Usitumie Dawa Ya Meno Kurejesha Uke Mkubwa Uliolegea- Wataalum Waonya Mabinti

Usitumie Dawa Ya Meno Kurejesha Uke Mkubwa Uliolegea- Wataalum Waonya Mabinti

Kadri wanawake wengi wanavyo zidi kupata umri zaidi, huenda wakawa na swali la ‘jinsi ya kubana uke uliolegea’. Hata kama jambo hili halipaswi kukutia wasiwasi, (jinsi ulivyo m-bana huko chini), uke wao hufanya wanawake wengi wakawa na maswali mengi na kutaka kujua jinsi wanaweza rejesha uke mkubwa uliolegea.

Hawana ujasiri kuhusu miili yao, wanakuwa na shaka kuhusu ujinsia wao na kuhisi kana kwamba hawatoshi. Pengine huenda hii ikawa sababu kwanini wamejaribu kutafuta suluhu za aina zote kutatua jambo hili. Ikiwemo kutumia dawa ya meno kukaza uke wao. Naam, jambo hili lina fanyika. Kutoka kwa kutumia vitu kama apple cider vinegar na aina zote za bidhaa za kukaza uke.

how to tighten vagina

“Jinsi ya kukaza uke” Bila shaka si kwa kutumia dawa ya meno

Daktari wa matibabu, Oluwole Yusuf amewaonya mabinti dhidi ya kutumia dawa ya meno kubana uke uliolegea. Anasema kuwa wanapaswa kujilinda dhidi ya kuto hisi starehe na maambukizi mengineyo.

Yusuf  aliiambia News Agency ya Nigeria (NAN) siku ya Alhamisi huko Ilorin kuwa shaka ya wanawake ya sasa hivi ya kuwa na uke mkonda sio ya afya. Pia, kutumia dawa ya meno kukaza uke ni jambo lenye hatari nyingi. Kulingana na yeye, uke ni kiungo cha mwili ambacho mwili huosha bila usaidizi wowote.

Kubana Uke Uliolegea: “Usikubali Watu Waongee Hasi Kuhusu Mwili Wako” – Daktari. Yusuf

Dawa ya meno ina kemikali nyingi ambazo zina hatari kali kutumika kwa sehemu ya mwili kama uke. Na kutumia bidhaa kama dawa ya meno huenda kukaharibu viumbe vinavyo kusudiwa kulinda uke kutokana na maambukizi. “Wakati ambapo uke hauwezi jilinda tena, mwili uko kwa hatari ya maambukizi ambayo huenda baadaye yaka haribu tubes na kuzuia nafasi za kupata mimba, Yusuf alisema.

Aliwahimiza wanawake wasijikubalishe kuongelewa hasi kuhusu miili yao na wenzi wao. Alionya kuwa huenda kukasababisha ‘safari ya kujiharibu na kujuta’.

“Mwanamme anapokuambia kuwa umelegea sana huko chini na unataka kuharibu maisha yako ya usoni kwasababu ya hilo, baadaye atakuwacha kwa jambo hilo.

“Kuwa na ujasiri kuhusu mwili wako na ukubalishe mwili wako kubaki ulivyo. Baadhi ya mazoezi tofauti na utaratibu unaweza fanyika polepole kubana uke bila ya kuhatarisha maisha ya mwanamke. “Mazoezi ya Kegel na Yoga ni baadhi ya mazoezi ambayo yanaweza fanya uke uliolegea uwe mkonde bila ya kufanya mambo yatayo hatarisha maisha yako,” Yusuf alisema.

Jinsi ya kubana uke uliolegea kwa njia asili

vaginal tightening

Njia asili kabisa ya kuhakikisha kuwa uke wako ni freshi na mchanga kwa wakati mrefu ni kufanya mazoezi ya misuli ya pelviki. Unaweza fanya hivi kwa njia tofauti sana.

Tiba ya mwili ya misuli ya pelviki

kubana uke uliolegea

Kulingana na jukumu la misuli yako ya pelviki, mtaalum wa tiba ya mwili anaweza tengeneza ratiba ya mazoezi. Ratiba hii inalingana na mahitaji maalum na hali ya uke wako. Kwa mfano, iwapo umejifungua tu, ratiba ya mazoezi yako itakua mepesi kwanza kisha yazidi hapo baadaye.

Jinsi ya kubana uke kwa kutumia mazoezi ya kegel

how to tighten vagina

Hizi ni maarufu sana na huenda ukawa umezisikia ama kusoma kuzihusu. Haya ni mazoezi yanayo husu hatua ambazo zinapunguka na kutuliza misuli ya pelviki. Kabla ya kuanza, utahitajika kuenda msalani. Kaza misuli yako ya pelviki na uishikilie kwa hesabu ya nane hadi kumi, wachilia kisha urudie. Utagundua tofauti kubwa ukifanya hivi mara kwa mara.

Yoga na pilates

Mazoezi ya yoga na pilates pia inasaidia na kukaza uke. Mazoezi haya yote hunyoosha mwili na kuufanya uwe na uwezo wa kunyooka na kurudi hali yake asili. Na hii ni kweli kwa misuli yako ya pelviki pia. Baadhi ya mazoezi ya yoga ni bora zaidi kwa jambo hili. Kwa mazoezi ya pilates, husisha ‘bridge’ kwenye ratiba yako na itakusaidia sana.

Mashine za kukaza misuli ya mwili

kubana uke uliolegea

Pia unaweza jaribu mashine za kukaza sehemu yako ya pelviki. Unaweza husisha bidhaa muhimu kama vile ‘pelvic floor stimulator, Kegel exerciser, pelvic floor muscle toner ama pelvic toner, pelvic floor toner, na piapelvic floor exerciser. Daktari wako huenda pia akakushauri kutumia barbells, vaginal weights ama cones zilizo tengenezwa hasa kushikwa ndani ya uke wako.

Jinsi ya kukaza uke wako? Kula chakula chenye afya

Lazima ule lishe yenye afya wakati wote. Imedhibitiwa kuwa chakula kinacho faa kinaweza saidia uke wako kuwa na afya, furaha na mbali na maambukizi yoyote.

Kwa mfano, iwapo ungependa uke wako ukose maambukizi yoyote, unapaswa kunywa chai ya kijani na kuhakikisha kuwa haikosi kwenye ratiba yako. Catechins zinazo kuwa kwenye chai hii hupita kwa mfumo wa mkojo na kupunguza ukuaji wa bakteria hatari.

Mara kwa mara, kula probiotics kama vile yogurt, ogi, masa na zinginezo huenda pia kukakusaidia katika kutimiza lengo lako la kuwa na uke wenye afya. Zinasaidia kusawasisha bakteria nzuri na mbaya.

Hizi ni njia asili ambazo zinaweza kusaidia kubana uke uliolegea. Ni vyema kwa kila mwanamke kujua kuwa hapaswi kuhatarisha maisha yake ili kumfurahisha mwanamme yeyote yule. Ukifanya mambo haya mara kwa mara na uhusishe lishe yenye afya, tujulishe inavyo saidia uke wako na maisha yako ya kimapenzi.

Soma pia: Huenda Uke Wako Ukachomeka- Wataalam Waonya Dhidi Ya Mvuke Wa Uke

Written by

Risper Nyakio