Wiki 43 Ya Ujauzito: Mwongozo Wako Wa Ujauzito Wiki Baada Ya Wiki

Wiki 43 Ya Ujauzito: Mwongozo Wako Wa Ujauzito Wiki Baada Ya Wiki

Wakati ambapo mtoto wako anazaliwa huku amechelewa, huenda hautashuhudia kujifungua kwa asili.

Tunafahamu kuwa tumelinganisha na matunda hadi sasa, ila kwa sababu tuko katika wiki ya 43 ya ujauzito, tusiende hapo kwa sasa. Iwapo unasoma makala haya, kuna uwezekano mkubwa kuwa unajiuliza wakati ambapo mtoto huyu atafika. Mtoto wako huenda akawa amestareheka ya kutosha tumboni, penda ama usipende, amekawia sana kufika.

Wakati huu, mtaalum wako wa afya ya uzazi, huenda akaanza kuongea nawe kuhusu upasuaji wa C-section ama njia zingine za kuanzisha uchungu wa uzazi ili kuanza kumkaribisha mwanao.

Wiki 43 Ya Ujauzito: Ukuaji wa Mtoto Wako

pregnancy weekly guide

Katika mwongozo huu wa ujauzito, utagundua kwamba:

  • Hata kama mtoto wako hataki kufika bado, haimaanishi kuwa uwache kuhesabu mateke ya kiinitete chako ili kuwa na uhakika. Huenda kukawa hakuna nafasi tosha iliyo baki kumkubalisha kusonga. Ila katika wakati fulani, mtoto wako ambaye si mdogo sana atasonga mwilini ili awe na starehe.
  • Kuwa tumboni kwa wakati mrefu kuna maana kuwa mtoto wako anazidi kuongeza kilo, na kuna maana kuwa utajifungua mtoto mkubwa. Baada ya haya yote kufanyiwa upasuaji wa C-section hakuonekani kama fikira mbaya.
  • Shaka kubwa sana zaidi kujifungua baada ya wakati kutimia ni kazi ya placenta kupunguka na idadi ya amniotic fluid kupunguka pia. Kama matokeo ya haya, kuna hewa idadi ndogo na virutubisho vinavyo mfikia mtoto wako. Kuna hatari ya kitovu kufinywa na kuhatadharisha maisha ya mtoto wako.

Dalili Za Ujauzito

pregnancy week 43

Picha shukrani kwa: Pixabay

  • Hadi wakati ambapo utamshika mtoto wako mikononi mwako, utakuwa unapita kila mahali na mtoto wako anayetoshana tikiti tumboni mwako. Kiungulia, kuenda msalani mara kwa mara, uchungu wa pelviki, kuumwa na mgongo ama maji kubaki mwilini –  bado kutakuwepo.
  • Kujaribu kupata usingizi mwanana huenda kukawa tatizo kubwa wakati huu, kwa sababu kwa wakati huu umekuwa mkubwa sana na kwa sababu unakaza sehemu ya mgongo wako wa chini. Ila, jaribu kadri uwezavyo kupumzika sasa. Utauhitaji mtoto wako anapo fika.

Utunzaji wa ujauzito

  • Angalia kwa makini kuwa umeweka vitu unavyo hitaji kwenye begi lako la hospitali na kwa wakati huu huenda daktari wako akawa ameratibisha tarehe ya upasuaji wa C-section ama tarehe ya kuanzisha uchungu wa uzazi. Kati ya haya, unaweza jaribu njia asili za kuanzisha uchungu wa uzazi.
  • Kwa wamama wanao tumainia kujifungua kwa njia asili kupitia uke wao, usitie shaka kuhusu jambo hili. Baadhi ya mambo huwezi thibiti, ila kuwa makini kwa kujingua salama. Iwapo una maswali ama shaka, unaweza wasiliana na daktari wako.

Wiki 43 Ya Ujauzito: Mwongozo Wako Wa Ujauzito Wiki Baada Ya Wiki

Orodha muhimu ya kufuata

  • Kuangalia kwa mara ya mwisho mkoba wako wa kujifungua katika wiki mwongozo wa wiki 43 ya ujauzito!! Uko tayari kumwona mtoto wako wakati wowote kutoka sasa!

Jaribu kuto kuwa na uwoga mwingi haijalishi ulicho kisoma katika mwongozo wa ujauzito wiki ya 43. Siku yako ya kujifungua (EDD) ina karibia kwa sasa. Hata kama huenda ukawa na uwezo wa kujifungua kupitia kwa uke wako kama ulivyo panga, endelea kuhesabu mateke ya kiini tete chako. Daktari wako atakusaidia na kukuongoza kwa hivyo, kuwa na matumaini na maoni chanya!

Kumbukumbu: Mayo Clinic

Wiki iliyo pita: 42 weeks pregnant

Je, una maswali kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Mama, shaka zako ni zipi katika wakati huu? Tujulishe kwa kutuwachia ujumbe mfupi hapa chini!

Written by

Risper Nyakio