Dalili za mimba huwa tofauti kati ya wanawake. Huku wengine wakiwa na kichefuchefu kingi katika wiki za kwanza chache, wengine hawasumbuliwi na hali hii. Kukosa hedhi na mimba huhusiana kwa sana. Kukosa hedhi huwa dalili ya kwanza ya mimba kwa wanawake wengi. Je, kukosa hedhi huwa ishara ya mimba wakati wote?
Hedhi na Mimba

Hata kama kukosa hedhi kunafahamika kuwa ishara kuu ya ujauzito, kuna sababu zingine ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukosa hedhi. Mambo kama vile:
- Kusafiri
- Kubadili mazingira
- Kukwazwa kimawazo
- Kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida
- Kuwa na matatizo ya kiafya
Wanawake wengi pia hushangaa iwapo kuna uwezekano wa kushika mimba wanapokuwa katika vipindi vya hedhi. Jibu ni ndiyo na la, kulingana na mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Kwa kawaida, sio rahisi kwa mwanamke kushika mimba anapokuwa na hedhi. Kwa wanawake walio na vipindi vifupi vya hedhi, ni rahisi kwao kushika mimba. Manii yana uwezo wa kubaki hai kwa kipindi cha siku 7. Kufanya mapenzi siku ya mwisho ya hedhi huenda kukawaweka katika hatari ya kushika mimba katika hedhi.
Dalili za kwanza za mimba

- Kutapika mara kwa mara
- Kuhisi kichefuchefu
- Utoaji wa damu nyepesi (damu ya implantation)
- Kukosa kipindi cha hedhi
- Kuhisi kufura tumbo
- Tumbo kujaa gesi ama hewa
- Mhemko wa hisia
- Kuhisi uchovu hata unapoamka
- Maumivu ya mgongo
- Kuhisi kwenda msalani mara kwa mara
- Kuumwa na chuchu
- Kulala sana kuliko ilivyo kawaida
Kuvuja damu katika mimba
Kushuhudia damu ya ovulation ni kawaida katika mimba. Damu hii huwa tofauti na damu ya hedhi. Damu ya hedhi huwa nyingi wakati ambapo damu ya implantation huwa nyepesi. Wakati ambapo damu ya hedhi hujaza pedi baada ya muda, damu ya implantation haijazi pedi. Rangi ya damu ya hedhi huwa nyekundu iliyokolea, huku ya implantation ikiwa ya hudhurungi na nyepesi zaidi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mimba Ya Miezi Mitatu: Kinachofanyika Mwilini Na Mambo Ya Kutarajia