Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Daktari Toka Kenya Aeleza Kwa Nini Watoto Wa Kiafrika Hawalii

3 min read
Daktari Toka Kenya Aeleza Kwa Nini Watoto Wa Kiafrika HawaliiDaktari Toka Kenya Aeleza Kwa Nini Watoto Wa Kiafrika Hawalii

Lala na mtoto wako. Wakati mwingi, utamlisha mtoto wako kama hajaamka kabisa, na kumaanisha kuwa atarudi kulala bila kutatiza na kukuwezesha kupumzika zaidi.

Wakati ambapo Claire Niala alipata mimba, alifanya vitu ambavyo wanawake wengi wanao tarajia watoto wanafanya.  Alianza kusoma vitabu kuhusu ulezi, huku akianza kujitayarisha kuwa mama bora kadri awezavyo. Na vingi kati ya vitabu hivi viliongea kuhusu kitu sawa- watoto wa kiafrika hawalii. Ama hawalii sana wakilinganishwa na watoto wa Uingereza.

Hili ni kweli? Claire aliamua kufanya majaribio mwenyewe. Alichukua ushauri kutoka kwa nyanyake wa Africa. Na kunyonyesha mtoto wake asipokuwa na furaha, kulala akilala na kunywa maji moto kabla ya kulala kuboresha utoaji wa maziwa yake.

Haikua safari rahisi. Wakati ambapo watoto wa marafiki zake walikuwa wana anzishwa chakula kigumu. Wake alizidi kunywa maziwa ya mama na kumaanisha kuwa alhitajika kuamka angalau kila baada ya masaa mawili. Alipo jumuika na watu wengine kwenye sherehe za harusi, watu walisema jinsi mtoto wake alivyo onekana kuwa mtulivu na kuto sumbua.

Imani za nyanyake Claire

watoto wa kiafrika hawalii

  • Mpe mtoto wako titi anyonye kila anapo kasirika- hata inapo maanisha umlishe tena
  • Lala na mtoto wako. Wakati mwingi, utamlisha mtoto wako kama hajaamka kabisa, na kumaanisha kuwa atarudi kulala bila kutatiza na kukuwezesha kupumzika zaidi
  • Wakati wowote kunywa maji ya vuguvugu kabla ya kulala ili kukuwezesha kuwa na maji tosha mwilini na kuboresha utoaji wa maziwa
  • Patia kipau mbele kumlisha mtoto wako na uwakubalishe walio karibu nawe kukufanyia mengi wawezavyo
  • Msome mtoto wako, sio vitabu

Mambo haya yalifuzu kwa Claire hata ingawa yana uchukua muda mwingi.

Ni sawa mtoto wako anapo lia hata kama, watoto wa kiafrika hawalii.

Walakini, wamama wengine wame jaribu imani hizo na hazikufuzu kwao.

"Wakati ambapo wasichana wangu walikuwa watoto, nilifanya mambo mengi ambayo wazazi wengi wakiafrika wanaweza kuwafanyia watoto wao.." alisema mama mmoja. Alimlisha mtoto wake alipo taka, na kumbeba mtoto wake badala ya kutumia kijigari cha watoto.

"Lakini na kwambia, watoto wangu wamelia, wamelia sana. Nilianza kuhisi vibaya nilipo ona habari hizo zinatapakaa kwenye Facebook kuwa watoto wa kiafrika hawalii."

watoto wa kiafrika hawalii

Na wingi wa vyanzo vya ulezi vinavyo dai kuwa na majibu ili vina utatanishi, mmoja atajuaje kilicho bora kwa mtoto wake?

Kuna jambo moja ambalo nyanyake Claire alimwambia la maana zaidi-"Soma mtoto wako, na wala sio vitabu."

Mwishoni mwa siku, kila mtoto ni kiumbe. Usiangazie saizi moja inawatosheleza wote katika ulezi. Ikiwa una tatizika kutoa maziwa tosha ya mtoto wako, huenda ikawa kunyonyesha sio jibu kwako. Ama pengine mtoto wako ana penda kulala peke yake badala ya kulazwa akinyonya. Haimaanishi umefeli kama mzazi, la hasha. Kumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti, kila mzazi ni tofauti na ulezi uta tofautiana.

Lakini ikiwa una masuala yoyote kuhusu afya ya mtoto wako, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wa mtoto wako.

Soma Pia:Maisha Baada Ya Mtoto Kuwasili: Mambo Ambayo Hukufahamu!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Daktari Toka Kenya Aeleza Kwa Nini Watoto Wa Kiafrika Hawalii
Share:
  • Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

  • Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

    Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

  • Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

    Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

  • Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

    Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

  • Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

  • Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

    Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

  • Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

    Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

  • Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

    Kanuni 5 Za Ulezi Wa Kiislamu Unazo Paswa Kujua

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it