Will Smith aomba msamaha baada ya kumzaba Chris Rock kofi.

Jada, tunasubiri kwa hamu na gamu GI Jane 2. Kisha akatabasamu na kucheka kama ambavyo waigizaji hufanya wanapochekesha umati. Chris Rock ambaye ni mwigizaji alimwambia Jada Pinkett Smith katika tuzo za Oscars.
Jambo ambalo halimkufurahisha Will Smith, bwanaye Jada, alipoona kuwa bibi yake aliumizwa na maneno yale ya Chris Rock, alitembea kwa ujasiri kwenye jukwaa na kumzaba Chris kofi. Kisha kurudi kwenye kiti chake na kumwambia Chris kwa sauti ya juu, "Weka jina la mke wangu nje ya kinywa chako." Unaweza tazama kilichotendeka hapa.
Baadaye, mwigizaji, mwimbaji na mtu mashuhuri Will Smith aliomba msamaha alipokuwa akipokea tuzo la mwigizaji bora.
"Ningependa kuomba msamaha kwa waandalizi wa tuzo, kwa wasanii wenzangu na waaniaji wenza."

Hapo awali, Jada Pinkett Smith alikuwa amezungumzia suala la kunyoa nywele zake. Anatatizika na hali ya kiafya inayojulikana kama Apolecia. Alismea kuwa ana tatizo la kupoteza nywele na lilipoanza, alikuwa na shaka na hofu nyingi. Na hiyo ndiyo sababu kwa nini alifanya uamuzi wa kunyoa nywele zake.
Chris alishtuliwa na tukio hilo lakini aliendelea na kupatiana tuzo la Makala bora ambalo lilikuwa limempeleka kwenye jukwaa.
Tukio hili limezungumziwa kwa sana. Katika utani ambao Chris alifanya, alikuwa akirejelea filamu iliyotokea mwaka wa GI Jane ya mwaka wa 1997 iliyochezwa na Demi Moore ambaye amenyoa nywele.
Kwa mara ya kwanza Chris alipoyasema maneno yale, ilionekana kama ilikuwa staged ama utani uliopangwa kwani hata Will alicheka hapo mwanzoni. Lakini punde tu utani ule ulipo settle kwake na akaweza kufahamu kilichosemwa kwa bibi yake, sura yake ilibadilika. Jada alionekana kukasirishwa na utani ule, kisha ghafla tu, Will akafika jukwaani alipomzaba kofi. Na ikaonekana kuwa haukuwa utani wa kupangwa.
Chris alionekana kutikiswa na tukio lile lakini aliendelea na tuzo kwa ujasiri, bila kutamka maneno ya ukali wala kufanya kitendo kibaya.

Katika chapisho kwenye kurasa yake ya Instagram, Will Smith aomba msamaha kwa Chris na waandalizi wa Tuzo za Oscars na waliokuwa wakishuhudia tuzo hizo msamaha. Kuwa vurugu za aina yoyote hazikubaliki. Utani ni mojawapo ya kazi yake lakini hangeweza kuchukua utani kuhusu hali ya kiafya ya Jada na akafanya kitu kufuatia hisia zake. Na kuomba msamaha na kuwa tabia yake iliweka doa kwenye safari iliyokuwa nzuri kwa kila mmoja wao.
Soma Pia: Corazon Kwamboka Na Frankie Watengana Baada Ya Kuwa Pamoja Kwa Miaka Mitatu