza na sio jambo la kufanya mara moja baada ya muda mrefu, mbali ni kitu unacho stahili kuwa unafanya mara kwa mara.

Unapaswa kuwa na starehe tosha kufanya hivi mara nyingi iwezekanavyo. Sababu moja ni kuwa, wakati ambapo wanaume hawana uwoga wa kufanya hivi, inafika wakati ambapo hawawezi tambua ikiwa unataka kufanya tendo hili ama unalifanya kwa sababu wanalitaka. Na huenda wakawa na hofu kuwa moto ulio kuwa kwenye uhusiano wenu ama ndoa una pungua.

Kwa Nini Wanaume Wanapendelea Wanawake Kuanzisha Ngono

wanawake kuanzisha ngono

Ngono ni bora wakati ambapo wachumba wote wana ujasiri kuwa hilo ndilo mchumba mwingine anataka katika wakati huo pia. Pia, wanaume wanataka kuhisi kuwa wana pendwa na kutamaniwa sawa na wanawake. Ni jambo linalo wasisimua wanapo hisi kuwa wana tamaniwa. Kwa hivyo unapo wacha ujumbe mdogo wa kimapenzi kwenye bafu kuhusu kinacho mngoja chumbani usiku huo na kufanya hatua ya kwanza ya kimapenzi, una boresha maisha yenu ya kingono na uhusiano wenu.

Tena, kuanza mazungumzo ya ngono na mchumba wako ni vizuri kwani kuna inua hisia zake za kuwa mwanamme kamili na kujiamini kwake, pia kuna ongeza furaha kwenye uhusiano ama ndoa hiyo.

Wakati ambapo kila mwanamke ana stahili kujua haya, ni muhimu zaidi kwa wanawake walio katika uhusiano na ndoa kwani inaweza kua tofauti kati ya kuwa na maisha ya kingono yenye afya na kuwa na yaliyo vugu vugu na yasiyo na furaha.

Soma Pia: Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue

Written by

Risper Nyakio