Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Bara la Afrika lina vifo vingi vya wamama wenye mimba vinavyo husishwa na matatizo ya ujauzito. Tuta kumbana vipi na changamoto hizi ili kupunguza idadi ya vifo? Soma zaidi...

Karibu wanawake 830 hufa kila siku kufuatia matatizo ya ujauzito na kujifungua yasiyo epukika. Nusu ya wanawake hawa huishi Sub-Saharan Afrika. Asilimia 99 ya vifo vyote vya wamama hutendeka katika nchi zinazo kua. Vifo vya wamama viko juu zaidi katika sehemu za mashinani na katika jamii masikini. Vijana wachanga huwa na nafasi za juu za hatari na vifo kufuatia ujauzito ikilinganishwa na wanawake walio komaa. Watafiti wanasema kuwa wanawake hawa hawakufi kufuatia magonjwa. Lakini kufuatia kukosa hatua za utunzi wa afya za kimsingi.

Matatizo ya ujauzito ni changamoto za afya zinazo tendeka wakati wa ujauzito. Mara nyingi zina husisha afya ya mama, afya ya mtoto ama zote mbili. Kabla ya kupata mimba, baadhi ya wanawake huwa na shida za afya ambazo huenda zika sababisha matatizo ya mimba. Shida zingine huibuka wakati wa mimba. Iwapo shida fulani ni maarufu ama nadra, kuna njia za kusuluhisha matatizo yanayo ibuka wakati wa mimba.

Baadhi Ya Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

matatizo ya ujauzito

 

Katika utafiti ulio fanyika katika miji na mitaa katika nchi 6, wanawake 3-9 katika kila kujifungua 100 walipata changamoto nyingi ambazo zina husishwa na mimba. Angalau 1/3 ya hizi zilizo na sepsis ama kutoboka kwa uterasi, na angalau 1/5 ya hizi zilizo kuwa na eclampsia, walikufa.

Utafiti ulitahini tukio la vifo vinavyo husishwa na mimba katika miji mikuu ya Burkina Faso, Cote d'Ivoire, Mali, Mauritania na Niger na katika mitaa miwili midogo na mji mkuu wa Senegali. Katika zote, wanawake 20,326 wali shiriki. Kwa wastani, kulikuwa na wanawake wa miaka 26 na waliokuwa na mimba ya wiki 27 walio shiriki. Shida zilizo ripoti na waliokuwa na mimba ya wiki 36 zilikua:

Kutoka damu sana maarufu kama haemorrhaging

Hii huenda ikawa ni kufuatia kutoboka kwa placenta, hali ambapo placenta ina tengana na kuta ya uterasi kabla ya kujifungua. Huenda ika maanisha kuwa fetusi haipati hewa tosha. Kuna sababu zingine za haemorrhaging baada ya kujifungua.

Maambukizi (mara nyingi baada ya kujifungua)

Haya mara nyingi yana husisha maambukizi ya mfumo wa mkojo na kuhatarisha kuathiri mafua na kusababisha kuharibika kwa mimba. Baada ya kujifungua, mwanamke huenda aka ambukizwa na Strep Kikundi cha B; Hepatitis ama bacterial vaginosis. Ishara zina husisha uchafu ulio na harufu kana kwamba ya samaki, kuhisi kujikuna unapo kojoa, kuhisi kutapika na kadhalika.

Shinikizo la juu la damu wakati wa mimba(Pre-Eclampsia na Eclampsia)

Maarufu kama toxemia, ina tendeka kwa mwanamke mjamzito baada ya wiki yake ya 20 ya ujauzito. Na kusababisha shinikizo la juu la damu na matatizo yanayo husika na maini na viungo vingine. Ishara huwa kama vile ongezeko la ghafla la shinikizo la damu, protini nyingi kwenye mkojo, kufura kwenye mikono na uso wa mwanamke na kuumwa na kichwa.

