Punde tu unapofika wiki yako ya kumi ya ujauzito, utagundua kuwa kuna badiliko mwafaka yanayo tendeka katika kiinitete chako. Mwili wake utaanza kubadilika na kukua kwa kasi.

Mtoto wako ni mkubwa kiasi gani
Katika wiki kumi ya ujauzito, mtoto wako anatoshana chaza. Ana kipimo cha sentimita 3.1 na gramu 3.9.Katika wiki kumi ya ujauzito, mtoto wako anatoshana chaza. Ana kipimo cha sentimita 3.1 na gramu 3.9.
Image courtesy: Pixabay
Ukuaji wa mtoto wako
Katika mwelekezo huu wa kila wiki ya ujauzito, utajifunza kwamba:
- Akili ya mtoto wako inakua kwa kipimo cha hali ya juu: karibu niuroni 250000 zinatengenezwa kila dakika.
- Sehemu zake zote muhimu kama figo, matumbo, akili na maini, zimeanza kufanya kazi.
- Vidole vyake vya miguu na mikono vinaanza kuachana na kucha zinaanza kutokea.
- Mifupa ya mtoto wako inaanza kupata nguvu na kupata umbo.
- Mtoto wako ameanza kupata viungo vya meno katika wiki ya kumi ya ujazito.
- Mwili wa mtoto wako wa kiume imeanza kutengeneza testeroni.

Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi
- Hisia mbaya ya kichefuchefu haiishi katika wiki hii ya kumi.
- Unahisi kwamba una hewa nyingi sana ndani yako, hewa hiyo inatoka kwa njia ya kuaibisha kama kushuzi.
Utunzaji wa ujauzito
- Ili kumaliza hisia ya kichefuchefu, jaribu chakula tofauti tofauti na uweze kuona ni nini ambacho kinasaidia kwa kupunguza hisia hii. Kina mama wengine wanapenda biskiti za chumvi au chai ya tangawizi ili kuwasaidia mchana na usiku. Tembelea daktari wako na upate ushauri kuhusu vitamini B6 na B12 ambayo inasaidia kupunguza hisia ya kichefuchefu. Pata chakula ambacho kina mama wanakula katika wiki ya kumi ya ujauzito.
- Jitahadhari na chakula ambacho hakijaiva kama vile mboga, nyama na mayai, hauwezi taka kushikwa na shida ya tumbo ukiwa mjamzito kwa sababu inaweza kuletea shida ya kuumwa na tumbo ambayo inaweza adhiri kitoto chako.
- Ukiona dalili za kutoa damu kwa kiasi kidogo au kutoa uchafu usio wa kawaida, pata ushauri wa daktari wako. Katika wiki za kwanza kwanza za ujauzito, kiinitete hakina nguvu kwa hivyo kipindi hiki cha ujauzito mtoto wako ako katika muda ambao anaweza kukabiliwa na hatari sana.
- Usibebe vitu mzito. Kama unahitaji kubeba vitu hivi mzito, tafuta usaidizi badala ya kuhatarisha mtoto wako katika ujauzito.
Orodha muhimu ya kuzingatia
- Kula chakula bora kama vile mboga (fotale), matunda (vitamin na fiba) na maziwa (kalsiamu) ili kuuweka mwili wako katika hali ya afya njema.
- Tembea kidogo ilikusaidia katika uenezaji wa damu katika mwili wako.Pia hewa safi unayoipata inaweza saidia kubadilisha mhemko wako. Tembelea ufukoni wa ziwa au kwenye mbuga ili uweze kupa akili yako utulivu huo.
- Angalia misa za wajawajito, ili uweze kupata utulivu ufaao katika kipindi chako cha pili cha ujauzito.Kuwa na ujuzi kwamba kampuni nyingi zitakuwa na mazoezi haya kutoka wiki ya kumi na tatu (kuanza kwa kipindi cha pili cha ujauzito)na wiki thelathini na mbili (kabla ya kuanza kwa mwezi wa tisa).
Wiki yako ijayo: 11 weeks pregnant
Wiki yako iliyopita: 9 weeks pregnant
Je, una maswali yoyote kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Mama, shaka zako ni zipi wakati huu? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!