Ishara 7 Katika Mimba Zinazo Ashiria Kuwa Kuna Hatari

Ishara 7 Katika Mimba Zinazo Ashiria Kuwa Kuna Hatari

Ni vyema kwa mama mwenye mimba kuwa na maarifa ya ishara za hatari katika mimba ili afahamu wakati anapo paswa kuwasiliana na daktari wake

Baadhi ya ishara wakati wa ujauzito huwa kawaida na ni sawa, ila kuna zingine ambazo zina taswishi. Utajuaje tofauti? Kwa sasa, huenda swali lako kuu ni jinsi ya kutofautisha ishara za hatari katika mimba na zisizo hatari. Mama mjamzito anapaswa kuwa makini na mwili wake katika safari ya ujauzito. Kujua jinsi mwili wako unavyo kuwa wakati wa kawaida kutamsaidia kujua kunapokuwa na mabadiliko mwilini.

Ukiwa na shaka, wasiliana na daktari wako. Angalia baadhi ya ishara zenye maana kuwa kuna jambo lililo haribika mahali.

Orodha ya ishara za hatari katika mimba

kupoteza mimba ya wiki mbili

 

  1. Kuvuja damu kwa wingi

Kuvuja damu kuna maana tofauti katika kila hatua ya ujauzito. Kutoa damu nyingi, maumivu ya tumbo sawa na uchungu wa hedhi na kuhisi kuzirai katika trimesta ya kwanza, huenda ikawa ni ishara ya ujauzito wa ectopic. Wasiliana na mtaalum wa afya bila kukawia kwani hali hii ina hatarisha maisha yako.

Kutoa damu nyingi na kuumwa na tumbo katika trimesta ya kwanza ama mwanzoni mwa trimesta ya pili, huenda ikawa ni ishara ya kuharibika kwa mimba. Kutoa damu na kuumwa na tumbo katika trimesta ya tatu huenda kukawa ni ishara ya kujeruhiwa kwa placenta. Kuvuja damu katika ujauzito ni suala nyeti na linapaswa kushughulikiwa kwa kasi.

2. Kutapika sana ama kuhisi kichefu chefu

Kuhisi kichefu chefu ni ishara ya mimba na pia ni kawaida katika mimba. Hisia hii ikizidi, huenda kukawa na suala linalo paswa kutatuliwa. Ukishindwa kula na kunywa, uko katika hatari ya kukosa maji tosha mwilini na kuathiri afya ya fetusi. Ukihisi kulemewa na kichefu chefu, hakikisha umemwona daktari wako.

3. Kubanwa ama kukazwa mwanzoni mwa trimesta ya tatu

Kubanwa huenda kukawa ishara ya uchungu wa uzazi usio komaa. Lakini mama wengi wa mara ya kwanza, huenda waka changanywa na kudhani ni uchungu wa uzazi usio wa kweli (Braxton-Hicks contractions). Ukiwa katika trimesta yako ya tatu kisha uanze kuhisi kubanwa, wasiliana na daktari wako akutibu.

4. Kuvuja kwa maji ya mama

Ukiwa nyumbani ukifanya kazi zako za kila siku, kisha usikie maji kwa wingi yakitiririka miguuni mwako, huenda ikawa maji yako yame vuja. Lakini katika mimba, uterasi iliyo nenepa inaweza shinikiza kibofu chako cha mkojo. Kwa hivyo huenda ikawa ni mkojo unatiririka. Ikiwa hauna uhakika, enda msalani, maji hayo yakiendelea, maji yako yame vuja, wasiliana na daktari wako ama utembelee kituo cha afya kilicho karibu nawe.

5. Kuumwa na kichwa, tumbo ama kufura katika trimesta ya tatu

Ishara hizi zote huenda zikawa za preeclampsia ambayo ni hali sugu katika ujauzito na inayo hatarisha maisha. Hufanyika baada ya wiki ya 20 ya ujauzito na ina ashiriwa na shinikizo la juu la damu na kuwepo kwa protini kwenye mkojo wako. Enda hospitalini na ufanyiwe vipimo vya shinikizo la damu.

6. Ishara za homa (flu)

Wataalum wana shauriwa wanawake kupatiwa chanjo ya flu kwani wanawake wengi wajawazito wana uwezekano mwingi wa kugonjeka na kupata matatizo mengi kutoka na flu ikilinganishwa na wanawake wengine katika msimu wa flu. Lakini ukipata flu, wasiliana na daktari wako kwanza, kabla ya kuenda hospitalini.

7. Mtoto kuto songa tumboni

Ishara 7 Katika Mimba Zinazo Ashiria Kuwa Kuna Hatari

Mtoto aliyekuwa ana songa kila mara anapo koma kusonga ama kupunguza mwendo wake tumboni kuna maana gani? Ni kawaida?

Kujaribu kumgusa gusa kunaweza kusaidia kudhihirisha kama kuna tatizo. Wataalum wa afya wana shauri kujaribu kula ama kunywa kitu baridi. Kisha ulale kwa upande kuona kama mtoto ata songa. Kuhesabu mateke pia kunaweza saidia, kulingana na Nicole Ruddock, professa msaidizi wa afya na matibabu ya wanawake wajawazito katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Texas. Hakuna nambari hasa ya mateke ambayo mtoto anapaswa kurusha kila siku. Lakini kama mama, unaweza jua kama mtoto anaendelea kurusha mateke tumboni ama amewacha, kati ya mateke 10 ama zaidi kwa masaa mawili. Nambari chini ya hiyo ni ishara kuwa unapaswa kuongea na daktari wako mapema uwezavyo.

Mama anashauriwa kuna makini sana katika mimba na kuto puuza jambo analo ona kuwa sio la kawaida. Ukishuhudia mojawapo ya ishara hizi za hatari katika mimba, hakikisha kuwa una tembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe ama kumpigia daktari wako bila kukawia.

Chanzo: NHS

Soma pia:Ongezeka Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

Written by

Risper Nyakio