Wiki 12 Ya Ujauzito: Mwongozo Wa Ujauzito Wa Wiki Baada Ya Wiki

Wiki 12 Ya Ujauzito: Mwongozo Wa Ujauzito Wa Wiki Baada Ya Wiki

There are so many exciting things your little one can do now, one of them being able to curl his teeny fingers and toes. Plus, its time to go maternity clothes shopping, thanks to your growing bump.

Karibu kwa wiki ya mwisho ya trimesta yako ya kwanza! Utafurahikia kujua kuwa baada ya wiki 12 ya ujauzito, nafasi za kuharibika kwa ujauzito ama mimba yako hupungua kwa kiasi kikubwa! Na iwapo unatarajia mapacha, tumbo lako litakua likionyesha.

wiki-12-ya-ujauzito

Mtoto wako ni mkubwa kiasi gani katika wiki ya 12?

Katika wiki ya 12, mtoto wako ni mkubwa kiasi cha rambutan Ana urefu wa sentimita 5.3 na uzito wa gramu 13.8.

wiki-12-ya-ujauzito

Image courtesy: Pixabay

Ukuaji Wa Mtoto Wako

Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, utagundua kuwa:

 • Mtoto anajitayarisha kwa hatua ingine ya ukuaji wa kasi wa viuongo na tishu zake.
 • Katika wiki 12, anaanza kukuza uwezo wa kuitikia mguso. Kwa sasa, mikono yake na miguu midogo ina mwendo. Ambayo inakaa kana kwamba anapunga mtoto unapoenda kukaguliwa ukuaji wake kwenye mashine.
 • Anaikunja mikono yake na miguu yake na hata kufunga na kufungua mikono yake.
 • Uwezo wake wa kuonja pia unaimarika.
 • Vidole vyake vya mikono na miguu vinaanza kukua.

wiki-12-ya-ujauzito

 Dalili Za Ujauzito
 • Homoni huifanya ngozi yako ikawa na upele ama kujikuna, na kukufanya usiwe na usalama. Usitie shaka, kuna dawa kama vile calamine ya kujipaka itakayo kusaidia. Iwapo ni kesi nyingi, pata ushauri kutoka kwa mtaalum wako wa afya ya wanawake.
 • Mask ya ujauzito inayojulikana kama chloasma ama melasma huenda ikakutia shaka.
 • Misuli yako ya tumbo haiko hai vile na kukufanya uwe na kinya kigumu na kuitoa hewa mbaya zaidi. Kunywa maji mengi zaidi na ule matunda mengi kuhimiza mwenendo wa boweli na kuepuka kufunga choo.
 • Shukrani kwa tumbo lako linalo mea, tumbo yako huenda ikakaa imepanuka kiasi na huenda baadhi ya nguo zao zikaanza kukufinya kwenye kiuno. Pumua kwa urahisi kwa kuvalia nguo zinazo kustarabisha.
 • Kwa sasa, habari njema katika wiki hii ya mwongozo wetu: huenda ukaanza kung’aa na hili ni jambo njema! Ng’ara mama na uufurahikie wiki 12 ya ujauzito wako!
Utunzaji wa mimba
 • Iwapo u-miongoni mwa wachache wenye hamu ndogo ya chakula, kwa kweli una bahati! Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, jua kuwa kuongezeka kwa uzito katika wiki ya kwanza unapaswa kuwa kwa upole. Ila, iwapo unakula chakula kingi, kuwa makini na uzingatie ongezeko la uzito kutoka kwa mtaalum wako wa afya ya wanawake.
 • Kama umekuwa ukiipoteza hamu yako ya kula na kuhisi uchovu mara nyingi, ni kawaida kupoteza ama kuongeza kilo kwa kiasi kidogo. Katika mwisho wa trimesta yako ya kwanza, punde tu ishara hizi zinapo pungua, uko katika safari ya kufurahikia ujauzito wako.
 • Tumbo lako la mama/ uterasi yako inapo endelea kupanuka, kwa mara huenda ukaishi kuumwa na tumbo kiasi kunapo kuwa na mwendo kama vile kukohoa ama kulala ama kukaa kwa namna tofauti. Kuumwa na misuli ni kawaida ila uchungu huu unapo ongezeka, na kuwa mwingi, usiupuuze.

Orodha muhimu ya kuzingatia

 • Katika hatua hii, kuna uwezekano kuwa matiti yako yamekuwa makubwa zaidi. Ni wakati wa kununua ngup mpya za kuzisitiri.
 • Iwapo umekuwa ukivalia mifuto ama vinyasa mara nyingi, ni wakati dhabiti wa kununua nguo za ujauzito zitakazo kuwa njema katika wakati huu. Hakikisha kuwa una starehe unapo valia nguo ili kukuwezesha kufanya kazi zako ama kukaa kwa urahisi.
 • Huenda ukaanza safari ya kutafuta mfanya kazi wa kukuchungia mtoto na kusaidia na kazi za kinyumbani ili kukurahishia kazi hii wakati unapo fika.

Wiki yako ijayo: 13 weeks pregnant

Wiki yako iliyopita: 11 weeks pregnant

Je, una maswali yoyote kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Mama, shaka zako ni zipi wakati huu? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Republish with permission from theAsianparent

Written by

Risper Nyakio