Covid 19: Orodha Ya Watu Wanao Kubalika Kuwa Nje Wakati Wa Kafyu

Covid 19: Orodha Ya Watu Wanao Kubalika Kuwa Nje Wakati Wa Kafyu

Huenda ukawa na maswali mengi baada ya rais ya Kenya Uhuru Kenyatta kuhutubia wananchi. Ambapo alitoa kafyu kuthibiti mwendo wa watu. Ila je, unawafahamu watu wanao kubalika kuwa nje wakati wa kafyu? Hata ingawa hakuna anaye paswa kuwa nje baada ya saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na moja asubuhi. Kuna vikundi muhimu vya watu walio pewa kibali cha kuwa nje wakati huu. Unawafahamu kweli?

Makala haya yana kusudi la kukujuza zaidi kuhusu vikundi hivi vya watu muhimu. Kwa hivyo usiwe na shaka kuhusu usalama wako wakati huu. Kwani huenda watu wengi wakaitumia fursa hii kufanya mabaya. Lakini usijali kwa kiongozi wako aliyatia haya maanani na usalama wako ni muhimu sana. Soma zaidi upate maarifa ya watu watakao kubalishwa kuwa nje ama mahali pao pa kazi katika kipindi hiki.

Covid 19: Orodha Ya Watu Wanao Kubalika Kuwa Nje Wakati Wa Kafyu

Kulingana na rais, kuthibiti mwendo huku ni muhimu sana katika kukomesha kusambaa kwa virusi vya homa ya korona. Ni jukumu la mwananchi wa kawaida asiye kuwa kwa orodha hii kufuata maagizo ya serikali ili tupunguze kusambaa kwa virusi hivi.

 

Orodha ya watu wanao kubalika kuwa nje wakati wa kafyu

Orodha ya watu walio na kibali cha kuwa nje hata baada ya masaa ya kafyu kuanza

 1. Wataalum wa matibabu na wafanyakazi wa afya

watu wanao kubalika kuwa nje wakati wa kafyu

 1. Maafisa wa usalama wa kitaifa, utawala na uratibu
 2. Afya ya umma na maafisa wa mitakasio ya vileo kwenye serikali ya kata.
 3. Maduka ya dawa yaliyo na kibali ama liseni
 4. Watangazaji walio na kibali na vyumba vya habari
 5. Kampuni ya Kenya ya umeme na sitima
 6. Wanao uza chakula, kupelekea wengine vyakula, maduka ya vyakula na waafirishaji wa bidhaa za shambani.

Covid 19: Orodha Ya Watu Wanao Kubalika Kuwa Nje Wakati Wa Kafyu

 1. Supermarkets, mini-markets na hypermarkets zilizo na kibali
 2. Wauza petroli na mafuta ikawa ni kwa idadi kubwa ama ndogo
 3. Wanao husika na mawasiliano ya simu za mkono ama rununu na wana vibali na wanao toa huduma hizi
 4. Benki zilizo na liseni na taasisi za kifedha na huduma za kulipana
 5. Wazima moto na huduma zingine zinazo hitaji mwitiko wa dharura
 6. Mashirika ya usalama yaliyo na vibali

Written by

Risper Nyakio