Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Mrembo! Vyakula Hivi Vitakusaidia

Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Mrembo! Vyakula Hivi Vitakusaidia

Hatua hizi zinamhakikishia kila mama mwenye mimba kuwa atapata mtoto mrembo.

Hivi sasa kwani una mimba, huenda ukataka kujua jinsi ya kujifungua mtoto mrembo. Vitu unavyo fanya unapokuwa na mimba vita athiri maumbile ya mtoto wako. Na sio imani za kale kuwa mtoto wako atazaliwa na meno usipokula vyakula vyenye pilipili. Kwa hivyo tume orodhesha vidokezo vya vyakula vya kula ili kujifungua mtoto mwenye afya. Tazama hapa chini:

Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Mrembo: Vyakula Muhimu Vya Kuongeza Kwa Lishe Yako

1. Bidhaa za maziwa

what to eat to have a beautiful baby

Unapokuwa na mimba, ni muhimu kwako kula bidhaa za maziwa. Zitakupa protini na kalisi zaidi zinazo hitajika katika kuegemeza mtoto wako anaye kua. Kunywa angalau glasi moja ya maziwa kila siku na maziwa ya bururu ili kuhakikisha kuwa mtoto wako ana afya.

2. Mayai

what to eat to have a beautiful baby

Mayai ni vyakula bora! Ni vyanzo vyema vya vitamini, protini na madini. Protini zilizoko kwenye mayai zinayafanya kuwa bora kwa mtoto anaye kua kwani yana tengeneza seli za fetusi. Mayai yana wingi wa choline; ambayo inahitajika katika ukuaji wa akili ya mtoto wako na mfumo wa neva.

3. Mandizi

what to eat to have a beautiful baby

Mandizi yatakupa folic acid, kalisi, potassium na vitamini B6. Pia yana wingi wa antioxidants na yana saidia kuongeza nishati yako. Kwa hivyo ni wazo la busara kuyaongeza kwenye lishe yako unapokuwa na mimba.

4. Viazi vitamu

jinsi ya kujifungua mtoto mrembo
Viazi vitamu ni chanzo chema cha beta-carotene inayo badilishwa kuwa vitamini A ndani ya mwili wako. Na ni muhimu kwa ukuaji wa seli na tishu. Vitamini A pia inasaidia katika kuboresha kinga na uwezo wako wa kuona. Kwa hivyo, kula viazi vitamu zaidi kunaweza kuwa na faida kwa mama na mtoto aliye tumboni la mamake.

5. Jamii ya kunde

beans

Mimea iliyoko kwenye familia hii ni kama vile lentils, soybeans, peas, beans, chickpeas na peanuts. Ni vyanzo vikuu vya fibre inayotokana kwa mimea, protini, folate, kalisi, na iron na zote hizi ni muhimu sana kwa wamama wenye mimba. Kuwa na viwango tosha vya folate kutahakikisha kuwa mtoto wako anazaliwa akiwa na afya na kuwa amelindwa kutokana na maradhi na maambukizi siku za usoni.

6. Njugu

jinsi ya kujifungua mtoto mrembo

Njugu zina ladha na zina wingi wa ufuta wenye afya, na kuzifanya chaguo bora la vitamu tamu unapokuwa na mimba. Zina omega-3 fatty acids, protini, fibre na virutubisho vingine muhimu ambavyo ni lazima ili mtoto wako akue ipasavyo.

7. Sharubati ya machungwa

jinsi ya kujifungua mtoto mrembo

Kutoka kwa chungwa, utapata folate, potassium na vitamini C. Mtoto wako atapata virutubisho anavyo hitaji ambavyo vitasaidia kuepuka matatizo ya kuzaliwa. Vitamini C iliyoko kwenye sharubati ya machungwa itaongeza uwezo wa mtoto wako wa kutumia iron mwilini. Kwa hivyo hakikisha kuwa unakunywa glasi ya sharubati ya machungwa unapokula chamcha chako.

8. Mboga zenye majani

veggies

Mboga zenye majani zina wingi wa virutubisho na sote tunajua kuwa zinaweza saidia katika kulinda mwili kutokana na maradhi mengi. Ni chanzo kikuu cha antioxidants, kalisi, protini, fibre, folate, vitamini, potassium, mboga za kijani ni ongezeko bora kwenye lishe yako.

