Kinacho Wafanya Wanawake Kuwa Na Wachumba Nje Ya Ndoa

Kinacho Wafanya Wanawake Kuwa Na Wachumba Nje Ya Ndoa

Kwa wanawake wengine, wao hukimbilia wapenzi wao wa awali kuhisi joto na katika visa kama hivyo, haijalishi ikiwa waume zao ni waaminifu ama la.

Huenda nambari ya wanawake walio olewa wenye wachumba huku nje ika kushtua. Sio wazi kama ya wanaume walio oleka, ama haija chapishwa kiwango sawa kwa sababu ni vigumu kwao kupatikana, lakini usidanganyike kuwa wanawake katika ndoa hawana tabia ya kutoka nje ama kiwango kidogo chao hufanya hivi.

Lakini, kipi kinacho wafanya wanawake katika ndoa kutoka nje?

wanawake kutoka nje ya ndoa

  1. Kupuuzwa

Ikiwa maisha yasiyo na doa ama hadithi za mitandaoni ni za kuaminika, bila fiche wanaume walio oa hawana uwoga kutoka nje ya ndoa hata baada ya kuapa kuwa waaminifu katika ndoa.

Na wengi wao hufanya hivi kwa kupuuza wake zao ambao mahitaji yao ya kupendwa huwafanya kuishia mikononi mwa wanaume wachanga kuwaliko.

2. Mapenzi ya hapo kale

Kwa wanawake wengine, wao hukimbilia wapenzi wao wa awali kuhisi joto na katika visa kama hivyo, haijalishi ikiwa waume zao ni waaminifu ama la, inachukua kukutana mara moja tu ama kuwasiliana na wachumba wao wa hapo awali kurejesha hisia za hapo awali ambazo walidhania kuwa hazipo tena.

3. Kutoka nje kulipiza kisasi

Kwa wanawake ambao waume wao wame onyesha uraibu wao wa kutoka nje ya ndoa bila kuhisi huruma, kupata egemezo la kihisia na kutoshelezwa kimapenzi nje ya ndoa huenda likaonekana jambo la kawaida na lisilo na athari hasi.

4. Mahitaji ya ngono bora

Mara zingine, huenda ukapata kuwa baada ya kuwa kwa ndoa kwa muda mrefu, wana ndoa wanakosa hamu ya kufanya mapenzi ama yana onekana kama kazi. Ikiwa mwanamke ana hamu ya juu ya ngono ambayo bwana yake hana, nafasi kubwa ni kuwa mwanamke huyo atakuwa na majaribio ya kutoka nje ya ndoa kutafuta ngono ya kusisimua itakayo mtosheleza.

Mara nyingi, baada ya kupata mtu anaye watosheleza, huenda wakakosa kurudi tena. Na kufanya tendo hili liwe uraibu kwao.

5. Kufuatia sababu za kifedha

Mara kwa mara, huenda wanawake waka jiingiza katika uchumba nje ya ndoa ili kupata fedha. Pale ambapo waume zao hawakimu mahitaji yao ya kifedha, huenda baadhi ya wanawake waka pata majaribio ya kupata wachumba nje ya ndoa wenye fedha zaidi.

Soma Pia: Utafiti: Wanawake Wenye Wanaume Wa Kuvutia Huwa Na Nafasi Zaidi Za Mitindo Ya Lishe Isiyo Ya Afya

Written by

Risper Nyakio