Kufika kilele katika ngono sio jambo la kipekee katika kufanya mapenzi. Hata hivyo ni muhimu kuangazia wanawake kufika kilele katika ngono na sababu zinazo wazuia kuwa na kipindi cha kusisimua cha mapenzi.
Wanawake walipatiwa vikundi hivi wachague:

- Tendo la ndoa na mchumba asiye wapendeza
- Kufanya mapenzi nami hakumpendezi mchumba wangu
- Sifurahii kufanya mapenzi na mchumba wangu
- Mchumba wangu haonekani kufurahia kufanya mapenzi nami
- Sifiki kilele katika ngono
- Sija tayarishwa vya kutosha wakati wa ngono
- Nahisi uchungu wakati wa kitendo cha ngono
- Hatuna wakati wa kutosha katika ngono, tuna kimbilia
- Nafikiria kuhusu mwili wangu na ninavyo kaa katika ngono
- Kutumia dawa ama hali fulani ya mwili inani zuia kufika kilele katika ngono
- Naskia kuwa ni vigumu kufika kilele kwa sababu ya shaka zangu
Asilimia 58 ya wanawake wali kiri kuwa mawazo mengi na shaka zilikuwa vyanzo vikuu vya kuto fika kilele wakati wa ngono
Sababu zingine kuu zilikuwa:
- Asilimia 48 walikosa hisia za kimapenzi
- Asilimia 40 walisema kuwa kuto kuwa na wakati tosha kuliwazuia kufika kilele
- Asilimia 28 wali ripoti kuwa na mawazo na hisia hasi kuhusu miili yao
- Asilimia 25 walisema kuwa uchungu wakati wa ngono ulikuwa tatizo kuu
- Asilimia 24 walisema kuwa hawa tayarishwi vya kutosha wakati wa ngono
- Asilimia 17 wali laumu matatizo ya kiafya
Kulingana na watafiti walio ongoza utafiti huu, kuna uwezekano wa mwanamke kuwa na zaidi ya sababu moja. Kwa mfano, mwanamke anaweza kuwa na mawazo mengi na kukosa kutayarishwa vya kutosha kabla ya kitendo cha kufanya mapenzi.
Jinsi ya kukabiliana na tatizo la wanawake kufika kilele katika ngono

Utafiti una dhihirisha kuwa angalau asilimia 50 ya wanawake hawafiki kilele katika ngono. Ni muhimu kujua kuwa hauna kasoro yoyote. Kutofika kilele hakuonyeshi kuwa una tatizo.
Vyanzo vya kutofika kilele katika tendo la ndoa kwa wanawake ni hisia na mawazo yao kuhusu ngono. Uwezo wa mwanamke wa kutosheleka katika ngono kuna lingana na wanavyo fikiria kuhusu mapenzi. Wanawake wanaweza jaribu mbinu hizi kuboresha kuwa na ngono inayo pendeza.
- Kuboresha mitindo yao ya ngono
- Kuimarisha mbinu zao za mazungumzo
- Kuimarisha ubora wa uhusiano wao na kuwa makini kusikiliza wachumba wao
- Iwapo kuna tatizo la kiafya, wanandoa wanapaswa kuwasiliana na mtaalum
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Faida Za Kiafya Za Tendo La Ndoa Kwa Wanandoa