Willis Raburu anatarajia mtoto wake wa pili.
Willis Raburu ambaye ni mtangazaji katika stesheni ya Citizen pamoja na mpenzi wake Ivy Namu walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili. Kupitia kwa mitandao yao ya kijamii ya Instagram, wawili hawa waliweka video fupi iliyoandamana na ujumbe. "TUMELIFANYA TENA! Mwingine mmoja wa kupenda! #Bazu #Mazu #BabyBazu +1."

Baada ya ujumbe kutamba kuwa Willis Raburu anatarajia mtoto wake wa pili, wafuasi wao waliwapongeza kufuatia habari hizi za kusisimua na kuwatakia kila la heri wanapotarajia mtoto wao wa pili.
Wawili hawa wana mtoto wa kiume pamoja. Mtoto wao atakuwa anafikisha mwaka mmoja mwezi ujao wa Juni. Baada ya uvumi kuibuka kuwa wawili hawa huenda wakawa wanatarajia mtoto mwingine. Kulikuwa na aina zote za upinzani. Huku wengine wakisema kuwa haiwezekani mwanamke aliyejifungua kupitia kwa upasuaji wa C-section kuwa na mimba, hata kabla ya mwaka mmoja kuisha baada ya kujifungua kifungua mimba chake. Huku wengine wakisema kuwa ni mikononi mwa wanandoa kutangaza iwapo wanatarajia mtoto ama la. Kuongeza kuwa, masuala ya ujauzito ni nyeti na mada hii inapaswa kubaki kati ya wanandoa. Iwapo wana tarajia, watawajuza watu katika wakati wao.

Bila shaka Willis Raburu na Ivy wamekuwa kazini. Baada ya wawili hawa kupitisha ujumbe huu, tunaelewa ni kwa nini Ivy hajakuwa akiweka picha zake kwenye mtandao kwa muda sasa. Tofauti na mimba ya kwanza ambapo Namu hakuonyeshana picha zake hadi alipojifungua, mara hii ameweka picha muda kabla. Watu watapata nafasi ya kuona mtindo wake wa mavazi ya mimba.
Ivy Namu ana miaka 27, huku Willis akiwa na miaka 32. Inaonekana wawili hawa wangependa kuwa na umbali mfupi kati ya miaka ya watoto wao. Watoto wanaozaliwa na umbali mfupi wa kimiaka kati yao huwa marafiki wakubwa mara nyingi. Wapenzi hawa walijifungua mara ya kwanza kupitia upasuaji wa elective C-section. Ambapo wanandoa wanachagua tarehe wangependa kupata mtoto wao.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Mavazi Bora ya Watu Mashuhuri Katika Uzinduzi wa Fenty Beauty Kenya