Mtoto huwa kiumbe cha kushangaza. Bila lugha lakini kwa njia moja au nyingine huweza kupitisha ujumbe. Wakiwa wametosheka wana furaha na tabasamu nyusoni mwao ila kulia na kusumbuka huwa dalili ya kutotosheleka. Mtoto kulia ovyo inaweza kuwa dalili ya mambo mengi kama tunavyoangazia.
Vyanzo Vya Mtoto Kulia Ovyo?

Kulia ni lugha moja ya watoto kote duniani. Hivi ndivyo wao huweza kudhihirisha kuwa hawajafurahia ama kuna kitu kinachowasumbua. Kulia huweza kuashiria mambo mengi na wakati mwingine huwa changamoto kujua kwa nini mtoto analia ovyo.
Mambo yanayoweza kusabababisha mtoto kulia ovyo ni pamoja na:
Hii bila shaka ni sababu ya kwanza na kuu kwa nini mtoto anaweza kuwa analia ovyo. Kwa vile watoto hawawezi sema wana njaa, wanapoanza kulia jambo la kwanza kuhakikisha ni kuwa mtoto amepata lishe. Iwapo kulia kwa mtoto kulitokana na njaa mara tu anaposhiba ataanza kuwa mchangamfu. Hivyo ni vyema kuwa na chakula tayari kila wakati.
- Magonjwa ama anahisi vibaya
Ni changamoto kwa kila mzazi kuelewa kwa nini mtoto anaweza kuwa analia. Ugonjwa ama mtoto anapokuwa kwenye maumivu ataanza kulia ovyo. Hii ni ishara kuwa kila kitu hakiko shwari. Iwapo mtoto haachi kulia ata baada ya kumwangalia ni vyema kumpeleka hospitalini kupata uchunguzi wa ziada.

Watoto wengi huweza kusumbuka sana iwapo wana usingizi. Wengi huwa wana usingizi lakini hawataki kulala hivi wanaanza kulia. Iwapo ni wakati wa mtoto kulala, anapoanza kulia mzazi anaweza kumbebeleza ili alale. Huku kulia hukoma mara tu anaposhika usingizi.
- Anaweza kuwa ameenda haja
Kulia ni aina nyingine ya kumwambia mama kuwa mtoto amejisaidia. Watoto wengi wanapoenda haja na mzazi achukue wakati kabla ya kuwabadilisha napi wataanza kulia ovyo. Hili ni kwa kuwa pia wanahisi kutokuwa sawa. Mara wanapobadilishwa wataanza kuwa wachangamfu na wenye furaha.
Mtoto pia anaweza lia ovyo akitaka mtu wa kucheza naye. Pia watoto huweza kutambua iwapo kuna mtu anayewaangalia au la. Hivi itabidi amelia ili kutafuta mama ama mzazi mwingine yeyote. Pia huwa ishara kuwa anataka mtu wa kucheza naye. Unapomchukua atanyamza na ukimweka chini ataanza kulia tu. Hii ni kuwa anahitaji mtu wa kukaa naye.
Kulia ni lugha ya watoto ulimwengu mzima. Kuwa mzazi ni kuelewa kuwa mtoto kulia ovyo ni njia ya kuzungumza. Ila kulia kunaweza ashiria mambo mengi, unapomzoea mtoto wako utaanza kuelewa kila anapolia anamaanisha nini. Vilio tofauti humaanisha mambo tofauti.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kwa Nini Mtoto Hulia Baada Ya Chanjo?