Hofu Yatamba Huku Idadi Ya Watoto Wachanga Waliopachikwa Mimba Ikiongezeka

Hofu Yatamba Huku Idadi Ya Watoto Wachanga Waliopachikwa Mimba Ikiongezeka

Nchi ya Kenya ina huzuni nyingi baada ya ripoti moja kudhibitisha kuwa watoto zaidi ya 4,000 wamepachikwa mimba katika kaunti ya Machakos.

Ni wakati wa kuhuzunisha baada ya ripoti iliyo fanyiwa kudhibitisha kuwa zaidi ya watoto 4,000 wamepachikwa mimba katika kaunti ya Machakos. Hii ni idadi kubwa sana katika kipindi cha miezi isiyo zidisha minne. Idadi hii ilidhibitishwa na Afisa mkuu wa watoto wa kaunti ya Machakos. Jambo hili limeibubuwaza nchi, huku likiwafungua wazazi mimba na serikali macho. Suala la watoto wadogo kupachikwa mimba limezua mijadala tofauti nchini kote.

watoto wachanga kupachikwa mimba

Watoto Wadogo Kupachikwa Mimba

Wasichana hawa waliopata mimba wana umri mdogo na wako kati ya miaka 15 na 19, hii ina maana kuwa wangali sekondari ama shule ya msingi. Macho yote yaliwageukia wazazi na kila mtu akawa na swali iwapo wazazi wame feli katika jukumu lao la kuwachunga na kuwaongelesha watoto wao. Kwa sababu wao ndiyo wamekuwa wakiishi na watoto hawa kipindi hiki cha lockdown Kenya. 

Daktari Alfred Mutua gavana wa Machakos aliwashauri wazazi kuongea na watoto wao, wa kike na wa kiume. Kuwaongelesha watoto wao kuhusu athari za kufanya ngono kama vile kupata mimba ama hata kupata maambukizi ya kingono kungewasaidia wanapo fanya uamuzi. Kulingana na gavana wa kaunti hii, watoto hawa walishiriki ngono na watu wa rika lao. Kumaanisha kuwa wote ni wanafunzi wa shule na huenda walikuwa wanajaribu kitendo hiki bila kujua athari zake. Hakutupilia kuwa baadhi ya visa hivi vya ujauzito vili tendeka na wanaume wakomavu. Kwa hivyo, ni vyema kwa wazazi kuwa na mjadala wazi na watoto wao kuhusu mambo haya na kuwa ambia mambo wanayo paswa kufanya na wasio paswa kufanya.

ishara za kunyanyaswa kimapenzi

Kulingana na maafisa wanaohusika na mambo ya watoto, walishuku kuwa huenda kuna visa vya watoto wenye mimba ambavyo bado havijaripotiwa na idadi hii huenda ikawa juu kuliko iliyoko kwenye ripoti. Kuna huzuni kwani ikiwa kaunti moja inaweza rekodi idadi kubwa hivyo ya watoto wadogo kupachikwa mimba, ni bayana kuwa idadi ya watoto wadogo hasa wa shule walio na mimba katika kipindi hiki cha lockdown Kenya ni kubwa zaidi.

Soma pia: Watoto Washule Kenya Washiriki Ngono Ili Wapate Pedi Za Hedhi

Written by

Risper Nyakio