Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

Ndoa ni uhusiano ulio mtakatifu kwani watu wawili wanao funga ndoa wana fanya uamuzi na kuahidiana mbele ya Mungu na watu kuwa wataishi pamoja miaka na mikaka. Kwa mema na mabaya, umasikini na utajiri. Hapo awali siku za nyanya zet, uhusiano huu ulipewa kipao mbele na kuheshimika. Mtu aliye kuwa na familia haikuwa rahisi umpate akitoka nje, ili siku hizi ni rahisi kwa wamchumba wengi kutoka nje ya ndoa.

Ila siku hizi, si vigumu kupata watu walioana na wana familia wakitoka nje ya ndoa. Nyakati zimebadilika sana na vitu haziko kama zilivyo kuwa hapo awali. Ila kuna watu ambao wana enzi ndoa kama inavyo hitajika. Baada ya wachumba wao kutoka nje, walifanya juu chini kuhakikisha kuwa hawaja achana na wakaendelea na ndoa yao na kuwalea watoto wao pamoja.

kutoka nje ya ndoa

Baadhi ya wanandoa walio rudiana baada ya kesi za kutoka nje.

  1. Nameless na Wahu

David Mathenge mwimbaji mashuhuri nchini Kenya kama Nameless na bibi yake Wahu Kagwi ambaye ni mwimbaji pia wanasifika sasa kwa kuwa na ndoa sawa anayo igwa na wengi. Wana watoto wawili wanao pendeza kwa kweli, pia ndoa yao inasifika kwa kutokuwa na visanga ama kuweka habari zao zote kwenye uma. Ila, ndoa hii yao imeyapitia mengi. Miaka kadhaa iliyopita, Nameless alipatikana na kisa cha kutoka nje ya ndoa. Kisa ambacho kiliitetemesha ndoa yake na uhusiano wake na kipenzi chake kutoka siku zao za chuo kikuu. Ila, Wahu hakumwacha, walipambana na kuifufua ndoa yao. Kwa kweli ndoa nzuri ina kazi na juhudi nyingi kutoka kwa wahusika wote wawili. Hivi leo wanasifika kwa kuwa na ndoa bora zaidi kati ya watu mashuhuri nchini kote.

Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

  1. Terrence Creative na Milly Chebby

Terrence ni mwigizaji mashuhuri na kujulikana kwa jina ‘kamami’. Aliuvunja mtandao baada ya kukubali hadharani kuwa alitoka nje ya ndoa yake na mkewe na kuwa na uhusiano na msichana mwenye umri wa makamo kwa jina Anita Soina. Kitendo hiki kilimwuma sana bibi yake Milly ambaye alisema kuwa kisa hicho kilimfanya akate tama ya kuishi. Ila, Milly hakumwacha mumewe, alisimama kidete na kumpigania na kuipigania ndoa yao. Hivi sasa, wao ni wazazi wa mtoto mmoja mrembo wa kike wanaye mlea kwa pamoja. Terrence aliomba msamaha kwa bibi yake na watu wanaomfuata kwani walisikitishwa sana na kitendo hiki. Kwa sasa, walifanyia kazi matatizo yao na wana uhusiano wa kuigwa.

kutoka nje ya ndoa

Picha: Dailyupdates

  1. Jayz na Beyonce Knowles

Jina Jayz ni maarufu na hata bila ya kueleza, kila mtu anamtambua kuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani kote. Licha ya kuwa na bibi anaye tambulika na kuheshimika kama mwanamke mrembo zaidi duniani, Jayz alipatikana na kisa cha kutoka nje ya ndoa na kuwa na mchumba mwingine. Na katika harakati hizi, mtoto wa kiume alizaliwa. Licha ya haya yote, wawili hawa wali suluhisha matatizo yao na kuendelea na uhusiano wao. Kwa sasa wamebarikiwa na ni wazazi kwa watoto watatu. Kifungua mimba chao kikifuata nyayo zao na kuanza kutoa muziki kama wazazi wake.

kutoka nje ya ndoa

Beyonce na Jayz. Picha: Shutterstock

  1. David Beckham na Victoria Beckham

Mchezaji mashuhuri wa kadanda David Beckham alisemekana kuwa na uhusiano na mwanamke aliyekuwa ameajiri kazi. Baada ya kisa hiki kujulikana msichana huyo aliwacha kuwafanyia kazi. Wawili hawa bado wako pamoja na mapenzi yao kunoga.

  1. Larsa Pippen

Visa vingi vya kutoka nje katika ndoa hushuhudiwa upande wa mwanamme, ila Larsa bibiye Scott Pippen mchezaji mashuhuri wa NBA, ni miongoni mwa wanawake wanao julikana kutoka nje ya ndoa. Alisemekana kuwa na uhusiano na mwimbaji  Future. Kwa kawaida, wanaume wengi hawangerudia mabibi zao waliotoka nje ya ndoa ila Scott walisuluhisha matatizo yao na Larsa na wakarudiana. Wanaendelea kuwalea watoto wao kwa pamoja.

kutoka nje ya ndoa

Picha: Shutterstock

  1. Kevin Hart na Eniko Parish

Kevin Hart alitoka nje ya ndoa alipokuwa Las Vegas wakati ambapo bibi yake alikuwa na mimba. Baada ya vuta nikuvute nyingi, walirudiana na wakaendelea na ndoa na ulezi wao. Ndoa yao ina mengi ya kuigwa huku Kevin Hart akifanya juhudi za kuwa baba bora zaidi kwa watoto wao.

kutoka nje ya ndoa

Picha: Shutterstock

  1. Dwayne Wade na Gabriel Union

Dwayne anasemekana kutoka nje ya ndoa yake na Gabriel Union katika kipindi kigumu cha maisha ya Gab. Kufuatia kutoka nje kwake, mtoto alizaliwa huku Gab akikumbana na tatizo la kutojifungua. Wawili hawa walibarikiwa na mtoto wa kike, mwaka uliopita. Wanaonekana kuifurahia ndoa yao huku wakiposti picha zao na watoto wao kwenye mtandao mara kwa mara. Dwayne alikubali kuwa alikosea na kupotoka njia ila aliomba msamaha kwa makosa yake na wakajaribu kutatua shida zao kwani walikuwa wanapendana sana.

 

Vyanzo: Tuko news

Written by

Risper Nyakio