Matayarisho Rahisi Ya Chakula Cha Ikokore

Matayarisho Rahisi Ya Chakula Cha Ikokore

Matayarisho yetu ya chakula cha ikokore ni rahisi zaidi ambayo utakayo pata. Chakula hiki cha Ijebu sio kitamu tu; ila kina ladha, virutubisho na chenye afya. Kiungo kikuu ni mhogo ambao una limwa kwa umuhimu wake wa chakula na matibabu.

Utafiti umedhihirisha kuwa mhogo unaweza tumika kuegemeza mahitaji ya watu wengi ya fiber na madini na pia una jukumu la kulinda dhidi ya magonjwa sugu.

 

Matayarisho Rahisi Ya Chakula Cha Ikokore

Chanzo: Ajapaworld.com

Ni rahisi kivipi kutengeneza chakula cha Ikokore?

Ikokore (baadhi ya wakati inajulikana kama ifokore) ni rahisi sana kutayarisha. Kuongeza kiwango kikubwa cha protini ni mojawapo ya siri ya kufanya chakula hiki cha ikokore kiwe na ladha. Protini kutoka kwa wanyama ziko kwa orodha ya viungo – nyama ya ng’ombe, kuku, crayfish, catfish ya iliyo kaushwa na moshi, periwinkles, crabs, lobster, nyama ya mbuzi, kpomo na kadhalika.

Matayarisho
 • Mhogo
 • Mafuta ya nazi
 • Nyama ya ng’ombe, samaki na kuku
 • Pilipili ya chaguo lako (pilipili ya Nsukka, shombo, tatashi, chilli na ama pilipili iliyo kaushwa)
 • Samaki wa kukaushwa na moto ama moshi (samaki wa bonga, stockfish na ama wild catfish)
 • Samaki freshi wa panla aliye katwa ama samaki wa scumbia (kwa hiari yako)
 • Ponmo
 • Periwinkles
 • Ground crayfish
 • Lobsters na prawns (kwa hiari yako)
 • Iru ama ogiri Ijebu ama okpei
 • Vingo vya ladha vya hiari yako
 • Chumvi.

Mwongozo wa hatua baada ya nyingine ya jinsi ya kutengeneza Ikokore

Matayarisho Rahisi Ya Chakula Cha Ikokore

Chanzo cha picha: William Haun, Flickr

Hatua ya 1

Toa ngozi ya mhogo. Osha mhogo vizuri na uisiage. Ama una utumie sehemu konda kabisa ya kifaa chako cha kusiaga.

Mara nyingi, utapata matokeo yanayo teleza kwa sana. Hakikisha kuwa bakuli haitoki mikononi mwako.

Hatua ya 2

Weka chungu kisafi motoni. Ongeza glasi mbili ama tatu za maji, iwapo unatumia hadi nusu ya mhogo wako.

Kubalisha maji yachemke kabla ya kuongeza kiwango kidogo cha mafuta ya nazi. Usiweke mafuta mengi. Kubalisha mafuta yapate moto vizuri.

Hatua ya 3

Weka nyama yako ya kuku ama ya ng’ombe iliyo pikwa kidogo. Toa samaki wako mifupa kisha umwage. Ongeza idadi tosha ya crayfish kwenye chungu chako cha kupika. Ongeza pilipili na nyama ya kuku ama ng’ombe na uwache iive kwa dakika kumi na mbili hadi kumi na tano.

Matayarisho Rahisi Ya Chakula Cha Ikokore

Chanzo: wivestownhallconnection.com

Hatua ya 4 (kwa hiari yako)

Unaweza fanya uamuzi wa kuchota nyama yako na samaki kutoka kwa chungu ili ziwe tayari wakati ambapo chakula chako kitakuwa karibu kuiva. Iwapi, walakini utachagua kuwacha nyama yako ama samaki kwenye chungu, usiwe na shaka utakapo pata kuwa zime chomeka nusu na kubaki kwenye upande wa chini wa chungu chako. Ikokore sio aina ya chakula unacho pika uki changanya.

Hatua ya 5

Weka chumvi na viungo vya ladha kwenye bakuli ya mhogo ulio siagwa. Changanya pamoja.

Hatua ya 6
Chota viwango vya mhogo kwenye chungu. Endelea kuongeza mihogo, ili iive na itengane iwe kana kwamba mipira.

Weka kifuniko tofauti cha chungu. Na uwache ziive kwa dakika kumi.

Hatua ya 7

Mwaga samaki aliye katwa vizuri, kpomo, shaki, periwinkle na ground crayfish. Onja chakula hicho na uamue iwapo ungependa kuongeza pilipili na chumvi zaidi.

Iwapo ulichota nyama ya ng’ombe ama samaki, huu ndio wakati bora wa kuziongeza kwenye chungu chako.

Punguza moto uwe wa wastani ama kiwango kidogo, na ukubalishe chakula cha ikokore kiive kwa joto ya chini. Funika chungu chako na uwache chakula hicho kiive kwa dakika tano zaidi.

Pakua kingali moto.

Vidokezo

Chochote ukifanyacho, epuka majaribio ya kuchanganya uji ule. Kidokezo muhimu cha kujua ni kuwa wakati wa kutengeneza ikokore, mhogo hujipika. Uji wako utatoka ukiwa umeiva vizuri ukifuata vidokezo kwenye matayarishio yetu ya chakula cha Ikokore.

Kwa sasa kwani tuna maarifa ya kutengeneza chakula cha Ikokore, ni wakati wa kujua jinsi ya kukipakua.

Ni muhimu kufahamu kuwa Ikokore ina pakuliwa vyema na corn pap, uji wa oatmeal, ega, garri ama oats fufu.

Matayarisho haya rahisi ya Ikokore ni mazuri ya chakula cha mchana cha wikendi ama chakula cha mchana wakati wowote ule!

Soma pia: Prepare Yamarita Fries In These Easy Steps

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio