Zari Hassan amewasili nchini Kenya. Zarinah Hassan ambaye ni mtu mashuhuri maarufu kwenye mitandao wa kijamii ya Facebook na Instagram kama Zari the Bosslady yuko nchini Kenya.

Kulingana na ujumbe kwenye status yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, amefika nchini kwani ana nunua nyumba mjini mkuu wa Kenya, Nairobi. Alisema, "Niko huku kwa uvumbuzi wa nyumba ya kifahari inayojengwa na mtindo wa kindani wa kisasa, ni mojawapo ya manyumba usiyotarajia Afrika Mashariki."
Zari mwenye miaka 42 ni mwanabiashara kutoka Uganda anayeishi Afrika Kusini. Alizaliwa mjini Jinja huko Uganda, wazazi wake ni Waganda kwa kuzaliwa. Kiwango kikubwa cha utajiri wake kimetokana na uwekezaji katika nyanja ya mali isiyohamishika ama real estate, hoteli ya kifahari ya nyota tano huko Kampala na mashule ye Brooklyn huko Afrika Kusini.

Ana watoto watatu na bwana wake wa kwanza Ivan Semwanga. Wawili hawa waliwachana mwaka wa 2013 baada ya Zari kumshtaki bwanawe kumdhulumu kifizikia. Katika mwaka wa 2017, Ivan alifariki kufuatia mshtuko wa moyo na kisha kuzikwa nchini Uganda. Miaka michache baada ya kifo cha Ivan, Zari walipatana na kuwa na uhusiano na mwimbaji Diamond kutoka Tanzania. Zari na Diamond wamebarikiwa na watoto wawili.
Miaka michache baadaye, wawili hawa walitengana na kila mtu kuenda njia zao. Licha ya kutengana, wanahusika katika maisha ya watoto wao na wangali marafiki.
Zari Hassan amewasili Kenya na watu wengi wanahamu kubwa kuona nyumba yake mpya atakayoivumbua.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Lori Harvey na Michael B. Jordan Wametengana Baada ya Kuwa Pamoja Kwa Mwaka Mmoja