Baadhi ya jinsi za kupunguza matukio ya watoto kuzama kwa maji

Baadhi ya jinsi za kupunguza matukio ya watoto kuzama kwa maji

Visa vya watoto wachanga kuzama kwenye maji ni nyingi zaidi. Ni muhimu kwa mama aliye na mtoto mchanga kufanya jitihada kuhakikisha kuwa anamlinda mtoto wake mchanga kutokana na visanga hivi.

Watoto wana maswali mengi kuhusu dunia inayo wazingira. Pamoja na ustadi wa kimwili unao kua, nyumbani kwako kunakuwa mahali pa kustahabisha na dunia wanayo taka kujua zaidi kuihusu. Na pia mahali hatari kama hawana wa kuwaangalia. Wana weza ingia taabani mahali pasipo kusudiwa- ikiwepo watoto kuzama kwa maji nyumbani. Ni muhimu kwa wazazi kujua jinsi ya kuepuka mikasa nyumbani.

 

 Hivi karibuni, mtoto mchanga alizama kwa ndoo ya maji, kuwakumbusha wazazi umuhimu wa kujua jinsi ya kuepukana na mikasa ya kuzama kwa maji wakiwa nyumbani na hata nje.

 

Jinsi ya kuepuka mikasa ya kuzama kwa maji: mtoto mchanga azama katika ndoo ya maji nyumbani

Mtoto mmoja wa miezi 14 alizama kwa maji, baada ya kujitumbukiza kwa ndoo ya maji nyumbani.

Mamake alikimbia msalani baada ya Kuziskia sauti za maji ikimwagika kumpata mtoto wake bila uhai. Kijana yule mchanga alikua ndani ya ndoo kichwa kikiwa chini. Alimuita mumewe mbio aje amsaidie. Wanandoa hawa walikuwa wanakichukua chakula chao cha mchana tukio hili lilipo tendeka. Mama alisema kuwa ndoo hii ilikuwa bure kwani alikuwa anaitumia kumwoshea ndugu yake mkubwa, mapema siku hiyo.

Kijana huyo alikimbizwa hospitalini, ila alisemekana kuaga dunia na wauguzi hospitalini.

Kesi hii ili ainishwa kama kifo cha ghafla.

Hakuna maumivu yaliyo patikana mwilini mwa kijana yule aliye kuwa amevalishwa diaper peke yake. Polisi hawakupata ushahidi wa uhalifu ama michezo mibaya ilhali uchunguzi bado unaendelea.

Jinsi ya kuepuka mikasa ya kuzama kutendeka nyumbani

Ni rahisi sana kwa watoto wachanga kuzama kwa maji. Kuna uwezekano wa watoto hawa kuzama kwa maji kidogo kama sentimita 2.5 na inawezekana kwa chini ya dakika moja. Kwa hivyo si kwa dimbwi za maji na dimbwi za watoto peke yake zinazo hatadharisha maisha ya mtoto ila pia vitu usivyo kusudia kama sinki za bafu na pia ndoo za maji.

 

Hakikisha unawachunga watoto kwenye bafu.

Hizi ni baadhi ya njia za kuepuka mikasa ya kuzama nyumbani kutendeka.

  • Usiwai muacha mwanao bafuni peke yake. Hata kama una jambo la dharura unalo hitaji kuliangazia nyumbani, kama vile kumfungulia mtu mlangoni ama kujibu simu, Funika mtoto wako na taulo na umbebe popote uendapo naye. Usi kusudie ndugu zake wakubwa kumchunga- hata kumwacha kidogo inaweza hatadharisha maisha yake.
  • Borake una mtoto kwa nyumba, usiwache maji yamejaa kwa nyumba. Kwa vyombo kama ndoo, bafuni na vyombo vyovyote kwenye bafu ama jikoni
  • Kama inawezekana, eka kifuniko cha msalani kimefungwa wakati wote. Pasi na hivyo, kumbuka kuuweka mlango wa bafu yako umefungwa wakati wote na uwakumbushe ndugu zake wakubwa
  • Kama ni bafu ya kukalia, inafaa kutumika kwa mtoto chini ya usimamizi wako.
    Kwani mkasa wowote unaweza tendeka kwa bahati mbaya na mtoto kupinduka na kuzama kwenye maji.
  • Chukua darasa la kinga ya kwanza na CPR
    Tenga wasaa wa kusoma CPR na kinga ya kwanza ili uweze kufanya upesi kumwokoa mtoto wako kunapo kuwa na jambo la dharura.

Read Also: Afrobeats Star D’banj Loses Son In Swimming Pool Drowning: Pool Safety Tips

 

Written by

Risper Nyakio