Wiki ya tisa ya ujauzito: Mwongozo wa kila wiki wa ujauzito

Wiki ya tisa ya ujauzito: Mwongozo wa kila wiki wa ujauzito

Your baby can now make tiny movements, thanks to the equally tiny muscles on his/her hands and feet. As for you, loss of appetite may lead to weight loss, though you may need loose-fitting clothes thanks to your ever-expanding belly.

Mtoto wako katika kipindi hiki ni kiinitete, lakini ni mapema sana kuhisi akisonga. Jua kwamba mtoto wako yuko hai ndani ya tumbo yako. Kwa muda huu mama naye anapigana na ugonjwa wa asubuhi na mhemko mbaya. Soma zaidi ili kujua kuhusu mabadiliko na ukuaji unaoendelea kati yako na mtoto wako katika wiki hii ya tisa a ujauzito.

week 9

Mtoto wako ana kipimo kipi?

Mtoto wako anatoshana tunda la Longan kwa kipimo cha sentimita 2.3 hadi 3 kwa urefu na uzito wa gramu 1.9 hadi 3.5.

wiki ya tisa ya ujauzito

Ukuaji wa mtoto wako katika wiki ya tisa ya ujauzito

Katika mwongozo wa ujauzito wa kila wiki, utafahamu kwamba:

 • Mtoto wako amekua kutoka kuwa kiinitete na kuwa fetusi, ambaye ni hai na anapumua na kukua katika tumbo yako.
 • Sura za usoni zinaanza kukua haraka. Kitoto kinakaa kama kiluwiluwi lakini kina viungo vinvyokaribia vya mtu.
 • Kichwa na shingo zinaanza kupata usawa na huonekana unapotembelea daktari wako katika scana.
 • Unaeza kuskia roho ya mtoto wako ikipiga kupitia skana. Roho yake imemaliza kugawanyika katika vigao vinne na mishipa imeanza kukuua.
 • Viungo vingine vya mwili kama vile maini na wengu zinakua.
 • Chuchu na follicle za nywele zinakua.
 • Mkia wa kiinitete ulio chini ya mgongo umeisha katika wiki ya tisa ya ujauzito.
 • Mtoto anaweza kukanganywa wakati wa skana na kusongesha miguu na mikono. Lakini ni mapema sana kuhisi mtoto akisonga katika kipindi hiki.
Dalili za ujauzito
 • Ugonjwa wa asubuhi utakupata siku yote. Mtaalamu ambaye aliita ugonjwa wa asubuhi hakuita ugonjwa huu sawa kwani wengi hushikwa na ugonjwa huu siku nzima katika kipindi cha kwanza cha ujauzito Lakini kuna njia za kupunguza kichefu chefu hiki.
 • Uchovu na kuumwa na mgongo na kushindwa kuzingatia, ukosefu wa hamu ya kula au pia kupunguza kilo. Inawezekana kuwa dalili hizi zinakuadhiri kwa sababu bado mwili wako unazoea kukidhi ukuaji wa mtoto.
 • Mhemko mbaya utakuadhiri kwa muda mrefu katika wiki ya tisa ya ujauzito.

wiki ya tisa ya ujauzito

Utunzaji wa ujauzito

 • Daktari wako anaweza kushauri ukunywe dawa za vitamini kama folate na multivitamini ili kuusaidia mwili wako kuwa na virutubisho vya kutosha ili kusaidia mtoto anapokua. Jambo la muhimu la kufanya kutoka kwa mwongozo huu wa kila wiki ni kula chakula kidogo mara kadha kwa siku, badala ya chakula kingi kwa mara chache, ukila hii itakuwa rahisi kwa mwili wako kuwa na virutubisho.
 • Maji yana umuhimu sana ili kuuweeka mwili wako na maji kila wakati kwa sababu ya ugonjwa wa asubui wa kutapika ambao umekuwa ukikuadhiri. Ukishindwa kunywa maji jaribu kunywa maji ya sharubati au supu yenye lishe bora ili kusaidia katika kuongeza electrons ulizopoteza. Ukiadhirika na kiwango cha juu cha kichefuchefu tembelea daktari wako. Unaposhikwa na hali ya ukosefu wa maji daktari atakutibu kwa kukuweka maji mwilini (IV drip), kwa hivyo ni vyema tukunywe maji kila wakati.
Orodha muhimu ya kuzingatia
 • Unaweza adhirika na riahi tumboni ambayo ni jambo la kawaida. Vaa nguo ambazo hazikufinyi au rinda kama suruali zako zimeanza kuteremka katika kiuno chako. Kama kwa kweli hauna nguo kubwa kanunue-zoezi hili laweza kubadilisha mhemko wako kwa kukufaya usahau mambo ambayo yanaharibu mhemko wako.
 • Anza kufikiria kuhusu likizo yako ya uzazi. Angalia sheria katika kampuni unayoifanyia kazi.

Republished with permission from theAsianparent

Wiki yako ijayo: 10 weeks pregnant

Wiki yako iliyopita: 8 weeks pregnant

Je, una maswali yoyote kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki? Mama, shaka zako ni zipi wakati huu? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Written by

Risper Nyakio