Baadhi ya mambo unayo weza kujihusisha nayo ukiwa na wazazi wa Kenya

Baadhi ya mambo unayo weza kujihusisha nayo ukiwa na wazazi wa Kenya

Wazazi wa Kenya ni baadhi ya wazazi wanao kuwa makini zaidi na ulezi bora. Kuna baadhi ya mambo ambayo haya kubaliki kamwe. Kama vile kuingia nyumbani usiku ama kuto soma kwa bidii.

Mambo Unayo Weza Kujihusisha Nayo Ukiwa na Wazazi Wa Kenya 

Wazazi  ni watu wa maana maishani mwetu. Kama umebarikiwa kuwa na mzazi mmoja ama wote wawili, shukuru Maulana. Kwa wale waliowapoteza wazazi wao, pokea rambi rambi. Unaweza kuongea na kuomba ushauri kutoka kwa mzazi wako ama mlinzi wako unapotatizika maishani. Wanakupa moyo unapo patana na matatizo maishani.

Juma alizaliwa nchini Kenya na kulelewa mji wa Mombasa. Alipofika umri wa miaka 10, darasa la tano, alianza kumea pembe na kuwa mgumu. Alianza kukosa kwenda shule siku zote. Punde tu wazazi wake walipo enda kazini, alirudi kitandani na kuendelea kulala. Jambo hili liliendelea kwa muda hadi walimu wake walipo anza kushangaza kinacho endelea. Alikua ameanza kufeli mtihani na hapo awali alikuwa analiongoza darasa lake. Walimu walimpigia mamake rununu na kumwuliza kinacho endelea kwani mtoto wake haendi shuleni. Mamake Juma alipigwa na butwaa kwani wakati huu wote alidhani mwanawe anajiunga na darasa kama wanafunzi wengine. Alimpigia Bwanake simu na kumjulisha lililo kuwa likiendelea. Walimwadhibu Juma aliye waeleza kuwa alikua anakosa kwenda darasani ili aende bichi. Siku iliyo fuata, alirudishwa shuleni na wazazi wake na kuadhibiwa na walimu kwa kukosa kuenda shuleni.

Tutayaangazia baadhi ya mambo ambayo unaweza kujihusisha nayo ukiwa na wazazi wa Kenya

Baadhi ya mambo unayo weza kujihusisha nayo ukiwa na wazazi wa Kenya

Masomo ni muhimu

Ukiwa na wazazi wa Kenya, hakuna kujadili kuhusu umuhimu wa masomo. Unapaswa kwenda shuleni na kujitahidi. Ukiwa mchanga, kuna uwezekano hautapenda shule sana na utahitaji msukumo kutoka kwa mzazi ili uende shuleni. Katika nchi zingine, una pewa mawaidha ya umuhimu wa kusoma. Ila nchini Kenya, unachapwa viboko ili uone umuhimu wa kusoma. Unapelekwa shuleni kwa lazima. Wanaamini kuwa bila masomo hauna maisha mema. Pia wazazi wengine hawakufika kiwango cha juu cha masomo, kwa hivyo wana kuadhibu ili uende shuleni na ujitahidi upate kiwango cha juu cha masomo.

Kuingia kwa nyumba kabla ya saa moja usiku

Maadili ni jambo ambalo wazazi wengi wa Kenya wanafuatilia. Wana imani kuwa ifikapo saa moja jioni, unapaswa kuwa kwa nyumba. Kuwa nje wasaa huu ni ishara kuwa umekomaa na umeanza kupotoka ki maadili. Pia wana amini kuwa unaji husisha na mambo mabaya. Wakati wa hapo zamani, ungefika kwa nyumba usiku ukiwa msichana, ungefukuzwa ama kuadhibiwa. Pia wazazi wangekupeleka kwa babu na nyanya yako ili upewe ushauri.

Kuwatii wazazi wako

Unapo tumwa, wazazi wana tarajia utaenda uliko ambiwa uende. Hata kama ulikuwa na jambo lingine ulikuwa unafanya, wanatarajia utaacha uliyo kuwa uki yafanya na ufuate maagizo yako. Kukawia sana kabla ya kufanya ulicho ambiwa ni ishara kuwa umeanza kumea pembe na hufuati wazazi wako.

Kuamka mapema kufanya kazi za nyumba

Wazazi wa Kenya wanapenda kutumia maneno ya kejeli unapo lala sana. Kama vile “kiongozi ame amka”. Hii ni kukukejeli kama njia ya kuonyesha ulicho fanya si sawa. Una stahili kuamka mapema, kutayarisha kiamsha kinywa ama kusaidia kufanya kazi zingine za nyumba. Kama vile kuosha nyumba, kuosha vyombo, kupika chai na kadhalika. Kuamka ukiwa umechelewa haikubaliki.

Kujitahidi maishani

Jitahada ni muhimu maishani, ukiwa na wazazi wa Kenya, unajua kuwa jambo lingine la kufanya ila kutia bidii katika mambo unayo yafanya. Wana sisitiza jambo hili kutoka umri mchanga. Wanakupea kazi za nyumba unazo faa kumaliza kwa muda walio kwambia. Pia unakua ukijua kuwa usipo jitahidi na kufanya kazi, hautapata lishe. Jambo hili lina kufanya kutia bidii ile upate chakula siku hiyo. Kukuwa na maadili haya wanasaidia kutoa uzembe maishani. Unajua kuwa hakuna mtu atakaye kuokoa maishani mbali ni bidii yako itakayo kupa maisha bora na kukusaidia kupata vitu vyote unavyo vitamani maishani.

Ukarimu 

Kutoka ukiwa na umri mdogo, unafunzwa kugawa vitu ulivyo navyo na marafiki na watoto wengine walioko karibu nawe. Vitu kama chakula, peremende. Ni vibaya mzazi akikuona ukikula peremende peke yako na aliye karibu nawe hana. Wana weza kuadhibu kwani huko ni kujipenda na kuto jali masilahi ya mwenzako. Unapaswa kuwapenda walio karibu yako na kuwagawai vitu ulivyo navyo. Hii imesaidia kusisitiza umuhimu wa kuwapenda jirani, kuwajalia mema na kuwatunza. 

Hayo ni baadhi ya mambo unayo weza kuelewa ukiwa mtoto wa mzazi wa Kenya. Ni maadili haya yanayo wasaidia watoto wao kuwa bora kwa jamii.

 

Read Also: Hospitality 10 bora za kujifungua nchini kenya

Written by

Risper Nyakio