Watoto 13 Maarufu Wanao Badilisha Ulimwengu Na Talanta Zao

Watoto 13 Maarufu Wanao Badilisha Ulimwengu Na Talanta Zao

Unaweza waita watoto wenye talanta za kububuwaza zaidi duniani kote, ila kitu moja kinabaki kuwa sawa: watoto hawa wame barikiwa kwa njia tofauti. Tuna angazia watoto 13 walio na talanta zaidi duniani kote.

Watoto Wenye Talanta Duniani Kote!

1. Autumn de Forest, USA

Autumn de Forest alikuwa na miaka saba wakati ambapo Discovery Channel ilimtambua kama genius. Uwezo wake wa kupaka rangi hautoshanishwi. Ana barua ya kujiunga na chuo cha Havard na kazi yake imetambulika katika museums zote Umarekani.

watoto wenye talanta

2. Onafijiri ‘Fuji’ Remet, Nigeria

Fuji alijulikana na watu alipokuwa miaka mitatu. Tayari alikuwa mpiga picha mashuhuri kwa umri mchanga hivyo. Pamoja na kamera iliyo kuwa na urefu kama wake, Fuji alichukua picha za maisha ya kila siku ya Lagos yalivyo kuwa. Ana zaidi ya picha 3000 kwenye jina lake.

modern child prodigies

3. Akrit Pan Jaswal, India

Akrit alifanya upasuaji wake wa kwanza alipokuwa miaka saba. Hakuwa na shahada yoyote ya kimatibabu ama liseni ya kufanya hivi, ila alifanikiwa kufanya upasuaji wa vidole kwa mtu aliye chomeka. Akrit alienda shule ya kimatibabu alipokuwa na miaka 12. Kwa sasa, mtoto huyu mwenye talanta anatafuta matibabu ya saratani.

modern child prodigies

4. March Tian Boedihardjo, Hong Kong

March Tian Boedihardjo alipata barua ya kujiunga na chuo kikuu cha Hong Kong akiwa na miaka tisa na kumfanya mtu mchanga zaidi kujiunga na chuo hicho. Alikuwa mwanafunzi mchanga zaidi katika darasa lake. Na pia alihitimu mwaka mmoja kabla ya watu wengine wote. Kwa sasa anasomea PHD ya hesabu.

modern child prodigies

5. Akim Camara, Germany

Akim Camara alikuwa stadi wa kucheza violin alipofikisha miaka miwili. Alipofikisha miezi mitatu, alianza kuigiza watu katika sherehe za krismasi. Mwalimu wake wa violin aligundua kuwa mtoto huyu alikuwa na uwezo wa kuigiza kwa ustadi hata kabla aanze kuongea.

modern child prodigies

6. Tanishq Matthew Abraham, Indian-American

Tanishq alikuwa na miaka minne alipo kuwa mshirika wa Mensa. Katika umri wa miaka mitano, aliweza kukamilisa Standford University's Education Program ya watoto wenye talanta katika kipindi cha miezi sita. Katika umri wa miaka sita, Tanishq alikuwa tayari ameanza masomo ya chuo kikuu na kupata GPA ya 4.0 katika kosi zake zote.

modern child prodigies

7. Taylor Ramon Wilson, USA

Katika mwaka wa 2008, Taylor Wilson wa miaka 14 alijenga nuclear reactor na kumfanya mtu mchanga zaidi duniani kote kufanya hivi. Kabla ya hapa, alikuwa amejenga kilipuzi akiwa na miaka 10. Taylor Ramon alifaidika na Thiel fellowship na mshirika wa Helena Group.

modern child prodigies

8. Amira Willighagen, kutoka Netherlands

Amira aliwaacha watu na bubu wazi alipo enda kwa stegi ya Hollands Got Talent na kuimba. Alikuwa na umri wa mika tisa wakati huo. Sauti yake iliwashangaza watu wengi hata ma jaji. Alipatiwa tikiti ya dhahabu na akajiunga na televisheni ya maisha ya kweli. Cha kushangaza ni kuwa mtoto huyu hakuwa amefunzwa jinsi ya kuimba.

watoto wenye talanta

9. Umi Garrett, USA

The Huffington Post imemtambua Umi Garrett kama ‘a budding musical genius.’ Msichana huyu mchanga anaye cheza piano amejulikana duniani kote baada ya kuonekana katika programu ya Ellen Degeneres alipokuwa umri wa miaka minane. Uwezo wake wa kucheza piano ni mkuu kwa umri wake.

watoto wenye talanta

10. Ryan Wang, Canada

Katika mwaka wa 2013, Ryan Wang wa miaka 5 ambaye ni mchezaji piano alianza kuonyesha watu talanta yake katika Carnegie Music Hall. Katika mwaka uliopita, aliigiza watu pamoja na Shanghai Symphony Orchestra.

watoto wenye talanta

11. Keith O’Dell Jr., USA

Katika umri wa miaka miwili, mtoto huyu mdogo alikuwa anasimama kwa kiti kucheza pool na alishinda wakati wote. Wakati ambapo video zake zili ibuka kwenye mtandao na kujulikana kama mchezaji mdogo zaidi. Yeye ndiye mwanachama mchanga zaidi katika American Pool Association.

watoto wenye talanta

12. Gregory Smith, USA

Alipokuwa wa miezi 14, Gregory Smith alikuwa tayari anatatua maswali ya hesabu. Alihitimu kutoka sekondari alipo fikisha miaka 10. Akiwa na miaka 12, aliteuliwa kwa tuzo la Nobel Peace Prize kwa usemi wake katika kazi za amani na kuboresha maisha ya watoto.

watoto wenye talanta

13. Cameron Thompson, kutoka United Kingdom

Cameron ni stadi wa hesabu, ambaye kwa miaka minne alimrekebisha mwalimu wake wa hesabu darasani. Alipatiwa barua ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Open kusomea hesabu alipokuwa miaka 11. Mafanikio yake ni ya kufana kwani ana tatizo la Asperger's syndrome.

watoto wenye talanta

Kila mtu anazaliwa na kitu spesheli, ila watoto hawa kwenye orodha yetu ya watoto wenye talanta wana badilisha dunia na vitu wanayo fanya kila wakati.

Soma piaIdentifying children with high IQ: An age-by-age guide for parents

Written by

Risper Nyakio