Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Mitano

Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Mitano

Watoto wa miezi mitano wanaweza kukaa chini kwa vipindi virefu vya wakati. Ili kuwasaidia kukaa kwa urahisi na bila kuchoka sana, unaweza tumia mto kuwaegemeza.

Mwezi wa tano wa maisha ya mtoto wako huwa na mabadiliko mengi. Tarajia mengi kutoka kwa mtoto wako. Ni katika mwezi huu ambapo ataanza kufanya juhudi za kuongea. Mwendo wake huenda ukaanza katika mwezi huu, kwa hivyo tarajia kumwona mtoto wako akitambaa. Jumuika nasi tunapo angazia hatua muhimu katika mtoto wako wa miezi mitano zinazo tendeka katika mwezi huu.

Mtoto wa miezi mitano: Mwendo wa mwanao

mtoto wa miezi mitano

Watoto katika umri huu wanaweza kaa chini kwa vipindi virefu vya wakati. Ili kuwasaidia kukaa kwa urahisi na bila kuchoka sana, mara nyingi wanaegemezwa kwa kutumia mto. Huenda pia ukawashika mkono wanapo kaa ili wasianguke.

Mbali na kukaa chini, huenda mwanao akaanza kujiviringisha unapo mlaza kwa mgongo hadi kulala kwa tumbo. Unapaswa kuwa makini unapo mlaza kwani anapo fanya hivi ako katika hatari ya kuanguka vibaya. Anapo shika kitu, utagundua kuwa anakishika kwa nguvu bila kuachilia. Mikono na vidole vyake vinazidi kukua na kupata nguvu zaidi.

Hatua muhimu: Usingizi wa mwanao

Watoto wanapo kuwa changa, wengi wao hulala usiku wote hata wanapo fikisha miezi mitano, ila sio wote. Ili kuhimiza mwanao kuwa na utaratibu hasa wa kulala, mwanzishie utaratibu wa kulala. Unaweza anza kwa kupunguza mwangaza chumbani chake, ili afahamu kuwa wakati wa usiku ni wa kulala. Pia, unaweza msafisha kisha kumshika kwa dakika chache huku ukimwimbia ili alale kisha umlaze kitandani. Kufanya hivi kwa muda kutamfanya azoe na ajue wakati wa kulala.

Mazungumzo yake

Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Mitano

Mtoto anapo timiza miezi mitano, huwa ameanza kujaribu kutamka maneno kwa lugha ya kitoto. Hata kama maneno haya sio hasa. Maneno kama 'ma-ma' na 'da-da'.

Mtoto wa miezi mitano: Uwezo wake wa kuona

Katika umri huu, uwezo wake wa kuona una anza kuimarika kila kuchao. Hata kama haoni kila kitu vyema, macho yanaweza kuangalia kitu kimoja kwa pamoja na kwa muda. Pia anaweza kutofautisha rangi tofauti.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo utakuwa umeanza kuona katika mtoto wako wa miezi mitano. Kumbuka kuwa watoto wanapenda muziki, kwa hivyo hakikisha kuwa unaweka muziki wa polepole na usio na kelele nyingi. Mnunulie mtoto wako vidoli vya rangi tofauti acheze navyo. Hakikisha kuwa chumba chake kiko salama na hakuna vitu ambavyo vinaweza kumwumiza.

Soma Pia: Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Minne

Written by

Risper Nyakio