Katika wiki 34 ya ujauzito, uko karibu sana kumsalimia mtoto wako. Ila, ngoja, wakati bado! Mtoto wako bado anajitayarisha kuingia duniani. Mfumo wake wa neva bado unakua na vidole vyake vidogo vya mikono na miguu na kucha zina endelea kukua. Soma kuhusu mambo unayo tarajia katika wiki hii.

Mtoto wako ni mkubwa kiasi gani katika wiki 34 ya ujauzito
Mtoto wako mdogo anatoshana saizi ya cantaloupe na urefu wa sentimita 31 na uzito wa kilo 2.28. Siku yako ya kujifungua inakaribia kadri siku zinavyo zidi kupita. Tuna uhakika kuwa u
Image courtesy: Pixabay
Ukuaji wa mtoto wako
Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, utagundua kwamba:
- Mtoto wako anapata ufuta zaidi wa kumsaidia kuwa na joto wakati wote.
- Mfumo wake wa neva unaendelea kukua kwa kasi wakati huu.
- Kucha za miguu na mikono yake imekua.
- Iwapo unatarajia mtoto wa kiume, katika wiki hii, sehemu zake za kiume zinashuka.

Dalili za Ujauzito
- Uchovu utakuzidia! Utajipata umechoka zaidi kuliko hapo awali kwa sababu ya mkazo unao shuhudia.
- Katika wiki 34 ya ujauzito, utashuhudia uchafu mwingi kutoka kwa uke wako- shukrani kwa homoni.
- Shinikizo la chini la damu huenda likafanya uhisi kizungu zungu.
- Huenda ukakatizika kuona. Bila shaka, ni kwa muda tu katika wiki ya 34 ya ujauzito.
- Hakuna tiba ya kuenda bafuni mara kwa mara.
- Kadri tumbo yako inavyo zidi kukua, ndivyo mafua yako yanashindwa kupanuka zaidi na huenda ukashuhudia kupunguka kwa hewa mwilini.
- Kuumwa na miguu huwa kawaida katika hatua hii, wakati ambapo uzito wa ujauzito, kuvimba na kuhisi uchovu huwa mwingi zaidi.
Utunzaji wa ujauzito
- Pumzika kadri uwezavyo. Unaweza jihusisha katika shughuli ambazo zitakufurahisha.
- Weka ratiba yako ya kufanya mazoezi ikiwa nyepesi uwezavyo
- Kunywa maji mengi mapema siku inapo anza kuepuka kuhisi kiu usiku. Epukana na vinywaji hivi.
Orodha muhimu ya kuzingatia
- Hakikisha kuwa mkoba wako wa hospitali umepangwa ifaavyo.
- Iwapo unapanga kula placenta yako, jisajilishe kwa encapsulation wiki hii.
Wiki yako ijayo: 35 weeks pregnant
Wiki yako iliyopita: 33 weeks pregnant
Je, huenda ukawa na maswali kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Shaka zako ni zipi mama katika wiki hii? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa!
Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent