Wiki 32 Ya Ujauzito: Mwongozo Wa Ujauzito Wa Wiki Baada Ya Wiki

Huenda mwendo wa mtoto wako ukawa umepunguka zaidi katika wiki hii na ana mfumo wa kulala kati ya dakika 20 hadi 40. Huu ni wakati bora zaidi kwako mama kuanza kujua dalili za uchungu wa uzazi na kupanga sherehe ya kumkaribisha mtoto.
Kwa sasa kwani uko katika wiki ya 32 ya ujazito wako, kuna maana kuwa ngozi ya mtoto wako inaonekana vyema. Tumbo lako pia linapanuka kadri siku zinavyo endelea kupita, ila, ni ishara ya mtoto wako anayekua. Yeeeeei!
Mtoto wako ni mkubwa kiasi gani katika wiki 32 ya ujauzito?
Mtoto wako ni mkubwa kiasi cha tikiti ya mawe katika wiki hii, ana uzito wa kilogramu 1.8 na urefu wa sentimita 29. Mtoto wako amekuwa mnene, shukrani kwa ufuta ulio mwilini wako.

Image courtesy: Pixabay
Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, utagundua kuwa:
- Mtoto wako kwa sasa anameza, kupumua, kurusha mateke na kunyonya.
- Mfumo wa utumbo wake umekua unavyo hitajika.
- Ngozi yake inaanza kuonekana vyema.
- Siku hizi analala vyema, na mfumo wa kulala wa dakika 20 hadi 40. Huku pia kunaeleza kupunguka kwa mwendo unaoshuhudia siku hizi.
- Katika wiki 32 ya ujauzito, tumbo lako lililo fura linaendelea kuhusi kujikuna kadri ngozi yako inavyo endelea kunyooka na kukauka.
- Huenda ukahisi uchungu kwenye shavu la mguu na uchungu huenda ukaongezeka wakati wa usiku.
- Uterasi yako inayo endelea kukua inauma na huenda ukahisi ulegevu.
- Matiti yako yanavyo endelea kukua katika trimesta ya tatu, huenda chuchu zikaanza kutoa maziwa ya kwanza, ambayo hufuatwa na maziwa ya mama.
- Kuwa na mazoezi mara kwa mara (kitu chochote ambacho kinakusaidia kama kutembea ama kufanya yoga) na unywe vinywaji vingi.
- Beba protini ama wanga kwenye mkoba wako ule unapohisi kizunguzungu.
- Jaribu calamine ama mafuta ya kuzuia kujikuna kukumbana na kuhisi kujikuna wakati wote.
- Jaribu usijikwaze kuhusu alama za kunyooka mwilini mwako. Asilimia hadi 90 za wanawake hupata alama hizi. Ni ishara kuwa mtoto wako anakua na kurembeka ipasavyo.
- Kuwa tayari; soma kuhusu ishara za uchungu wa uzazi: kupasuka kwa maji, kuumwa na tumbo, kutoa damu kwenye uke, kuharisha na kupata mkazo kwenye uterasi.
- Ni wakati wa kuwa na sherehe ya kutayarisha kumpokea mtoto wako.
Wiki yako ijayo: 33 weeks pregnant
Wiki yako iliyopita: 31 weeks pregnant
Je, una maswali kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wiki baada ya wiki? Shaka zako ni zipi kwa sasa mama? Tujulishe kwa kutuwachia ujumbe mfupi!
Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent