Mwongozo Wa Wiki Ya 33 Ya Ujauzito: Yote Unayo Paswa Kujua

Mwongozo Wa Wiki Ya 33 Ya Ujauzito: Yote Unayo Paswa Kujua

Mtoto anapo zidi kukua, shinikizo huibuka kwenye neva ya sciatic ambayo ndiyo neva kubwa zaidi mwilini. Na huenda maumivu kwenye mgongo yaka ibuka.

Uko katika trimesta yako ya tatu, na katika kipindi hiki, nafasi kubwa ni kuwa tayari umeanza kufikiria jinsi maisha yako yatakavyo kuwa na mtoto wako. Na huenda athari za mimba zikawa zimeanza kuingia. Uta gundua kuwa mabadiliko mengi yametendeka, na hata kuanza kuhisi uchungu katika sehemu tofauti za mwili. Katika wiki ya 33 ya ujauzito, mwanamke anapaswa kufahamu kuhusu ishara za uchungu wa uzazi wa mapema na wakati anapo paswa kuwasiliana na daktari wake.

Ishara za wiki ya 33 ya ujauzito

wiki 33 ya ujauzito

Huenda ukawa unashuhudia mabadiliko kwenye mtima wako japo ujauzito wako unavyo zidi kukua. Ishara zingine ambazo ni dhabiti katika wiki ya 33 ya safari yako ya ujauzito ni kama vile:

  • Kuumwa na mgongo
  • Matatizo ya kulala
  • Kushuhudia kiungulia mara kwa mara
  • Kupungukiwa na hewa hasa unapo tembea ama kufanya kazi nyepesi
  • Kuanza kusikia mtoto akirusha mateke
  • Kufura kwenye miguu

Kufura miguu

Huenda ukashuhudia kuwa miguu imeanza kufura zaidi ikilinganishwa na miezi ya hapo awali. Hii ni kwa sababu uterasi inayo zidi kukua kila uchao ina shinikiza mishipa inayo peleka damu kwenye miguu yako. Ikiwa una tatizika na kufura kwenye miguu, hakikisha kuwa unapo kaa, unaiwekelea juu ya kiti ili kupunguza shinikizo hilo. Enda upewe masi angalau mara mbili kwa wiki.

Ikiwa kufura kuna zidi, huenda ikawa ni ishara ya preeclampsia na ni vyema kuwasiliana na daktari wako bila kusita.

Kuumwa na mgongo

Mtoto anapo zidi kukua, shinikizo huibuka kwenye neva ya sciatic ambayo ndiyo neva kubwa zaidi mwilini. Na huenda maumivu kwenye mgongo yaka ibuka. Ili kupunguza kuumwa na mgongo, unaweza jaribu mambo haya:

  • Kubadili pande unapo lala ili kupunguza uchungu
  • Kukoga kwa maji moto ili kutuliza mwili
  • Kutumia pedi ya joto kupunguza uchungu kwenye mgongo

Mama mjamzito ana shauriwa kufanya mazoezi mepesi kwani yana saidia kupunguza uchungu kwenye mgongo.

wiki 33 ya ujauzito

Hitimisho

Huku wiki saba zikiwa zimesalia hadi utakapo patana na mwanao, ni vyema mama kufahamu ishara zinazo ashiria kuwa ako karibu kujifungua. Katika wakati huu, mtoto wako ana inchi 15-17 na uzito wa kilo 2-2.3. Na atazidi kukua hadi utakapo jifungua.

Hakikisha kuwa una enda kuogelea, kufanya mazoezi mepesi na kutembea ili kupunguza uchungu mwilini. Kunywa maji tosha kila siku, ili mwili wako usipungukiwe na maji.

Usikome kwenda kwenye zahanati kuangaliwa jinsi hali yako ilivyo. Ukihisi kuwa huenda ukawa na uchungu wa mama usio komaa, usi site kuwasiliana na daktari wako.

Soma Pia:Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio