Wasichana Wa Shule Kenya Kushiriki Ngono Ili Wapate Pedi Za Hedhi

Wasichana Wa Shule Kenya Kushiriki Ngono Ili Wapate Pedi Za Hedhi

Umasikini wa hedhi una wa athiri wasichana wengi nchini Kenya na kuwafanya watumiwe vibaya kingono ili wapate bidhaa hizi.

Huku Kenya, kuna idadi kubwa ya wasichana wa shule kushiriki ngono ili kupata bidhaa za usafi wa hedhi. Hii ni kwa sababu ya asilimia kubwa ya umasikini wa hedhi na kuona haya, kutengwa na kukosa ujumbe kwa wanajamii kuhusu vipindi vya hedhi.

Unicef  imeongea kuhusu utafiti ulio gundua kuwa asilimia 10 ya wasichana walio komaa walikiri kujihusisha katika ngono ili wapate kununuliwa bidhaa za hedhi katika upande wa magharibi mwa nchi. Utafiti uligundua kuwa asilimia 54 ya wasichana Kenya walikumbana na changamoto za kupata bidhaa za usafi wa hedhi na asilimia 22 ya wasichana wa umri wa kujiunga na shule ilidhihirisha wali nunua wenyewe bidhaa za usafi wa hedhi.

wasichana wa shule kushiriki ngono

Akihojiwa na The Independent, Andrew Trevett,Mkurugenzi mkuu wa Unicef Kenya wa Water, Sanitation and Hygiene, alisema kuwa kituo cha utu kilipata kuwa ni kawaida kwa wasichana kutumika vibaya kingono ili wanunuliwe vifaa vya usafi wa hedhi.

"Tuna vijana wanaondesha pikipiki wanao fahamika kama boda boda wanao fanya ngono na wasichana ili waweze kununuliwa pedi za hedhi," walisema. "Hii inatendeka kwa sababu mbili. Moja ni umasikini- wasichana na wanawake hawana uwezo wa kifedha wa kununua bidhaa za usafi."

Aligundua kuwa imani za kale zinazo husishwa na hedhi nchini Kenya husababisha wanawake na wasichana kukosa ujumbe tosha kuhusu hedhi.

"Kukosa kujadili kuhusu hedhi za mwezi kuna maana kuwa wasichana na wavulana hawapati ujumbe wowote. Unge tarajia hii kuwa mada ya mjadala kati ya mama na bintiye ila inaonekana kuwa mambo hayako hivyo. Pia, hakuna ujumbe kutoka shuleni," alisema.

Soma Zaidi Kuhusu Wasichana Wa Shule Kenya Kushiriki Katika Ngono Ili Kupata Pedi

Kenyan School Girls Having Sex

Umasikini wa hedhi ni tatizo lililo tapakaa nchini Kenya kote, huku UNICEF ikipata asilimia 7 ya wanawake na wasichana wakitumia nguo nzee, na vipande vya blanketi, manyoya, matope na gazeti. Asilimia 46 ilitumia pedi za kutupa na asilimia 6 ilitumia pedi ambazo zinaweza tumika tena.

Cha zaidi ni kuwa asilimia 76 ya wanawake na wasichana walikumbana na tatizo la kupata maji na vifaa vya usafi vya hedhi na asilimia 17.5 peke yake ya vituo vya masomo vilikua na maji tosha karibu na vyoo na pia vifaa vya kunawa mikono na sabuni.

Asilimia 30 ya shule zilizo hojia Kenya zilikuwa na pedi za usafi za wanafunzi wake, ila katika nafasi nyingi, pedi zilipeanwa kwa wakati wa dharura tu.

Agnes, ambaye ni mwanafunzi wa miaka 15 wa kutoka kaunti ndogo ya Kuria West, ameshuhudia upande mbaya wa umasikini wa hedhi.