Ugonjwa wa kisukari wa Gestational

Viwango vya juu vya sukari kwenye damu wakati wa mimba. Mara nyingi, hakuna ishara. Baadhi ya wakati, mwanamke ata shuhudia kiu nyingi, njaa na uchovu. Kipimo cha screening kita dhibitisha viwango vya sukari.

Mimba ya Ectopic

Mimba ya aina hii, yai fertilized lina jishikilia nje ya uterasi, mara nyingi kwenye fallopian tube. Ishara: uchungu kwenye tumbo, mabega, kutoka damu kwenye uke na kuhisi kuzirai.

Anaemia/ Kukosa damu mwilini

Mwanamke mjamzito anapokuwa na kiwango cha chini kuliko cha kawaida cha seli nyekundu zenye afya. Baadhi ya ishara ni kukosa nguvu, ngozi kukosa rangi, kuhisi kuzirai na kukosa hewa.

Kutoa mimba kusiko kwa afya

Katika Afrika, wanawake wengi hujaribu kutoa mimba kwa kutumia njia sizio salama, baadhi ambazo hazikubaliki. Matokeo ni tatizo ama shida nyingi za kiafya kutokea ambazo huenda zika sababisha kupoteza maisha.

Uchungu wa uzazi usio komaa

Baadhi ya wanawake huingia kwenye uchungu wa uzazi kabla ya kufika wiki 37 za mimba kwa sababu tofauti hata kutoka kwa amniotic fluid na fikira nyingi. Kutoa uchafu kwenye uke, shinikizo kwenye pelviki na kuumwa; maumivu ya mgongo inayo toka kwenye tumbo na maumivu mara kwa mara.

Watoto wachanga kupata mimba

Wanawake wana jihusisha katika ndoa za mapema kwa sababu tofauti zinazo husishwa na tamaduni na imani. Kama matokeo, bara lime shuhudia nambari ya juu ya wamama wachanga na mimba ya watoto duniani kote. Changamoto nyingi za ujauzito ni kwa sababu mabinti ni wachanga sana.

Zinazo salia zina sababishwa na kuhishwa na maradhi kama malaria na ukimwi wakati wa ujauzito.

Sababu Zinazo Saidia Matatizo Ya Ujauzito Na Vifo Vya Wamama Afrika

Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

  1. Umasikini
  2. Kukosa utunzi bora wa ki afya
  3. Kukosa ujumbe na maarifa
  4. Kukosa usaidizi
  5. Matendo ya kitamaduni

Ili kuboresha afya ya wamama, visuizi vinavyo zuia kupata afya bora ya wamama walio na mimba lazima zitambuliwe na kuangaliwa katika viwango vyote vya mfumo wa afya.

Kuboresha Afya ya Wamam Wenye Mimba Afrika

matatizo ya ujauzito

Matatizo mengi ya ujauzito yanaweza epukika. Suluhu za utunzi wa afya kwa kudhibiti changamoto zinazo ibuka wakati wa mimba zina julikana vyema. Wanawake wote wanahitaji utunzi kabla ya kujifungua wanapokuwa na mimba. Pia wana hitaji utunzi makini wanapokuwa wakijifungua na utunzi na kuegemezwa wiki baada ya kujifungua.

Ni muhimu kwa visa vyote vya kujifungua viangaliwe na wataalum wenye maarifa hayo, kwani udhibiti na matibabu kwa wakati unaofaa unaweza fanya tofauti kati ya maisha na kifo kwa mama na mtoto.

Ili kuepuka vifo vya wamama, ni muhimu kuepuka mimba ya mapema na isiyo tarajiwa. Wanawake wote hata mabinti wachanga wana hitaji kupata bidhaa za kudhibiti kupata mimba. Pia kuna paswa kuwa na njia salama za kutoa mimba inavyo hitajika na sheria na utunzi bora baada ya kutoa mimba.

Chanzo: World Health Organization

Soma pia: Ishara Za Kupoteza Mimba Ya Wiki Mbili

Written by

Risper Nyakio