Wiki ya nane ya ujauzito: Mwongozo wa ujauzito wa wiki baada ya wiki

Wiki ya nane ya ujauzito: Mwongozo wa ujauzito wa wiki baada ya wiki

Your baby can start saying goodbye to that primitive tail and hello to primitive neural pathways! As for you, your sense of smell is heightened and you may be feeling fatigue and nauseated. Don't worry, though, as it will get better!

Uchovu, uvimbe wa matiti na kuongezeka kwa hisia za harufu na mabadiliko mengine mengi, zinazokaribishwa na zisizohitajika, zinafanyika mwilini mwetu katika wiki ya nane ya ujauzito. Unaweza kosa kuskia, lakini mtoto wako pia anapitia mabadiliko pia.

wiki ya nane ya ujauzito

Mtoto wako ni mkubwa kiasi gani

Katika wiki hii, mtoto wako ambaye kwa sasa hivi yuko katika wiki yake ya mwisho ni kiinitete, anakua kutoka sentimita 1.6-sentimita 2.2, kwa kuongeza kilo kutoka kutoka gramu 1.6-1.8 .Hiki ni kipimo cha Bengal currant ambayo kwa jina ya kisayansi ni Carissa carandas.

wiki ya nane ya ujauzito

Image from Wikimedia Commons

Ukuaji wa mtoto wako

Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, unajifunza mambo haya:

 • Hata ingawa bado haujahisi mtoto wako akisonga, bado yuko uhai na anaweza kutekeleza mambo mengi sana kama vile kuhamisha mikono.
 • sifa za usoni zinaendelea kukua pia mikono, midomo na ncha ya mapua yanaonekana.
 • Vidole vya mikono na miguu vinajitokeza kama vimeshikana.
 • Hata kama bado yu mdogo, mtoto wako anaanza kupata viungo vya kuonja ladha.
 • Kiungo cha nyuma cha mtoto wako kilichokaribia kufanana na mkia wa kiluwiluwi kinaanza kupotea katika wiki ya nane ya ujauzito.
Dalili za ujauzito
 • Homoni zilizoko mwilini mwako huenda zinaongezeka kufuatia uwezo wako wa kunusa. Huenda unapata kwamba harufu fulani zinakufanya usihisi vyema.
 • Iwapo baadhi ya sehemu za mwili wako hazina ishara za ujauzito, matiti yako bila shaka yana ishara! Yameongezeka na pia yakawa mazito zaidi kwani mishipa ya kutoa maziwa imeanza kupanuka.
 • Huenda unahisi kuchoka na kichefuchefu.
 • Unaanza kuhisi uchungu wa mapema wa ujauzito. Kwani mishipa yako ya tumbo inaanza kunyooka kwa sababu tumbo lako la uzazi linapanuka.
 • Unashuhudia matatizo ya tumbo. Jambo hili ni la kawaida na usiwe na shaka kuhusu kufunga choo ama kufura tumbo ama hata matatizo ya kiungulia. Ila, jitunze. Iwapo yanakusumbua, pata ushauri wa daktari.
 • Kitu kingine kinacho tendeka ni kuwa, idadi ya damu inayo zunguka mwilini inaongezeka. Katika mwisho wa safari yako ya ujauzito, huenda ukawa na lita moja na nusu zaidi ya damu mwilini mwako.
Utunzaji wa ujauzito

Hata kama hamu ya kula imepungua, unapaswa kula chakula bora. Mtoto akikua katika kipimo hiki, nyinyi wote wawili mnahitaji virutubisho vingi.

Jambo la muhimu katika mwelekezo huu wa wiki kwa wiki wa ujauzito ni kupata kalsiamu ya kutosha na pia ukumbuke kula vitamin D.

Orodha muhimu ya kuzingatia
 • Anza kwa kutafuta utunzaji wa mtoto mapema kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo yanafaa kukamilishwa kabla ya kujifungua.
 • Huu sio muda unafao wa kufanya mazoezi ya Yoga au kuanza kumeza dawa. Kumbuka ni muhimu kupumzika bila wasiwasi wowote.
 • Utahitaji kuahirisha mipango ya kusafiri kwa sababu ya uchovu na kichefuchefu, kuna mambo ambayo unaweza fanya ili kujiburudisha kama kupangia mtoto wako kabla ya kujifungua.

Wiki yako ijayo: 9 weeks pregnant

Wiki yako iliyopita: 7 weeks pregnant

Je, una maswali yoyote kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Tazama mtandao wetu wa kijamii wa familia yetu ya Africa parent.  Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Written by

Risper Nyakio