"Vipindi vyangu vya hedhi vilianza siku ya shule ya kawaida. Niliamka na kwenda shuleni kama kawaida," alisema. "Kipindi changu cha hedhi kilianza katika darasa ya kimombo. Niliogopa kumweleza mwalimu wangu na pia nilikuwa na hofu kuwa wavulana wangenicheka."

Ariana Youn, mtaalum wa Unicef Kenya Communication and Advocacy, alieleza kuanza kwa kipindi cha hedhi kwa msichana mdogo kwa kawaida kunaonekana kama ishara ya kukomaa, na kuashiria kuwa wamefika umri wa kuoleka.

Wasichana wa Kenya kujihusisha katika ngono: Mada ya hedhi haikubaliki

wasichana wa shule kushiriki ngono

"Wazazi wana shaka za watoto wao kupata mimba, na sababu hii huwafanya wajitenge na mijadala kuhusu vipindi vya hedhi. Wanajaribu kuwafanya wasichana wajitenge na chanya cha kuuliza kuhusu ngono ama kujihusisha katika kufanya ngono," aliiambia The Independent. "Baadhi ya jamii hutizama hedhi kama mwanzo wa uke na kuona kama wako tayari kufunga pingu za maisha,"

Ni vyema kujua kuwa ndoa za mapema huongeza nafasi za watoto hawa kupata mimba. Pia kusababisha kujifungua bila nafasi tosha ya miaka kati ya watoto wano zaliwa na hivi kwamba kuongeza matatizo kama obstetric fistula.

Bi Youn, alieleza bayana athari ambazo hedhi huenda zika sababisha kwa maisha ya wasichana wachanga Kenya.

"Baadhi ya wasichana na wanawake bila kupata taulo za hedhi hutumia hiari yoyote iliyoko karibu. Watachimba shimo kwenye mchanga na kuchuchuma hapo kwa siku wanapokuwa katika vipindi vya hedhi. Hii ndiyo sababu kubwa kwa nini wasichana wengi hubaki nyuma shuleni na kukosa vitu vingi. Wasichana wana jihusisha katika ngongo na vijana wa boda boda kwa sababu wana nguvu, pesa na uwezo wa kununua taulo hizi."

 Wasichana wa shule kushiriki ngono: Kukosa elimu kuhusu vipindi vya hedhi nchini.

Imani zisizo za kweli kuhusu vipindi vya hedhi ni nyingi sana. Imani zilizo maarufu zaidi kuhusu vipindi vya hedhi ni kuwa zinakufanya kuwa mwenye dhambi na mchafu. Hedhi ni ugonjwa ama laana. Na chakula huharibika unapo ingia jikoni unapokuwa katika kipindi chako cha hedhi. Na mimea pia hufa unapo enda shambani huku ukiwa katika kipindi chako cha hedhi.

Cha zaidi ni kuwa, watu wengi huamini kuwa unaweza zirai kufuatia kupoteza damu nyingi. Pia, unaweza kosa kutunga mimba unapo jihusisha katika ngono unapokuwa na kipindi chako cha hedhi.

Kutengwa kunako onekana unapokuwa na mimba kuna shuhudiwa Afrika kote. Moja kati ya wasichana kumi Afrika hukosa kwenda shuleni wanapokuwa wakishuhudia kipindi chao cha mwezi. Pia kukosa choo zilizo salama.

Bila hata kusema, kama ilivyo desturi, wasichana wanapokosa kwenda shule, nafasi nyingi ni kuwa watalazimishwa kuoleka wangali wachanga.

Hata hivyo, nchi ya Kenya imekuwa ikijitahidi katika nyanja hii. Shukrani kwa serikali, Unicef na washirika wengine. Karibu wasichana 90,000 walio katika shule 335 kwa sasa wanaweza pata vitambaa safi vya hedhi ikiwemo vifaa vingine muhimu.

Kumbukumbu: The Independent and UNICEF

Soma pia: UNICEF says 47 Million Nigerians Practice Open Defecation

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio