Kutambua Watoto Wenye Kiwango Cha Juu Cha Werevu

Kutambua Watoto Wenye Kiwango Cha Juu Cha Werevu

Mums, here's an age-by-age guide to identify children with high IQ

Je, uta wezaje kujua watoto wenye werevu mwingi? Kijana wako ni mrefu kupita umri wake? Ama mtoto wako wa umri wa miaka saba hukwamilia kwa vitabu?  Wazazi, hii huenda ikawa dalili kuwa kipimo cha werevu cha mtoto wako – kipimo cha werevu – kiko juu ya wastani. Wewe pia una watoto wenye kipimo cha juu cha werevu?

Utafiti mwingi umeonyesha viashiria muhimu vinavyotambulisha watoto wenye werevu zaidi wakizingatia umri.  Mtoto wako anavyozidi kukua na kupita awamu za huu miaka unaweza kuangalia viashiria hivi.

 Mwongozo wa kimiaka wa kutambua watoto wenye werevu mwingi

Mtoto mchanga: Kuwa na kichwa kikubwa zaidi ya wastani!

watoto wenye werevu mwingi

Kina mama, iwapo mtoto wako alikuwa na kichwa kikubwa akizaliwa ni wakati wa kusheherekea. Kulingana na utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Molecular Psychiatry, kuna uhusiano chanya kati ya ukubwa wa kichwa cha mtoto anapozaliwa, na uwezekano wa kuwa na kiwango cha juu cha werevu.

Uchambuzi wa utafiti huo ulionyesha kuwa “watoto waliozaliwa na kichwa kikubwa wana uwezekano wa kupata digrii na kufanya vizuri kwa majaribio ya kuongea na hisabati.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Kumkanda mwili mara kwa mara ilikukuza weledi wake wa mwili na kutembea
 • Kuitika mtoto wako anapobabaika na pia kumwongelesha kutaweza kukuza akili yake
 • Kumshika na kumpakata mtoto wako kutamfanya ahisi salama na imara.

Watoto wenye kiwango cha juu cha werevu, mwaka mmoja na miwili: kumfunza lugha tofauti

Kina mama, je, nyinyi huongea lugha tofauti?  Kama ndio, himiza mtoto wako kuongea lugha mbili kwa kuwaongelesha kwa lugha tofauti.

Kulingana na utafiti, kumwongelesha mtoto wako wa umri wa mwaka mmoja au miaka miwili kwa lugha zaidi ya moja hukuza uwezo wake wa akili.  Na kutamwezesha kuhesabiwa kati ya walio na kiwango cha juu cha werevu.

Watoto waliozaliwa kwa wazazi waliozungumza lugha zaidi ya moja, walifanya vizuri katika mitihani yao ya kipimo cha werevu ndivyo https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3322418/utafiti ulithibitisha.

Katika  utafiti husika wataalam Peal na Lambert  waliafikia kuwa: “Kimawazo,  mtoto aliyepitia kwa mfumo wa lugha zaidi ya moja( bilingual child)  alikuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, ukuu katika kujenga mawazo, na mseto wa uhodari wa akili.

Vidokezo vya kuboresha ukuaji wa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Unaweza kusaidia kuboresha uwezo wa kiakili wa mtoto wako kwa kuhimiza uigaji.
 • Kucheza michezo kama vile kitangangaya, peek a boo itasaidia kukuza uwezo wa akili katika huu umri.
 • Mpe mtoto wako mchaguo: “Je, unataka juisi ya matofaa au machungwa?” Hili humpa mtoto wako kujitawala ila umeshika usukani.

Miaka mitatu: ashiria yake ni kurefuka kuliko kawaida

watoto wenye werevu mwingi

Kids with high IQ: Is your 3-year-old taller than average?

Iwapo unafikiria mtoto wako ni mrefu kupita anavyofaa, kuna uwezekano atakuwa na kipimo cha juu cha werevu miaka ya baadaye.

Watoto walio na kipimo cha juu cha werevu huwa warefu kupita wengine kulingana na utafiti wa National Bureau of Economic Research.

Kundi la watafiti linasema: “mapema kama miaka matatu, kabla shule imeanza kumfunza na wakati wote wa utotoni, watoto warefu hufanywa vizuri kwenye majaribio ya kiakili.”

Utafiti unazidi kueleza kuwa, watoto warefu wana uwezekano wa kuwa warefu ata watakapo komaa. Hii ni kwa sababu uhusiano kati ya urefu kati ya watoto hadi watu wazima ni 0.7 kwa wazee na wanawake.

Watu waliokomaa walio warefu mara nyingi huchagua kazi zinazolipa vizuri ambapo maarifa ya juu ya kuongeza na hisabati inahitajika na pia werevu mkuu unahitajika.  Hii inaweza kulinganishwa na uwezo wa kiakili walipokuwa watoto.

Vidokezo vya kuboresha ukuaji wa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Mpe mtoto wako nafasi nyingi ya kucheza kwani ustadi wake wa kutembea bado unaimarika. Katika huu umri, watoto wengi huweza kujua kutembea na kukimbia bila ya kuanguka.  Pia unaweza kuhimiza matumizi ya baisikeli au baiskeli ya miguu matatu.
 • Himiza mtoto wako wa miaka matatu kuchora akitumia krayoni ama kugeuza kurusa ili kustawisha ukuaji wa akili.
 • Pia, unaweza kuanza kuwauliza maswali rahisi kama vile majina na umri wao. Uwezo wao wa lugha utachechemuliwa  na utendaji huu.

Watoto walio na kipimo cha juu cha werevu, miaka minne: uwezo wa kupaka mchoro rangi

watoto wenye werevu mwingi

Children with high IQ: Your 4-year-old’s painting skills can be a sign of their IQ.

Kina mama, iwapo mtoto wako wa miaka minne anavutiwa na kupaka rangi, kuna uwezekano wana kipimo cha juu cha werevu.

Utafiti unaonyesha kuwa watoto wa umri wa miaka minne wanaoweza kuchora umbo la binadamu kwa uhalisi, wanaweza kufanya vizuri katika majaribio ya vipimo vya werevu. kwani watoto hawa huenda wakawa na werevu mwingi.

Katika mradi huu wa chuo cha King’s huko London, watoto wa umri wa miaka minne walihitajika kufanya jaribio la ‘Draw-a-child’.  Kama sehemu ya hii, watoto walitakikana kuchora mtoto na matokeo yalitegemea kuwepo  na uhalisi  wa alama kama vile macho na mapua.

Kundi la utafiti lilichunguza michoro 15,000 iliyochorwa na hao watoto wa umri wa miaka minne.  Watoto waliokuwa wazuri kwenye sanaa walikuwa na nafasi bora ya kufanya vizuri kwenye majaribio ya vipimo vya werevu. Watoto waliofanya vizuri katika hili jaribio pia walikuwa na uwezo mkuu wa kiakili katika miaka nne na kumi na nne.

Daktari Rosaline Arden, mwandishi mkuu wa utafiti huu: “Jaribio la Draw-a-Child lilibuniwa mwakani 1920 ili kutathamini uwezo wa kiakili wa watoto, hivyo basi vile werevu ulivyooana katika umri wa miaka minne ulitarajiwa. Cha kustaajabisha ni kuwa waliyaona matokeo hayo mwongo mmoja baadaye.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Kucheza mpira wa kuruka ruka na mtoto wako kutamsaidia kukuza uwezo wake wa kutembea.
 • Pia, unaweza kuwauliza kutambua majina ya rangi, wanyama na vitu vingine ili kukuza uwezo wao wa kiakili.
 • Wahimize kuchora kwani katika huu umri wataanza kujifunza jinsi ya kushika penseli vizuri ambayo itawasaidia katika kuandika baadaye.

Miaka mitano: uwezo wa kudanganya

Labda wakati tu utakaofurahia kusikia mtoto wako akidanganya ni akiwa na miaka mitano.

Kudanganya uhusisha kubuni hadithi na hii yaweza kuwa jambo ngumu. Wataalam wanahisi kuwa iwapo mtoto wako ataweza kufanya hivi akiwa na miaka mitano, ataenda kuwa na kipimo cha werevu cha juu miaka ya usoni.

Utafiti uliofanyika huko Canada, watoto 1,200 waliokuwa kati ya umri wa miaka miwili na kumi na saba  uliegemea  kwa hili wazo. Kuwa watoto walioweza kudanganya utotoni mwao walipata kuwa na werevu wa kipimo cha juu.

Daktari Kang Lee, mkurugenzi katika taasisi ya Child Study katika chuo kikuu cha Toronto,alisema: “ Wazazi hawapaswi kushtuka watoto wao wanapowadanganya. Watoto wao hawatakomaa  kuwa wadanganyifu jasusi.  Karibu watoto wote hudanganya. Ni ishara kuwa wamefikia kiwango kingine cha kukomaa.  Wale walio na werevu wa juu hudanganya ili kusitiri njia zao.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Unaweza kumpeleka mtoto wako kwa mbuga na kumhimiza kubembea na kukwea.  Katika huu umri mtoto anatizamia kukuza hizi stadi za kimwili.
 • Waruhusu watoto wako kuhadithi pamoja nawe. Wanaweza kukamilisha hadithi katika huu umri. Kuwapa nafasi kuhadithiana mara kwa mara kutakuza uwezo wao wa kiakili kama vile uwezo wa kukumbuka vitu na kuwa wabunifu.
 • Pia unaweza kuwapa nafasi watoto wako kujivalisha nguo. Huu wakati watoto hujifunza kuvalia nguo wenyewe.

Watoto walio na kipimo cha juu cha werevu, miaka sita: kucheza ala za muziki

Utafiti wa chuo cha Vermont College of Medicine ulibaini kuwa kudhibiti wasiwasi na stadi za hisia kwa watoto waliocheza ala ya muziki zilikuwa nzuri ikilinganishwa wale hawakucheza.  Walichunguza ubongo  wa  watoto  232  waliokuwa  wenye afya nzuri kati  ya umri  wa  miaka sita na kumi na nane. Kucheza ala ya muziki mtoto anapokuwa na miaka sita hunawirisha stadi za mtoto za hisia.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Mpe nafasi mtoto wako kuwa huru kwani huu umri watoto hupenda kufanya mambo wao wenyewe
 • Wahimize kusakata dansi kwani katika huu umri watoto huweza kusonga kwa muziki na midundo
 • Mbali na hayo, wape muda wa kucheza ili miili yao midogo ikomae

Miaka saba: wasomaji kwa bidii

Je, wamwona mtoto wako akisoma chochote na kila kitu anachokishika. Mbali na kuongeza misamiati, kusoma pia ni ishara ya kiwango cha juu cha werevu.

Mwaka wa 2014, chuo kikuu cha Edinburgh na taasisi ya King’s huko London walifanya utafiti wa pamoja.  Waligundua kuwa watoto waliosoma vitabu vingi kwa miaka saba ya maisha yao walionyesha werevu wa juu maishani yao ya baadae.

Walifanya vizuri zaidi kwa mitihani ya vipimo vya werevu pia.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto kwa jumla  katika huu umri:

 • Wakati huu tabia ya mtoto inakua, kwa hivyo majibu ya kutia moyo inahitajika ili mtoto aweze kujistahi
 • Pia, ni muhimu kuwa mvumilivu na mfahamu iwapo mtoto wako atafadhaika ama hangaika kuhusu jukumu.
 • Himiza kuwajibika kwa kuwapa majukumu ambayo wanaweza kukamilisha.

Umri wa miaka minane: Kuchelewa Kulala

Kina mama, iwapo una wakati mgumu kumlaza mtoto wako wa miaka minane kuna uwezekano watakua kuwa watoto walio na kipimo cha juu cha werevu.

Kulingana na utafiti wa shule ya uchumi ya London, watu wazima werevu wana uwezekano wa kulala kama wamechelewa.  Unadhania  aje?  Walianza hii tabia wangali wachanga.

Watafiti waligundua kuwa: “watoto wenye werevu mwingi hukomaa kuwa watu wa usiku ambao hulala wamechelewa na kuamka wamechelewa siku za juma na zile za wikendi.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Katika huu umri, mtoto wako anaweza hisi mvuto mkubwa wa kuhusika. Huu waweza kuwa umri mzuri wa kuongea juu ya msongo wa marika.
 • Wazazi pia wanafaa kuelewa watoto wanahitaji faragha katika huu umri.
 • Wafunze watoto wako kudhibiti fedha kwa kuwapa mgao kidogo wa pesa yao ya matumizi.

Umri wa miaka tisa: Kukila kiamsha kinywa chenye afya

Watoto walio na kipimo cha juu cha werevu hupendelea kula kiamsha kinywa chenye afya.  Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Cardiff, uliohusisha watoto 5000 wa kati ya miaka tisa hadi kumi na moja ulionyesha kuwa watoto waliokula kiamsha kinywa chenye afya walifanya vizuri katika mitihani yao.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto wako kwa jumla katika huu umri:

 • Watoto walio na huu umri pia huwa na maswali mengi kuhusu mahusiano kati ya vijana na wasichana. Huu ndio wakati mwafaka wa kuzungumza nao kwa uwazi juu ya maoni yao.
 • Unaweza kuwaruhusu watoto katika huu umri kufanya uchaguzi wao. Katika huu umri watoto hudhamini huo uhuru sana kutoka kwa wazazi wao.
 • Wahimize kuwa na utaratibu katika maisha yao ya kila siku na pia kufanya mipango kwa kuweka shajara au ratiba ya kila siku.

Watoto wenye werevu mwingi zaidi, miaka kumi: ustadi wa kushiriki kwenye mazungumzo

Kutambua Watoto Wenye Kiwango Cha Juu Cha Werevu

Kids with high IQ at an older age love to have proper chats with you!

Katika umri wa miaka kumi, viashiria vya watoto wenye werevu mwingi ni kama vile kupenda mazungumzo, kubuni kanuni mpya za michezo ya bodi, kuboeka na watoto wengine.

Vidokezo vya kuboresha kukua kwa mtoto kwa jumla katika huu umri:

 • Unaweza kuwahimiza watoto wako kujiunga na vikundi ama kuwa na wakati na rafiki zao kukuza uwezo wao wa kutangamana.
 • Pia unaweza kuwapa majukumu makubwa wayafanye wao binafsi kama kusaidia kwa kazi za nyumbani.
 • Endelea kukuza mapenzi ya watoto wako ya kusoma kwa kuwatafutia uanachama kwenye maktaba.

Kwa ujumla, watoto walio na kiwango cha juu cha werevu huonyesha hulka mseto  kama vile ukumbuko mzuri na ustadi wa uchunguzi. Pia wanaweza angazia fikira zao vizuri. Ata katika umri mdogo wanaweza kuonyesha ustadi wa kitofauti katika eneo moja la ukuaji.  Wanaweza kuwa na mvuto mkubwa kwa jambo fulani ambalo wanalisoma kwa bidii.

Mfululizo wao wa mawazo unaweza kuwa mgumu ata kama umri mdogo.  Wana mseto wa mawazo ambayo wanawaza   na kuelewa vyema.  Akili zao za kuchunguza huwa inatafuta mambo mapya ama kusoma stadi mpya.  Huwa wana uwezo wa kuelewa mambo kwa haraka na pia huonyesha huu ustadi kwa kufafanua kuwa wamelewa kwa lugha iliyo rahisi ama kwa kutumia mifano.

Ni matumaini yetu kuwa utapata haya maakala ya viashiria vya kutambua watoto walio na kipimo cha juu cha werevu cha kuelimisha.  Mtoto wako anaonyesha dalili zozote zile?

 

Sources: Ministry of Education: Singapore, Psychology Today

Written by

Risper Nyakio