Kipindi cha Young Famous and African kilitolewa tarehe 18 mwezi wa tatu 2022. Hiki ndicho kipindi cha uhakika cha kwanza cha Afrika kilichotolewa na Netflix. Baada ya siku mbili, kilikuwa tayari kinaongoza katika orodha ya vipindi vinavyotazamwa nchini Kenya. Bila shaka wanakenya wanapenda vipindi vinavyozungumzia mapenzi na kuigiza. Kilichofanya kipindi hiki kufurahisha zaidi ni kuwa kilikuwa na watu mashuhuri kutoka nchi tofauti Afrika.
Je, ina husu nini?

Reality show hii inazungumza kuhusu maisha ya watu wanaofahamika Afrika kote, nyota katika nyanja tofauti wakifanya kazi, kujivinjari na kukwaruzana mjini Johannesburg huko Afrika Kusini. Watu hawa mashuhuri ni matajiri, wenye umri mdogo na wanaovuma kwenye mitandao, waimbaji, watu wa kuigwa kwenye mitindo ya mavazi huku wakifuata ndoto zao, kutafuta wachumba na kujaribu kufufua mapenzi ya hapo awali.
Kipindi hiki kina waigizaji kama nyota wa nyimbo za Bongo Diamond Platinumz kutoka Tanzania, Zari the Boss Lady kutoka Uganda, Khanyi Mbau, Nadia Nakai, Dj Naked, Andile Ncube, Kayleigh Schwark kutoka Afrika Kusini, Annie Macaulay Idibia, Swanky Jerry na Innocent Idibia (2face) kutoka Nigeria.

Tunaweza kuona uhusiano kati ya Diamond na mpenzi wake wa hapo awali na mama ya watoto wake Zari huku wakiwalea watoto wao kutoka nchi mbili tofauti. Kipindi hiki kinatuonyesha upande tofauti wa mwanamuziki wa bongo tofauti na upande tulio zoea wa kuwa mwimbaji. Urembo wa Johannesburg haufichiki, pamoja na maisha ya kifahari unayokuwa nayo unapokuwa na utajiri na mamilioni ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.
Mbali na kuigiza, kipindi hiki kinachora picha tofauti kuhusu Afrika. Kwa kawaida, bara la Afrika linahusishwa na umasikini, njaa, vita na kukosa mahitaji ya kimsingi. Young, Famous and African inaonyesha picha tofauti, kuwa Afrika pia inapendeza, ina sehemu zaidi na kuwa sio kila mahali kunapokuwa na ukame na njaa.
Picha shukrani kwa: Young Famous and African IG
Hii ni show sio ya Afrika pekee, mbali ya watu katika bara zingine.
Je, ungependa kujua zaidi kuhusu uhusiano kati ya Diamond na Zari na iwapo bado wana pendana na kama wangependa kurudiana? Tazama zaidi Netflix ufahamu kinachoendelea.
Soma Pia:Kenyan Star, Akothee Collapsed On Stage At Luo Festival In Kisumu