9. Oatmeal

Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Mrembo! Vyakula Hivi Vitakusaidia

Oatmeal ina aina tofauti ya faida za kiafya. Kula wanga ni muhimu kwetu sote, hasa kwa wanawake walio na mimba kwani inampa nishati ya kufanya kazi zake za kila siku. Oatmeal ni chanzo kikuu cha wanga, selenium, vitamini B, phosphorous na kalisi. Kwa hivyo ile kama kiamsha kinywa unapokuwa na mimba.

10. Salmon

Salmon ina wingi wa omega-3 fatty acids ambazo ni nzuri kwa moyo wenye afya. Kuwa na omega-3 tosha kwenye lishe yako ni muhimu kwa wanawake walio na mimba kwani inasaidia katika ukuaji wa akili na macho ya fetusi. Salmon ni chanzo kikuu cha vitamini D, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa na kinga ya mwili.

Vidokezo Vingine Muhimu Vya Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Mrembo

Orodha ya mambo ya kufanya ukiwa na mimba kujifungua mtoto aliye na afya ina njia zilizo aminika za kujifungua mtoto mrembo na mwenye afya.

Hapa ni baadhi ya vitu ambavyo unapaswa kufanya:

  • Kula lishe iliyo na wingi wa matunda na mboga
  • Kunywa maji mengi
  • Weka mazingira yako yakiwa safi
  • Maoezi mepesi
  • Mtembelee daktari wako mara kwa mara
Kujifungua Mtoto Mwenye Afya. Epuka Mambo Yafuatayo Unapokuwa Na Mimba

Kwa sasa kwani unajua cha kufanya unapokuwa na mimba kujifungua mtoto mwenye afya, hapa ni baadhi ya vitu unavyopaswa kuepuka.

1. Uvutaji sigara

Kuvuta sigara kuna athari hasi kwa afya yako na ya mtoto wako. Kuna kemikali 4000 kwenye kila sigara na kuna maana kuwa unaweza hatarisha mtoto aliye tumboni mwako kwa kuvuta sigara unapokuwa na mimba. Sigara zina athari hasi na zina weza punguza kiwango cha oxygeni ambayo mtoto wako anapata. Mbali na hatari ya kuzaliwa kabla ya wakati, huenda akawa na matatizo ya kula, ya moyo na ya kupumua.

2. Vileo

Vileo ama pombe zinaweza athiri sura na ukuaji wa mtoto wako. Iwapo ungetaka kujua cha kufanya unapokuwa na mimba kupata mtoto mwenye afya, kuwachana na pombe ni hatua kubwa. Kunywa pombe unapokuwa na mimba kunaweza athiri mtoto wako na huenda akazaliwa na tatizo la Fetal Alcohol Syndrome (FAS). Watoto wenye FAS hukua na changamoto za sura na pia za tabia, maumbile na ukuaji.

3. Fikira nyingi

Kulingana na WebMD, kukwazwa kifikira unapokuwa na mimba huenda kuka badilisha jinsi ubongo wa mtoto wako unavyo kua. Na kuka athiri tabia yake baada ya kuzaliwa ama matatizo ya kusoma. Fikira nyingi huenda zika sababishwa na kazi yako, mahusiano yako ama maisha yako kwa jumla. Usikubali vitu vikutatize unapokuwa na mimba. Itisha usaidizi unapohisi umelemewa.

4. Kula chakula kingi

Hamu ya vyakula unapokuwa na mimba ni jambo la kawaida. Homoni zako zinazo badilika huenda zikakufanya uwe na hamu ya kula vyakula ambavyo kwa kawaida huwezi vigusa. Kula chakula kingi huenda kukakufanya kupata uzito mwingi zaidi, kubaki na maji mwilini ama hata kuumwa na uchungu.

Kuwa na mtoto mwenye afya, na mrembo kuna wezekana. Unapaswa kujua tu cha kufanya unapokuwa na mimba kuwa na mtoto mwenye afya. Ukifuata vidokezo kwenye makala haya, nafasi kubwa ni kuwa utajifungua mtoto mrembo na utajishukuru!

Kumbukumbu: WebMD

MedicineNet

Soma pia: Baby upper teeth first myth: Nigerian Culture

Written by

Risper Nyakio