Je, ungependa kuwa na watoto wangapi? Nini unacho angalia kudhiti idadi ya watoto ambayo ungependa kuwa nayo? Tazama manufaa ya kuwa na watoto wawili katika familia.
Faida za kuwa na watoto wawili katika familia
Fedha

Watoto ni gharama. Wanahitaji pesa nyingi kukimu mahitaji yao ya lishe, mavazi, kutunza afya yao na kadhalika. Wanahitaji kutunzwa kabla ya kuingia shule na wanapoingia, ni gharama kubwa kulipia karo yao ya shule na mahitaji yote kabla ya kuanza masomo. Haya ni mahitaji ya kijumla, kuna mahitaji mengine kama vile kuwanunulia vidoli, vitamu tamu kila mara mnapo tembea, nepi na manunuzi yasiyo pangiwa. Hii ni mojawapo ya motisha kwa wazazi kubaki na watoto wawili.
Nishati sawa kwa watoto wote
Ni vigumu kuwatunza watoto wote na kuwapa nishati sawa hasa wanapokuwa zaidi ya wawili. Wanandoa wanapokuwa na watoto wawili, kila mmoja anaweza tunza mtoto mmoja na kuwasaidia kupata wakati wakuwa pamoja. Je, unaona sababu zaidi kwanini kuwa na watoto wawili ni bora?
Kutumia vitu vya mtoto wa kwanza kwa wapili
Mtoto wa pili anaweza kutumia vitu vya kifungua mimba na vitu hivi bado vitakuwa katika hali nzuri. Kwa njia hii, mzazi ana hifadhi pesa ambazo angetumia kununua bidhaa hizo, na pia mtoto wa pili anaweza kutumia vitu ambavyo havija zeeka sana.
Uhusiano mzuri kati ya watoto

Ndugu waliozaliwa wawili huwa na umoja kwani hawana mtu mwingine. Jambo linalo wafanya kuwa na uhusiano wa kindani na kusaidiana mmoja anapopatwa na tatizo. Tofauti na familia walio na ndugu zaidi ya wawili, kunapokuwa na tatizo, wataanza kuchukua pande, na huenda mmoja akahisi kana kwamba hana rafiki kwa hiyo boma ama hapendwi kama wengine.
Kwa wazazi walio na mtoto mmoja na wangependa kupata mwingine, ni vyema kumtayarisha mtoto wa kwanza. Huenda kifungua mimba akahisi kana kwamba ametemwa na wazazi hawana wakati wake. Hivi ataanza kumwonea wivu na kumchukia ndugu yake. Ila wazazi wanapo mtayarisha na kumdhibitishia kuwa hakuna mabadiliko yatakayo fanyika na bado atazidi kupendwa, atakuwa na mtazamio mpya kwa ndugu yake mdogo.
Hata hivyo, ni vyema kwa wazazi kuto puuza matakwa ya kifungua mimba chao hasa mtoto mdogo anapozaliwa. Tenga wakati wa kuwa na kifungua mimba hata baada ya kujifungua. Kuwa na watoto wawili katika familia kuna manufaa mengi kwa wazazi. Ila, kila mtu ana mtazamio wake kuhusu familia ambayo angependa kuwa nayo. Ikiwa ungependa kuwa na familia kubwa, bila shaka huo ni uamuzi wako.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Jukumu La Baba Katika Familia Na Maisha Ya Watoto Wake