Ndoa Yenye Mafanikio Kati Ya Mwanamme Wa Asia Na Mke Wake Kutoka Afrika

Ndoa Yenye Mafanikio Kati Ya Mwanamme Wa Asia Na Mke Wake Kutoka Afrika

Mwanamme huyu mchanga kutoka Asia alipatiana hadithi yake jinsi alivyo kubali mwanamke kutoka Afrika ilivyo fanikiwa. Hadithi hii ina mafanikio.

Hakuna kitu kizuri kama hadithi ya nzuri ya mapenzi inayo tangazwa duniani kote ili kumfanya kila mtu apate hisia. Wiki iliyo pita katika Subtle Asian Traits kikundi cha mtandao wa kijamii wa Facebook, nyumba ya mtandao ya mamilioni wa watu wa Asia, kijana mchanga aliwajulisha watu hadithi yake ya mapenzi na ndoa yenye mafanikio.

Clarence Tan aliye funga ndoa alisema kuwa yeye ni mtoto wa mama kutoka Singapore na baba kutoka Hongkong na bibi yake kwenye jina Sophia ni mzaliwa wa Ghana, Afrika Magharibi. Walakini, uhusiano wao haukuwa rahisi. Kufuatia babake Tan kuto taka kuwa bariki wawili hawa katika uhusiano wao. Katika ujumbe wake Facebook, Tan alielezea matatizo aliyo kumbana nayo.

Babake Tan Haku Kubaliana Na Uhusiano Wa Wachumba Hawa

Tan alisema kuwa baadhi ya vitu ambavyo babake alimwambia vili mwumiza roho.

Kulingana na Tan, babake alifikiria kuwa tofauti za kitamaduni zingewafanya wapigane sana. Na babake akadhani kuwa jambo hilo lilikuwa mbaya kwa ndoa. Babake pia alisema kuwa uhusiano wao ungekua mbaya kwa biashara. Hasa kama angekuwa anafanya kazi Asia. Kwa sababu hizi, babake Tan alimwambia asingoje baraka zake. Alimwambia kuwa asitarajie kumwona katika harusi yao.

Mapenzi sio kitu chochote usipo sisitiza

Clarence Tan alieleza jinsi walivyo kuwa na vita vingi na Sophia kufuatia uhusiano uliokuwa ukidhoofika na babake. Walakini, alikuwa ameamua kuifanya familia yake imkaribishe. Ange mhimiza mchumba wake kuja kuitembelea familia yake. Kadri wakati ulivyo zidi kusonga, Tan alisema kuwa familia yake ilimkubali baada ya kugundua kuwa alikuwa na moyo mkunjufu, mwenye heshima zake, mwenye mapenzi na mpole.

Ndoa Yenye Mafanikio Kati Ya Mwanamme Wa Asia Na Mke Wake Kutoka Afrika

Picha: Bwana Tan kupitia Facebook

Wanandoa hawa mwishowe walifunga pingu cha za maisha baada ya miaka tatu ya kuchumbiana. “Ilikuwa asilimia 100 vigumu,” Tan alisema, ila yeye ndiye niliye chagua.

Tan pia alisema kuwa hajai iona familia yake ikiwa na furaha zaidi ya alivyo iona siku ya harusi yake.

Ndoa Yenye Mafanikio Kati Ya Mwanamme Wa Asia Na Mke Wake Kutoka Afrika

Picha: Mr Tan Via Facebook

Soma ujumbe wake wa Facebook hapa chini:

ndoa yenye mafanikio

ndoa yenye mafanikio

Ndoa Yenye Mafanikio Kati Ya Mwanamme Wa Asia Na Mke Wake Kutoka Afrika

Jinsi ya kuwa na ndoa yenye mafanikio ilhali mchumba wako ni wa nchi ama sehemu tofauti

Vidokezo hivi vitakusaidia kukuza uhusiano wako na mchumba wako kutoka nchi nyingine. Kwa bahati njema kama Tan, mtaweza kukumbana na changamoto zenu na hata kufanya harusi. Tuna kutakia mema.

Mambo yakiwa magumu zaidi, kuwa mzuri na mkarimu

Changamoto hukuwa katika uhusiano wowote ule. Ni vigumu kuuepuka kwa sababu uhusiano una watu wawili tofauti pamoja na vitambulisho tofauti, ambalo ni jambo nzuri. Jambo muhimu ni jinsi unavyo tatua matatizo yenu. Wachumba wanapaswa kuwa na heshima kwa kila mmoja wanapo kumbana na matatizo yao. Huenda wakafikia hatua mpya kwa kuelewana. Utafiti una dhihirisha kuwa wachumba kutoka tamaduni ama nchi tofauti huchukua mkono wa mapenzi wanapo kumbana na matatizo na jambo hili huwafanya wawe na utangamano zaidi.

Kumbuka kuwa Mimi + Mimi = Sisi

Ni jambo moja kwa watu wawili kukubaliana kuwa wako katika uhusiano pamoja, na jambo tofauti kwa wawili hawa kuwa kitu kimoja. Wachumba wanapo jiona kama kitu kimoja wenye hadithi sawa na moja, wame dhihirisha u-sisi wao. Wanandoa wanaweza kuwa na u-sisi wao wa kisiri kati yao ama hata kwa umma ama zote mbili.

Tizama urembo ulioko katika tofauti zenu

Tofauti kati ya wachumba huenda ukawa mwingi baadhi ya nyakati. Hii ni bahati mbaya kwa sababu huenda tofauti zenu zikawa za vitu vingi. Na kwa wanandoa kutoka pande tofauti za nchi, huenda wakawa na tofauti za kitamaduni na njia ya maisha na wanavyo fanya vitu tofauti.

Msikize mchumba wako kwa makini

Ni vyema kuelewa tamaduni na njia ya maisha ya mchumba wako. Wakati wote hakikisha kuwa unamsikiza mchumba wako na kufanya yote uwezavyo ili uhusiano wenye uwe na mafanikio.

Soma pia: 10 Relationship Goals That Will Make Your Love Stronger

Written by

Risper Nyakio