COVID-19: Jinsi Ya Kuhakikisha Kuwa Watoto Wameburudika Nyumbani Bila Runinga

COVID-19: Jinsi Ya Kuhakikisha Kuwa Watoto Wameburudika Nyumbani Bila Runinga

Kutoka kutengeneza vyakula hadi kuoka mikate hadi kucheza michezo hata na nyanya zao.

Ni wakati wa kutatiza kwa wazazi wa watoto wachanga na wa wastani ama vijana. Na virusi vya homa ya korona vikisisitiza watu kubaki nyumbani, wazazi na watoto. Na woga wa kulazimisha familia kuwa nyumbani katika wakati wote, mazingara ya familia huenda yakawa ya kukwaza kadri joto ya nyumba inapo kushika. Zaidi ya hapo awali, wazazi watahitaji vidokezo vya jinsi ya kuweka watoto wako wameburudika nyumbani.

Jaribu kuhakikisha kuwa watoto wako wameburudishwa wakati wote na wakati ule bado uki dhibiti utumizi wa kiteknolojia kama vile ipads, tablets na rununu hata ingawa huenda likawa tatizo. Na wasiwasi wa wazazi kuhusu wakati wa runinga huwa kweli.

Utafiti wa muda wa miaka minne na Chuo Kikuu cha Hong Kong kilicho achiliwa mwaka wa 2017, kili dhihirisha kuwa watoto wanaopata zaidi ya masaa mawili ya kutazama runinga kila siku walikuwa na uwezekano zaidi wa kuwa na kilo zaidi na hatari kubwa ya matatizo ya kitabia.

Kusaidia kupambana na kuboeka kwingi, hapa kuna maoni 5 ya jinsi ya kuhakikisha watoto wako wameburudika wakiwa nyumbani wanapozidi kujiepusha na virusi vya korona.

Jinsi ya Kuhakikisha Watoto Wako Wameburudika Nyumbani

watoto wako wameburudika nyumbani

1. Shamba la ndani ya nyumba

Kuishi katika mazingira ya kisasa kama vile Hong Kong huenda ikasababisha utangamano kati ya "mtoto na mazingira" kwa hivyo ni muhimu sana kutafuta njia za kuhamasisha dhamana hii. Njia mojawapo ya kuleta vitu vya nje ndani ya nyumba kutumia mimea ni mimea ya msimu ya jikoni ama hata shamba la ndani. Njia zote rahisi za kupata rangi ya kijani  kwenye nafasi ndogo na kufanya iwe na rangi ya kuvutia na hewa safi. Kukuza mimea kutoka kwa mbegu pia kunampatia mtoto wako masomo muhimu kuhusu mazingara na sayansi. Hakuna hisia njema zaidi kuliko kuongeza mimea ya misimu ya nyumbani kwa lishe iliyo tayarishwa na familia.

watoto wako wameburudika nyumbani

2. Chezeni michezo ya mbao ama ya puzzles

Nyumba nyingi huwa na michezo ya mbao ama puzzle zilizo hifadhiwa kwenye kabati ya juu. Kwa hivyo huu ni wakati mwema wa kuzichukua na kuzipanguza vumbi kisha kuanza mahusiano ya kifamilia ya hapo awali. Wakati ambapo michezo ya video ina maana kuu katika maisha ya watoto wa leo, kuna anuwai pana kwenye mtandao. Michezo ya asili ya mbao itasaidia kuunda hali ya kufurahikia ya familia na kupunguza wakati wa runinga.

Puzzles ni njia ya nzuri ya kutangamana na wakati ambapo huenda ikaonekana na shughuli nyepesi, utafiti umedhihirisha kuwa ni njia ya nguvu ya akili kufanya zoezi. Hasa kwa watu wa miaka ya makamo ama watu wanaoishi na ulemavu wa kupoteza kumbukumbu ama dimentia. Kwa hivyo ni wazo nzuri kuwahusisha nyanya na babu zako.

