Je, Ni Vyema Kwa Mama Mjamzito Kunywa Zobo?

Je, Ni Vyema Kwa Mama Mjamzito Kunywa Zobo?

Kinywaji cha zobo kina faida nyingi za kiafya. Ila katika makala haya tuna angazia kwa nini mwanamke mwenye mimba anapaswa kukaa mbali na kinywaji hiki.

Zobo ama zoborodo, kama inavyo julikana huko Nigeria na kama Hibiscus katika sehemu zingine ni kinywaji ambacho ni rahisi kutengeneza na kina faida nyingi za kiafya. Huenda kikawa cha afya kwa watu wengi, ila je, zobo ni salama kwa mwanamke mwenye mimba? Katika makala haya, tuna angazia maoni ya wataalum kuhusu mada hii.

Je, kinywaji cha zobo ni salama kwa mwanamke mwenye mimba?

zobo drink

Kinywaji cha zobo kina julikana katika sehemu zingine za dunia kama chai ya Hibiscus, na kukuarifu kuwa kinywaji hiki kutoka kwa matawi ya Roselle sio maarufu Nigeria tu. Kwa mara nyingi kina kunywiwa kikiwa baridi, kina njia ya kufanya koo yako iwe freshi baada ya kuinywa hasa unapo ongeza tangawizi unapo tengeza. Kuna sababu ambayo zobo ni maarudu, na hii ni kwa sababu ya faida yake ya kiafya:

 • Kutibu uchovu na kichefu chefu
 • Kupunguza shinikizo la juu la damu
 • Kufanya mishipa ya damu iwe na nguvu na kuta zake pia
 • Wingi wa antioxidants
 • Kusaidia kupunguza uzito
 • Kutuliza mwili na kutoa mawazo mengi
 • Kuweka matumbo na afya na kusaidia na majukumu yake
 • Kutuliza neva na misuli
 • Kuimarisha mzunguko wa bile
 • Kupunguza cholesterol
 • Kusaidia mwili kutumia iron inayo tokana vyakula
 • Kuboresha uzazi na kuimarisha hamu ya ngono
 • Kuongeza kiwango cha haemoglobin mwilini
 • Kupigana dhidi ya maambukizi kwa sababu yana uwezo wa antimicrobial

Kwa nini zobo sio salama kwa mwanamke mwenye mimba

zobo ni salama kwa mwanamke mwenye mimba

Walakini, kwa faida zake zote za kiafya, swali muhimu linabaki iwapo ni salama kwa wanawake wajawazito kuinywa. Kwa sasa kwani tumeelewa faida zake za kiafya, tunaweza jadili kinywaji hiki kwa kukihusisha na wanawake wenye mimba. Kulingana na utafiti ulio chapishwa katika makala ya African Journal of Alternative and Complementary medicine, kunywa zobo wakati wa mimba huenda kukasababisha mwanamke kujifungua mtoto aliye na uzito mdogo. Watoto walio zaliwa na uzito mdogo wanaonekana wadogo kuliko watoto wanao zaliwa na uzito wa kawaida. Watoto wanasemekana kuwa na uzito mdogo wanapozaliwa na uzito mdogo kuliko pundi 5, ounci 8, yenye maana ya kuwa na kilo chini ya 2.5.

zobo ni salama kwa mwanamke mwenye mimba

Ili kuunga mkono imani za utafiti huu, usitafute mbali sana ila kwa faida za kiafya za zobo hapa juu tuliko sema kuwa inasaidia kupunguza uzito. Ni nzuri sana kwa watu wasio na mimba wanao taka kupunguza uzito, ila mbali sana na kuwa nzuri kwa wanawake wenye mimba. Kikundi kingine cha watu ambao zobo sio nzuri kwao ni wamama wanao nyonyesha. Hii ni kwa sababu zobo inapunguza kiwango cha ulaji cha mwanamke na kupunguza kiwango cha maziwa ya mama ambayo anatoa.

Kwa kuongezea, kunywa zobo wakati wa mimba kunakuwacha na hatari za kuwa na matatizo ambayo huenda yakapelekea uchungu wa mama usio komaa. Kinywaji hiki hufanya hivi kwa kuifanya uterasi yako kubana, na kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake kufika. Wakati wa ujauzito, bidhaa yoyote ama matibabu yanayo kuwa na matawi ya hibiscus yanapaswa kujadiliwa na daktari wako kabla ya kutumia.

Soma piaPregnancy Food: Can A Pregnant Woman Eat Egusi?

Public Health

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio