Mwanamke huwa na kiwewe anapokosa kupata kipindi chake cha kila mwezi. Tazama dalili za mimba kabla ya hedhi zinazo ashiria kuwa mwanamke huenda akawa na ujauzito.
Dalili za mimba
- Kuchelewa kwa hedhi

Sababu kuu ya kuwafanya wanawake kushuku kuwa wana mimba ni kukosa kupata kipindi cha hedhi. Ila, sio mimba pekee ambayo inafanya hedhi kuchelewa. Kuna sababu nyingi kama vile kuongeza uzito, kupunguza uzito kwa kasi, kutumia mbinu za uzazi wa mpango, kusombwa kimawazo, na viwango vya homoni kutokuwa sawa mwilini. Njia hasa ya kubaini iwapo mwanamke ana mimba ni kwa kufanya kipimo cha mimba, cha damu ama cha kinyumbani.
2. Mabadiliko ya matiti
Kushuhudia mabadiliko ya matiti ni kawaida katika mimba. Na mara nyingi kuona mabadiliko ya matiti huwa ishara kuwa mwanamke ana mimba. Mabadiliko haya husababishwa na viwango vya homoni mwilini kubadilika. Mwanamke huenda akahisi kuwa chuchu zake zimefura, zina uchungu ama ni nzito.
3. Kichefu chefu
Kuhisi kutapika ni ishara maarufu ya kuwa na mimba, hasa mapema katika mimba. Hisia hii husababishwa na mabadiliko ya viwango vya vichocheo mwilini. Mara nyingi hushuhudiwa mapema katika siku, ama asubuhi. Hata hivyo, hakuna wakati spesheli, mama anaweza kuhisi kutapika wakati wote wa siku.
4. Maumivu kwenye tumbo

Kuumwa na tumbo sawa na mwanamke anapokuwa na hedhi hufanyika baada ya yai kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Ila, tofauti na maumivu wakati wa hedhi, maumivu ya mimba ni mepesi na hupungua baada ya muda. Iwapo uchungu hautapungua, wasiliana na daktari wako, hasa ikiwa uchungu huu utaandamana na kuvuja damu.
5. Kuchoka wakati wote
Uchovu mwingi ni ishara ya mapema ya mimba. Uchovu huu husababishwa na ongezeko la viwango vya progesterone mwilini hasa katika wiki za kwanza chache za ujauzito. Ni vyema kwa mama kutenga muda wa kupumzika vya kutosha. Mama anapohisi hivi, ni vyema kuomba usaidizi kazini zake ili apate wakati tosha wa kujilaza.
6. Kuvuja damu nyepesi
Kuvuja damu nyepesi karibu na wakati mama anapotarajia kipindi chake cha ujauzito. Damu hii hufuata kujipandikiza kwa yai kwenye kuta za uterasi. Ni nyepesi ikilinganishwa na damu ya hedhi, na pia haijakolea rangi. Hata hivyo, sio wanawake wote wanaopata ishara hii.
Hizi ndizo dalili za mimba kabla ya hedhi ambazo zinamwashiria mwanamke kuwa ni wakati bora wa kufanya kipimo cha mimba.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Unatarajia Nini Kwenye Mimba Ya Miezi Mitano?