 

watoto wako wameburudika nyumbani

3. Tengeneza kinyunya cha kucheza

Shaka kuhusu idadi ya sumu kwenye vidoli vya watoto ni shaka kuu kwa wazazi wengi; na za bei ya chini, kinyunya cha kucheza chenye kemikali kina tia wasi wasi mwingi; kwani watoto wadogo huenda wakapata majaribio ya kula kinyunya hiki chenye rangi. Suluhisho la tatizo? Tungeneza kinyunya nyumbani kisicho kuwa na kemikali.

Kufanya iwe rahisi zaidi, ongeza mchanganyiko wa unga, mafuta, chumvi na rangi ya chakula. Tizama mojawapo ya maagizo ya kupika na video zilizoko kwenye mtandao.

watoto wako wameburudika nyumbani

4. Elekea jikoni

Ikiwa ni kutengeneza chakula ama kuoka mkate, kutayarisha na kula kwa pamoja kuna nguvu za kuleta familia pamoja. Kazi za jikoni pia zinasaidia mtoto na nafasi ya kupima, na kuhesabu na kuona jinsi chakula kinavyo geuka na kufanya njia nzuri ya kuanzisha hesabu na kisayansi kwenye siku yao. Kupika pia husaidia watoto kuwa na fahari na kuongeza ujasiri wao.

Utafiti pia umeonyesha kuwa kula pamoja kama familia kuna umuhimu."Utafiti unadhihirisha kuwa lishe za familia zina endeleza ulaji wa afya" matunda mengi, mboga na fibre; chukula zilizo punguka za kukaangwa; na vyenye kalori ndogo," asema mtaalum wa afya ya lishe aliye sajiliwa na msemaji wa Academy of Nutrition and Dietetics Angela Ginn. "Na lishe za familia zinafanya kazi zaidi kuliko kuwekelea lishe mezani.

"Zaidi na kutayarisha vyakula vyenyewe, wakati mwingine sisi husahau kuwa wakati wa lishe ni nafasi ya kuongea na kukuza uhusiano wa kifamilia. Na pia ni nafasi ya wazazi kuwa mifano miema ya kuigwa ya kula vyakula vya afya," Ginn anasema, kuongeza wakati wa lishe lazima uwe wakati bila rununu ama runinga.

5. Kuwa mbunifu

Mtu anapokuwa amejitumbukiza kabisa kwenye shughuli za ubunifu, wanaweza pata aina ya kufikiria; jina lililo patikana na mwanasaikolojia wa Hungarian-American Mihaly Csikszentmihaly inayo elezea jinsi ya kuwa makini zaidi ambapo tuma hisi na kufanya vyema zaidi.

Hii huenda ikaonekana kama sababu njema ya kuhamasisha ubunifu; njia moja ya kufanya hivi ni kwa kupitia sanaa na ufundi. Njia zingine za kusoma mojawapo ya uwezo wa ubunifu kama vile kucheza gitaa. Na ambapo uko katika hali ya kutaka kusikiza muziki. Mbona usiandike nyimbo zako na uanzie sherehe ya kusakata densi?

Makala haya yalionekana kwenye South China Morning Post (SCMP), sauti ya mamlaka zaidi ya kuripoti kuhusu Uchina na Asia kwa zaidi ya mwongo mmoja. Kwa hadithi zaidi za SCMP, tafadhali itembelee kurasa ya SCMP app ama utembelee kurasa ya mtandao wa kijamii wa  Facebook na Twitter . Copyright © 2020 South China Morning Post Publishers Ltd. All rights reserved.

Copyright (c) 2020. South China Morning Post Publishers Ltd. Haki zote zimehifadhiwa.

Makala haya yame andikwa tena kutoka kwa makala asili yaliyo andikwa na South China Morning Post  na kuchapishwa tena na TheAsianparent

Soma pia: Covid-19: How To Survive A Lockdown In Nigeria

Written by

Risper Nyakio