Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Sehemu Nene Ya Baa

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Sehemu Nene Ya Baa

Sehemu nene ya baa inahitaji mazoezi ili kuipunguza. Ila, kuna mbinu zingine za kuipunguza kupitia kwa upasuaji ama utaratibu usio hitaji upasuaji.

Huenda ikakosa kuonekana jinsi ilivyo kwa sababu ya habari tunazo ona kwenye runinga na mitandao, ila miili yetu ni tofauti sana. Kutofautiana kati ya shepu za mwili, chuchu na hata mapaja. Pia, vulva, haibaki nyuma, sehemu nene ya baa ama pubic (fupa) sio jambo lisilo la kawaida.

Yote unayopaswa kujua kuhusu sehemu nene ya baa

Wakati ambapo tofauti kati ya sehemu za mwili kama vile chuchu huenda ikawa ni dhibiti kwa wanawake, tofauti kwenye vulva huenda ikawa sio dhabiti. Hii ni kwa sababu chuchu ni rahisi kuonekana, hasa ikiwa ulikuwa shule ya bweni ya wasichana kama wengi wetu, vulva iko katikati ya miguu. Pia, huwezi penda kuonekana wa kuogofya kwa kuangalia sehemu za siri za mwanamke mwingine. Ama mbaya zaidi, kutambulika kama msichana anaye penda jinsia yake. Katika nchi nyingi za Afrika, kuna sheria kali kuhusu kupenda jinsia sawa.

Kama wanawake, tuna kumbana na matatizo mengi na kuto jiamini kuhusu miili yetu. Na katika jamii ambapo masomo yote unayo weza kupata kuhusu ngono ni tishio kutoka kwa mamako "iwapo mwanamme anakugusa, utapata mimba", huenda ukaona kama mabadiliko kwa mwili wako si ya kawaida ilhali yote ni kawaida. Mojawapo ya mambo yanayo onekana kama sio ya kawaida ni sehemu ya baa ama ya pubic inayo fahamika kama "FUPA" na wanawake wengi wa siku hizi na Beyonce. Walakini, hizi zina ashiria sehemu tofauti za baa yako.

Nini inayo sababisha sehemu nene ya baa?

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Sehemu Nene Ya Baa

FUPA ina maana ya sehemu ya baba yenye nyama nyingi ama nene, ambayo huenda ikajulikana kama uzazi mnene. Ila, sehemu ya juu ya baa iliyo nene ni kama tumbo kubwa. Iko chini ya kitovu na juu ya mon pubis.

Walakini, kitu ambacho watu wengi wanafahamu kama uke ni vulva. Vulva ndiyo sehemu inayo onekana, na ndiko vagina iliko. Vulva huja kwa shepu, saizi na rangi tofauti. Iwapo una shaka, unaweza angalia maktaba haya ya labia.

Mon Pubis ni sehemu iliyo na ufuta ya vulva ambapo nywele kwenye sehemu ya siri hukua.

Kwa asili, Mon Pubis ni sehemu iliyo na ufuta kwenye mwili. Miili yetu huwa kwa njia ambayo pelvis ina lindwa wakati wa ngono. Pia, sababu zingine zinazo ongeza saizi ya FUPA na Mon pubis. Baadhi ya hizi ni:

 • Hormoni
 • Ujana ama utu uzima
 • Umri wa kumaliza kujifungua
 • Kipindi cha hedhi
 • Ujauzito
 • Kuongeza uzito

Kwa sababu ya hizi, saizi ya sehemu yako ya baa itaendelea kubadilika. Hasa kuongeza uzito hufanya sehemu hii kuwa nene na hata wakati mwingine baada ya kupoteza uzito, unene huu haupungui.

Huku kuna maana kuwa naweza punguza saizi ya Mon pubis ama sehemu ya juu ya baa?

fat upper pubic area

Mitindo tofauti ya maisha huenda ikasababisha ngozi kunyooka, kama vile mimba. Na kwa sababu sehemu hii ina ufuta asili, inakuwa rahisi kuhifadhi uzito huu. Walakini, kuna mbinu tofauti za kupunguza unene huu.

 • Mazoezi

Njia pekee ya kupunguza uzito huu kwa kesi hii, ni kufanya mazoezi yanayo ilenga sehemu ya baa katika mazoezi yako. Mazoezi haya yanapaswa kulenga sehemu ya chini ya tumbo yako.

Mazoezi yafutayo ya sehemu ya chini ya tumbo yako yana shauriwa. Una shauriwa kufanya angalau mara tatu kila zoezi mara nne kwa wiki.

Zoezi la V pull:

 • Anza wa mgongo wako na miguu ikiwa imesimama na mikono na juu ya kichwa.
 • Inua miguu yako juu na ujaribu kugusa vidole vya miguu.

Rudi kwa hali uliyo anza.

Hiyo ndiyo mara ya kwanza.

Zoezi ya mountain climbers:

 • Anza kwa plank position.
 • Kwa mbio, leta mguu mmoja juu ya kifua chako na kisha urudishe mguu wako chini
 • Leta mguu mwingine kwenye kifua chako, na urudishe chini ulipo anza.

Hii ni mara ya kwanza.

Zoezi la plank jacks:

 • Anza kwa plank position.
 • Ruka na miguu yote miwili nje na ndani kana kwamba jumping jacks.

Hii ni mara ya kwanza.

Kama tulivyo sema, kupunguza uzito wa mwili ni njia ya afya inayo husisha kula chakula chenye afya na mazoezi na hayo haya tendeki kwa siku moja. Jipe angalau miezi minne ama mitano kabla ya kujaribu hiari hizi.

 • Utaratibu wa upasuaji

Kuna utaratibu wa upasuaji unaweza tumia kupunguza mon pubis na fupa yako unao julikana kama monoplasty. Daktari wa upasuaji anaweza ifanyia kazi sehemu hii kwa kupitia liposuction na mbinu zingine kupunguza unene wa sehemu hii.

 • Utaratibu usio na upasuaji

Kuna utaratibu usio husisha upasuaji kama vile cool sculpting na trusculpt inayo toa unene kwa kutumia mbinu zinazo vunja seli ya ufuta.

Je, napaswa kumwona daktari?

Iwapo una shaka kuhusu uke wako, sehemu ya uke nene, unapaswa kuona daktari. Daktari wako atakupatia mwongozo wa kimatibabu utakao kuongoza na hatua unayo paswa kufuata. Walakini, unapaswa kujua kuwa, kuwa na sehemu nene ya baa hakuna hatari yoyote.

Soma zaidi: Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

Chanzo: Healthline

Chanzo cha picha: Youtube

Written by

Risper Nyakio